Uchaguzi 2020 Nini maana CCM kuwashirikisha Wasanii katika Kampeni? Je, ni uzalendo?

scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,619
2,000
Habari zenu wadau,

Kipindi kampeni zikiendelea kushika kasi kuna kitu kusema ukweli sisi kama Watanzania tuna tafakari mara mbili mbili hasa aina ya kampeni zinazofanyika na chama cha CCM.

Kumekuwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, wasanii wa maigizo ambao wameshirikishwa kushiriki katika kampeni za CCM lakini ukitazama kwa jicho kali maana ya maudhui ya kazi zao za sanaa za kila siku wengi wao zimejaa mapenzi na kauli zenye ukakasi kusikiliza au kutizama pia maisha yao mfano hao bongo movie ni maisha ya kihuni na skendo zisizoisha.

Leo hii tunapokuja kufanya kampeni za chama lazima utamaduni na desturi za Kitanzania zisambazwe kwa njia ya sanaa kwani inakutanisha Watanzania wote na tunaangalia mustakbali wa maisha yetu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Kwann inatumia pesa nyingi kulipa vikundi hivi ambavyo kwa baadhi yao kazi zao haziendani na utamaduni wa Mtanzania?

Je, hawa wenyeviti wa CCM kila mkoa na wilaya wana kazi gani?

Kwenye vyuo kuna wataalamu wa siasa ambao wamesome fani ya siasa kwanini wasishirikishwe katika kampeni za CCM ili sisi Watanziania tupewe madini ya kisiasa kuliko kila siku kuwatazama kina zuchu, Ali Kiba, Aunt Ezekiel, Wema Sepetu na wengineo.

Kuna vikundi vya ngoma za kitamaduni, sarakasi, ngonjera na mashairi ambao wanaakisi utamaduni wa Mtanzania moja kwa moja katika kazi zao kwa nini hawashirikishwi kwenye kampeni za Chama cha Mapinduzi?

Hakika picha mnayotupa sisi watanzania ni kwamba CCM mnatuona sisi ni wapumbavu sana kwa kutumia makundi haya ya sanaa yasioyokuwa na tija kwetu.

Haya yote ipo siku yatafika mwisho.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,844
2,000
Wasanii ni wapiga kura .kushirikisha mpiga kura na kumobilize wapiga kura aina zote ndio kampeni yenyewe
 
scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,619
2,000
NINI MAAANA YA CHADEMA KUWAWEKA WASANII KAMA AKINA SUGU, PROFESA J KWENYE SIASA HADI KUWALUHUSU KUGOMBEA UBUNGE HADI WAKASHINDA?????
Je Sifa za kugombea ubunge katika jamhuri ya muungano unazijua mkuu?
Kuna sanaa na sifa za mgombea tofautisha na kinachoendela sasa katika kampeni za ccm maana kuna makundi yanakula pesa zetu na hayana tija kwa chama cha mapinduzi na hata kwa watanzania.
Kama unabisha baada ya uchaguzi 2015 wasanii walipata nini kwa ccm katika miaka mitano?
 
scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,619
2,000
Wasanii ni wapiga kura .kushirikisha mpiga kura na kumobilize wapiga kura aina zote ndio kampeni yenyewe
Kwahiyo mkuu nafasi za wenyeviti wa chama kila mkoa na wilaya ambao wanaunganisha chama hazina maana na hawa watu wanakula mishahara ya bure maana kazi zao zinafanywa na wasanii tu
Kuna tatizo hapo
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,089
2,000
Yaitwa ghiliba hiyo mkuu.

Hata kama wavuta bangi wanaweza saidia watajipanga nao.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,844
2,000
Chadema wanadharau sana wapiga kura ndio maana media wanawakimbia ,wasanii wanawakimbia,viiongozi wa dini wanawakimbia nk wao msanii sio mtu na si mpiga kura hatakiwi kuweko mkutano wa kampeni akiwepo kosa kwa nini awepo very funny chadema 2015 Chadema walijaza wasanii mikutano ya kampeni Leo wanawaona hopeless
 
Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,157
2,000
Je Sifa za kugombea ubunge katika jamhuri ya muungano unazijua mkuu?
Kuna sanaa na sifa za mgombea tofautisha na kinachoendela sasa katika kampeni za ccm maana kuna makundi yanakula pesa zetu na hayana tija kwa chama cha mapinduzi na hata kwa watanzania.
Kama unabisha baada ya uchaguzi 2015 wasanii walipata nini kwa ccm katika miaka mitano?
SASA KWA NINI CHADEMA NAO WANAWATUMIA WASANIII KAMA CCM TENA??
 
Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,157
2,000
Inaelekea uwezo wa kuelewa mada ni mdogo sana au haupo kabisa.
HAAA HAAA. TULIENI MKIJIBIWA MAIGIZO YENU NA MAPROPAGANDA YENUU. WASANIII NI WATANZANIA KAMA WATU WENGINE. KINACHOWAKEREKETA NYIE CHADEMA NIKUONA WASANII MAARUFU INCHINI KUTUMIKA KWENYEKAMPENI ZA CCM. ILA HAOHAO WASANIII WANAOINADI CCM LEO WAKESEMA WAGEUKIE KWENU CHADEMA MATAWAITA MAKAMANDA HATAKABLA HAWAJACHUKUA KADI ZA CHAMA CHENUU. ACHENI NONGWA WASAANIII WANAHAKI ZOZE KIUCHUMI KISIASA NA KIUTAWALAA.
 
Mkuu tuachane na hayo kwani kuna wasanii wanaojitolea katika kampeni hizi??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom