Nini maana halisi ya maneno haya? Je, yanastahili kuingizwa kwenye kamusi kwa jinsi yalivyomudu kubaki kwenye matumizi?

nasrimgambo

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
1,858
2,348
maneno kama vile;

magumashi

miyeyusho

shobo

jau

sanua (mfano; kimesanuka, imesanuka, 'mange kimambi kakisanua huko')

haya maneno yanafahamika sana ila sidhani kama wengi tunafahamu namna ya kuelezea kiundani yanamaanisha nini, sasa wanaojua kiswahili kizungumzwacho dar, tuambieni maana halisi ya maneno hayo, na je yanastahili kutiwa kwenye kamusi?

ongezea na wewe maneno yako.
 
Endapo toleo jipya la kamusi ya kiswahili itaandaliwa, maneno hayo yanaweza ingizwa au la kulingana na kupokewa na kudumu kwake ktk jamii.
Hiyo ni misimu
Hapo upo mwana?
 
Endapo toleo jipya la kamusi ya kiswahili itaandaliwa, maneno hayo yanaweza ingizwa au la kulingana na kupokewa na kudumu kwake ktk jamii.
Hiyo ni misimu
Hapo upo mwana?
hiyo misimu ipo pengine hata miaka kumi imepita tangu nimeanza kuisikia, bado tu ni msimu! na haijaqualify kuwa maneno rasmi, how comes!
 
Magumashi-Hili hutumika ktk hali ambayo jambo limefanyika ktk hali ya udanganyifu,mfano;Umenunua bidhaa ya shilingi laki moja unapewa risiti iliyoandikwa elf ishirini hapa tunasema risit ya magumashu
 
hiyo misimu ipo pengine hata miaka kumi imepita tangu nimeanza kuisikia, bado tu ni msimu! na haijaqualify kuwa maneno rasmi, how comes!
Samahani mkuu.

How comes✖

How come ☑

Kamusi ya kiswahili inahusu kiswahili sanifu.
TUKI hufanya utafiti ili kujua namna watu wanavyoyatumia maneno mapya. Hufanya michakato yao(wataalamu watatujuza zaidi) mingine hadi neno linangizwa kwenye kamusi.

Misimu hata itumike kwa kiasi kikubwa kiasi gani haiwezi kuwa sehemu ya msamiati wa lugha sanifu hadi hapo wana isimu jamii watakapiliingiza kwenye kamusi(niko tayari kuelimishwa nilipokosea)
 
Back
Top Bottom