Nini kitatokea endapo serikali itapandisha vigezo vya kusoma elimu ya juu? Je, kutakuwa na athari gani ktk jamii kiuchumi?

Tatizo lako kuna majibu unayoyataka wewe, hatupo kwenye hisabati kwamba kila utakayemuuliza 2+2=4, tegemea maswali, na hoja kinzani kutoka kwenye swali lako na ukiweza kuelewa maelezo ya wote hapo tutakuita muerevu
Mnacho kifanya wewe na wenzako ni kureact na sio kujibu kilichoulizwa, chukulia mimi sijui kitu nmekuuliza hilo swali ili nijifunze halafu wewe unaanza kujibu vitu ambavyo sijakuuliza
 
Mnaiita elimu ya bongo mbovu ni kweli ni mbovu maana umeshindwa kuelewa swali dogo kama hili
Itoshe kusema wewe jamaa ni pimbi sana, nimepitia comment huna uwezo wa kujenga hoja ni mtu wa kuattack kwa wanaotoa majibu tofauti na matarajio yako

Yaani wewe isingepaswa watu wasihangaike kukujibu
 
Tuna shida kubwa kwenye mfumo wa elimu. Achana na vitu vya kitoto kitoto kwa sasa. Tuzungumze mambo ya maana yanayohusu elimu yetu inayoteketea
 
Watakaopata elimu ya juu watakuwa kidogo sana lkn wafanyakazi NECTA watakuwa matajiri.
 
Ahsante mkuu kwa jibu lako zuri wengi wanajibu vitu ambavyo sijawauliza big up mkuu,

Je kuna athari gani za kiuchumi zitatokea?
Kwa vyuo binafsi vitashindwa kujiendesha na kupelekea kufungwa, maana kama hamna wanafunzi hakuna haja ya kuendelea kufanya hiyo biashara, ina maana tutakuwa tumeongeza idadi kubwa ya watu wasiokuwa na ajira mtaani.

Kwa serikalini sina uhakika lakini kama hali itaendelea kuwa mbaya kwa muda mrefu wafanyakazi wa kudumu wanaweza kuhamishwa kwenda sekta nyingine, bado kutakuwa na upungufu wa ajira na kipato kwa taifa maana hivyo vyuo pamoja na kufundisha huwa vinafanya tafiti na kazi mbalimbali kwa jamii zinazoajiri baadhi ya watu kwa mikataba ya aina mbalimbali zaidi ya wale wa kudumu.

wataalamu wa uchumi ndio wanaweza kutufafanulia athari nyingi zaidi !
 
Mnacho kifanya wewe na wenzako ni kureact na sio kujibu kilichoulizwa, chukulia mimi sijui kitu nmekuuliza hilo swali ili nijifunze halafu wewe unaanza kujibu vitu ambavyo sijakuuliza
Kukataa majibu inamaana umeelewa kilichojibiwa na wewe kuna majibu unayataka, sisi wengine hatujataka kujibu kama unavyotegemea kwa sababu wazo la namna hiyo halifai hatutakiwi kufikia huko, watu waelimishwe wengi zaidi kujadili hasara au faida ni sawa na kupendekeza jambo hilo lifanyike
 
Mara ya mwisho nafatilia nchini England kwenda University unapaswa uwe na A tano (5) wanaita AS LEVEL... sijui kwa sasa ipoje.
Serikali ya awamu hizi kuanzia JK, JPM, SSH wamefanya mazuri kwenye sekta ya ELIMU tuwapongeze lakini kwenye elimu ya juu kwa maana ya High school, vyuo vya kati na vyuo vikuu kuna usingizi mzito zaidi ya ule wa pono.
Kuna wilaya hazina High school hata moja.
Admission capacity ya vyuo vyetu ni ndogo sana.
Wadau wa elimu woote wahusishwe vyuo vijengwe hasa vya ufundi
 
Wakuu hili swali nimeliuliza sehemu nkashindwa kupata majibu nimeona nililete hapa.

Nini kitatokea endapo serikali itapandisha vigezo vya kusoma elimu ya juu? Je kutakuwa na athari gani ktk jamii kiuchumi?

