Nini maana ya hisa?!

Nguyaki

Member
Jan 3, 2013
91
22
Habari wa Jf,
Naomba kwa wanaofahamu maana ya hisa.
Nimekuwa naskia mtu anauza HISA kwenye kampuni au Bank
Pia saccoss wanasema sana kuhusu hisa,what is it?
 
Salaam,

Naomba fuatilia hapa then uulize lolote kuhusu hisa kuanzia hapo mkuu.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-biashara-na-uchumi/570244-msaada-jamani.html

Mjadala huu tuliuendesha hapa jukwaani.

Deus.

Asante sana mkuu,
Nimeelewa kwa sehemu
Kwamba HISA au share ni pesa zako unazowekeza kenye kampuni ili upate
gawio katika muda mliokubaliana kama ni mwezi au mwaka.pia unakuwa sehemu
ya umiliki wa kampuni ile(japo sijaelewa vizuri hapo,kama ni kwenye vikao vya kampuni?).
Hebu nieleweshe hizo hisa zinazouzwa 250,500 nk,bila shaka moja haitatosha wewe kupata
gawio.sasa ngapi inatosha kupata gawio angalao 1%?
Kama mwanahisa unapaswa kushirikishwa faida inapoongezeka au unapewa ile mliokubaliana
awli?Hisa lazima iwe pesa tu au yaweza kuwa kitu kingine?mambo gani ya msingi mwanahisa
anapaswa kushirikishwa?
 
Asante sana mkuu,
Nimeelewa kwa sehemu
Kwamba HISA au share ni pesa zako unazowekeza kenye kampuni ili upate
gawio katika muda mliokubaliana kama ni mwezi au mwaka.pia unakuwa sehemu
ya umiliki wa kampuni ile

Niyo, unakuwa sehemu ya umiliki wa kampuni kulingana na idadi ya % ulizo nazo kwenye kampuni. Kila kampuni itaweka utaratibu wao ni hisa ngapi unapaswa kuwa nazo ndipo uruhusiwe kuingia kwenye vikao vya bodi ya wakurugenzi au utaendelea kubaki kuwa mwana hisa na kimsingi vikao vya wana hisa vinakuwepo kwa kadri mtakavyoamua.

(japo sijaelewa vizuri hapo,kama ni kwenye vikao vya kampuni?).
Hebu nieleweshe hizo hisa zinazouzwa 250,500 nk,bila shaka moja haitatosha wewe kupata
gawio.sasa ngapi inatosha kupata gawio angalao 1%?

Kwenye soko la hisa la kampuni yoyote hilo ni suala la msingi sana kuangalia. Hii inategemea na mtaji wa kampuni, kwa mfano kama kampuni ina mtaji wa 10billion, ili upate gawio la 1% ni lazima ununue hisa zenye thamani ya 10million.

Kama mwanahisa unapaswa kushirikishwa faida inapoongezeka au unapewa ile mliokubaliana
awli?

Faida/Gawio huendana na mafanikio ya kampuni siyo fixed, kwa maana nyingine unaweza kupata eg.2million kwa miezi 6 lakini baadaq ya miezi 6 ukapata 7million kulingana na faida na kukua kwa kampuni. Pia guarantee ya kutokupoteza hisa zako inachukuliwa na kampuni husika.

Hisa lazima iwe pesa tu au yaweza kuwa kitu kingine?

Mara nyingi makampuni huuza hisa (Contract) ili kupata fedha ambazo kimsingi zitaisaidia kampuni kupiga hatua zaidi (Kuweza kuwahudumia wateja wake kwa wingi,ufanisi na ubora zaidi. Kampuni nyingine huweza kubadilisha hisa na vipande vya dhahabu (kulingana na gharama ya dhahabu kwa siku husika). Sijawahi kusikia kampuni ikichukua mali nyingine badala ya fedha.

mambo gani ya msingi mwanahisa
anapaswa kushirikishwa?

Kimsingi mwanahisa anapaswa kujua kinagaubaga mapato na matumizi ya kampuni kupitia mkutano mkuu wa wanahisa ambao kimsingi hufanyika kila mwisho wa mwaka na Management/Bodi ya wakurugenzi huwa tayari kujibu maswali ya wanahisa.

Naamini nitakuwa nimejaribu kukupa japo mwanga ktk suala hili
 
Back
Top Bottom