Nini kitatokea endapo Rais atashindwa kutimiza majukumu yake kutokana na tatizo la Afya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Endapo Baraza la Mawaziri litaona; kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili, laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili, hawezi kumudu kazi zake.

Baada ya kupokea azimio kama hilo, Jaji Mkuu atateua Bodi ya utabibu ya watu wasiopungua watatu atakao wateua kutoka miongoni mwa mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matabibu ya Tanzania, na Bodi hiyo itachunguza suala hilo nakumshauri Jaji Mkuu ipasavyo, nayeaweza, baada ya kutafakari ushahidiwa kitabibu kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais, kutokanana maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake.

Na iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na yaliyomo katika ibara ndogo ya (5) yatatumika.

Ibara ndogo(5) inasema: Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya Wabunge wote.
 
Back
Top Bottom