Mfano alama za kujiunga chuo ziwe atleast BBB

Nashauri wapandishe tuu Mkuu,
Sababu Wanaokwenda Elimu ya Juu wamekuwa wengi Mnooo na Hakuna Ajira,Wapandishe ila waongeze Kujenga Vyuo vya Kati kwa Fani za Mikono,Veta,Technical college za Kutosha ili Nchi ipae Kimaendeleo,Ipunguze white colour jobs
 
Mara ya mwisho nafatilia nchini England kwenda University unapaswa uwe na A tano (5) wanaita AS LEVEL... sijui kwa sasa ipoje.
Serikali ya awamu hizi kuanzia JK, JPM, SSH wamefanya mazuri kwenye sekta ya ELIMU tuwapongeze lakini kwenye elimu ya juu kwa maana ya High school, vyuo vya kati na vyuo vikuu kuna usingizi mzito zaidi ya ule wa pono.
Kuna wilaya hazina High school hata moja.
Admission capacity ya vyuo vyetu ni ndogo sana.
Wadau wa elimu woote wahusishwe vyuo vijengwe hasa vya ufundi
Ahsante mkuu kwa maoni yako,
 
Elimu kwa sasa ni biashara kama zilivo biashara zingine,,

Ukipandisha alama za ufaulu utafanya bidhaa(Wanafunzi) wapungue na biashara kudorora..

Vile vile nchi wasomi watapungua sana japo hata waliopo hawana msaada saaaana..

Nafikiri Elimu ya ufundi stadi ipewe kipaumbele sana kuliko hii ya kukariri vitu zaidi
 
Kuna athari gani za kiuchumi?
 
Wakuu hili swali nimeliuliza sehemu nkashindwa kupata majibu nimeona nililete hapa.

Nini kitatokea endapo serikali itapandisha vigezo vya kusoma elimu ya juu? Je kutakuwa na athari gani ktk jamii kiuchumi?

Mfano alama za kujiunga chuo ziwe atleast BBB

Niliingia UDSM mwaka 1995 nadhani hakuna aliyeingia Fuculty of Engineering akiwa na pungufu ya CCB. Muhimbili nako ilikuwa the same hivyo siyo kitu cha kushangaza
 
Athari zitakuwepo Kwanza kwa vyuo vyenyewe kwa maana vitashindwa kudahili wanafunzi kwa vigezo hivyo vilivyowekwa kwahiyo vyuo hasa vya binafsi ambavyo kwa kiasi kikubwa vinategemea idadi kubwa ya wanafunzi ndo pona yao kwa maana ya kupata pesa nyingi kwahiyo watakosa pesa ambazo zingetumika kufanyia Mambo mbalimbali ya kimaendeleo ktk vyuo husika, hata hivyo pia Kuna watu watakosa kazi hapo vyuoni hivyo kupelekea hata hizo nafasi chache za ajira nchini kukosekana. Pia hii itapelekea tatizo huko miaka ya mbeleni kabisa ambayo kwa kufikiri kawaida itaonekana Kama vile hicho kitu hakitotokea nacho kuwa na idadi ndogo zaidi ya waliosoma kufika vyuoni ambao hao wanaweza kutupa matokeo yasiyobadilika kwani hakutakua na Mambo mengi mapya yatakayofanyika kwa kuwa tu kwani wanaoshikilia mamlaka ni hao hao tu miaka yote hivyo watakosa maono kwa kiasi kikubwa namna gani Kama nchi inatakiwa kuwa na vyanzo vingi vya kujipatia Fedha,Mana idadi kubwa ya wasomi nao inasaidia kwa kuleta mawazo mbalimbali yanayoweza kusaidia kubuni njia nyingi za kupata pesa. Binafsi nafikiri zaidi kilichomuhimu ni kufundisha watu hasa wasomi namna ya kufanya jambo/kitu/kazi hi itasaidia kwa kiasi fulani...SIKU ZOTE KAMA HUTAKI KUHARIBU JAMII KWA VITA BASI WALA USIHANGAIKE SANA KUWALAZIMISHA KWA MTUTU WAKUTII, BALI UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUHARIBU NA KUITAPANYA HOVYO HOVYO MIFUMO YAO YA ELIMU, KWA HAKIKA HIYO NDO NJIA RAHISI YA KUUA CHACHU YA KUTAKA KUJARIBU VITU VYA KIMAENDELEO...
 
Back
Top Bottom