Nini logic ya kusoma Magazeti Redioni na kwenye TV?

Baba Heri

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
1,503
2,222
Kwa hali ya teknolojia ya habari na mawasiliano ilivyo kwa sasa hapa Tanzania ni rahisi sana kupata habari kupitia Redio, TV, magazeti na Mitandao ya Kijamii.

Najiuliza kama mchapishaji gazeti analenga kufanya biashara kwanini anakubali media nyingine ziwasomee wateja wake kilichochapwa kwenye gazeti lake, ataliuzaje?

Mimi naamka asubuhi kabla sijatoka nyumbani nimeshasomewa magazeti yote tena kwa kubembelezwa kuitwa mpenzi msikilizaji, napata wapi hamu ya kununua gazeti?

Maana kuna watangazaji wengine wanasoma habari halafu wanaichambua kuliko gazeti lenyewe nisipotosheka na uchambuzi naingia mitandaoni, gazeti sikutani nalo kabisa labda kwenye maandazi.

Nawashauri mfikirie upya huu utaratibu wa kuchapa magazeti na kutusomea bure.
 
wanaruhusiwa kusoma vichwa vya habari(kurasa za mbele na nyuma tu) haina tofauti na tunavyolundikanaga vituo vya kuuza magazeti ili kusoma kurasa za mbele.. namna zote zinavuta wateja. Shida kwa redioni wanasoma kichwa halafu wanachambua kwa kuweka taarifa husika toka chanzo chao wao!
 
Back
Top Bottom