Nini maana ya hakimiliki?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Nini maana ya hakimiliki.png

Hakimiliki ni utaratibu wa kisheria unaompa mmiliki wa kazi za akili haki ya kuamulia matumizi yake. Sheria za hakimiliki zinalenga kukinga watungaji wa kazi za akili dhidi ya matumizi ya kazi yao na wengine wanaojipatia faida kwa njia hiyo bila kumzingatia mtungaji anayeweza kukosa ruzuku kutokana na kazi yake.

Chini ya sheria za hakimiliki, kazi ya kiakili inaweza kunakiliwa pekee ikiwa mmiliki anatoa ruhusa. Ikiwa mtu ananakili kazi bila kibali, anakiuka hakimiliki.

Kutegemeana na sheria za nchi mbalimbali mkiukaji anaweza kushtakiwa chini ya sheria za biashara au wakati mwingine sheria za jinai. Mkiukaji anaweza kuhukumiwa kulipa fidia au hata kwenda jela. Kwa kawaida, sheria za hakimiliki hulinda haki za watungaji na warithi wao kwa kipindi fulani, katika sheria ya kimataifa angalau hadi miaka 50 baada ya kifo cha mtungaji. Nchi mbalimbali huwa na vipindi virefu zaidi.

Katika nchi zinazofuata zaidi sheria za Marekani kuna kanuni zinazorahisisha kampuni kushika hakimiliki badala ya wafanyakazi wake kama kazi ilitekelezwa ofisini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom