Nini maana ya Ashakum si Matusi?

Muugwana anapotaka kusema jambo na akajikuta hakuna jinsi ya kuyafanyia stara au kukwepa maneno anayo taka kuyatamka,hutaka radhi kabla kutamka yale maneno...ndio anatanguliza ashakum si matusi,yaani uniwie/mniwie radhi kwa nitakayo sema.
 
We Bu'yaka vipi, mbona mbishi sana?
Wewe utaita ubishi, mimi nasema ni mtu anaependa kuelewa vitu kwa undani.

Wengi mmeelewana maana ya msemo huo "ashakum si matusi."

Mimi nilitaka kuelewa "ashakum" ni nini.
 
Binafsi kiujulma nimeridhishwa na fasili na maana zilizoelezwa. isipokuwa kwa kuongezea tu ni kwamba, waungwana wanapozungumza hutumia neno la ashakum si matusi anapotaka kuzungumza neno ambalo katika hali ya kawaida ni tusi na huwezi kulitamka tu kama nyanya. Ashakum si matusi inapotangulia katika sensi haina maana ya kuomba msamaha bali huwa na maana ya kutaka kuzungumza nebno zito la matusi katika hali ya kiungwana
 
haina maana ya kuomba msamaha bali huwa na maana ya kutaka kuzungumza nebno zito la matusi katika hali ya kiungwana
Kuna uungwana katika matusi?

"Ashakum si matusi, alikuwa amevaa gagulo linaloonyesha kumma."

Nimefanya uungwana hapo?
 
Naamini Bu'yaka ameshaelewa maana ya matumizi ya hilo neno bali alitaka tu kurefusha huu uzi! nawashukuru wadau kwa kuwa wavumilivu
 
"Ashakum" (Ash'kum) si Matusi = "Pardon me" is not an insult.

Ashkum: excuse me, forgive me.
 
Kama kwenye hiyo mikazo ndimo unamomaanisha nimechanganya,
Unayo matatizo makubwa sana na wakuweza kukuelewesha kwa umbumbu huo sijui ni Mwalimu wa wapi.
Herufi kubwa hazitumiki katikati ya sentensi isipokuwa kwa majina ya watu.Hukwenda shule?

Usikubali kukaririshwa, "ashakum si matusi." Ashakum ni nini, hujui!
 
Herufi kubwa hazitumiki katikati ya sentensi isipokuwa kwa majina ya watu.Hukwenda shule?

Usikubali kukaririshwa, "ashakum si matusi." Ashakum ni nini, hujui!
Ulishindwa kuwaelewa walimu wako,
Ina maana hata wazazi wako walikuwa hawafuatilii na kuona kuwa huwa unaandika Madudu?

Dah! unatia aibu.
Narudia kuandika nilichoanika;
Walimu wana Kazi kwelikweli.

Kama wewe unaechanganya herufi kubwa na ndogo, mwalimu alikushindwa kabisa.
 
..Binafsi nimeelewa matumizi ya hiyo sentensi lakini pia naona hoja ya ndugu Bu'yaka..kwa kusoma tu maoni yake nae pia ameelewa matumizi ya hili neno anachotaka kujua zaidi ni maana ya hilo neno moja tu yaani "Ashakum" je hilo neno ndio lina maanisha niwie radhi/samahani au ni sentensi nzima. Lakini pia kwa ufahamu wangu sentensi ashakum si matusi inatumiaka tu pale ambapo neno ambalo kwa mazingira ya kawaida lingekuwa tusi linapokosa tafsida! Mfano aliotoa Bu'yaka...ashakum si matusi! alikuwa amevaa gagulo linaloonesha ku..m..Ki ukweli kwa kuwa neno "kum" lina tafsida yake ambayo inaweza kuwa ni "sehemeu za siri" kutumia ashakum si matusi ili tu uweze kusema neno "kum" kwenye sentesi hii..si sawa kabisa maana bado msemaji angeweza sema.." gagul;o linaloonesha sehemu za siri". Kwa ufahamu wangu msemaji wa sentensi hiyo angehalalisha matumizi ya ashakum si matusi kama angesema.." Ashakum si matusi, alikuwaa amevaa gagulo lililoonesha uchi wake!
 
Maana yake niwie radhi kwa nitakayosema.

Sina nia mbaya kutumia neno baya ninalokwenda kulitamka, nia yangu ni njema.
 
Back
Top Bottom