Elections 2010 Nini kitafuata baada ya hapa??

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Uchaguzi umeisha ,kura zimeibiwa live, kila mtu kaona kura zimeibiwa na Chadema hawajakubaliana na huu wizi , sasa kitu gani au hatua gani zitachukuliwa? mpaka sasa hivi sijui kwamba DR ametoa kauli yoyote baada ya NEC kukataa ombi lake na hatimaye wamemtangaza mtu wao wanayemtaka. so what next...maoni yako please!!!
 
Chadema wamepata wabunge wengi na madiwani hivyo ni lazima mapambano yahamie katika sehemu husika yaani bungeni na kwenye halmashauri.
Ni lazima tukubali kuwa hakuna la kufanya zaidi na ni lazima Slaa awpe moyo watu wake walioshinda na asifadhaike.
Sheria inasema matokeo ya rais yakitangazwa hapingwi tena na CHADEMA ni lazima tujionyeshe kuwa ni watu wa kufuata sheria mpaka hapo tutakapoweza kuzibadilisha.
SLAA jitokezi kabla hatujapoa!!!!!!
 
Bungeni kwenyewe ni kuhakikisha anachaguliwa SPIKA mwadilifu na makini na si wa kuzima hoja na mijadala!
 
... Sheria inasema matokeo ya rais yakitangazwa hapingwi tena na CHADEMA ni lazima tujionyeshe kuwa ni watu wa kufuata sheria mpaka hapo tutakapoweza kuzibadilisha. ...

Jibu ndio hilo. Uzuri sauti ya umma imesikika; CCM waipuuze kwa ujinga wao wenyewe. Hata ukichakachua matokeo huwezi kuchakachua dhamira ya wananchi ya kutaka kuung'oa mfumo wa kifisadi na kujenga misingi ya taifa thabiti kiuchumi, kijamii na kisiasa. Slaa ameshaingia katika historia ya nchi hii kama mtu aliyeleta mageuzi ya kweli (a true statesman). Kuingia Ikulu si kigezo kikubwa kama hicho alichofanya. Mafisadi/Mamafia wanao uwezo wa kumweka yeyote hata asiye na uelewa au mpuuzi ndani ya Ikulu. Kumbuka Mobutu na Marekani. Sasa mapambano yaendelee viwanjani (bungeni + halmashauri) kwa kishindo zaidi ili waelewe wenye nchi yao wako macho masaa 24!
 
Jibu ndio hilo. Uzuri sauti ya umma imesikika; CCM waipuuze kwa ujinga wao wenyewe. Hata ukichakachua matokeo huwezi kuchakachua dhamira ya wananchi ya kutoka kung'oa mfumo wa kifisadi na kujenga misingi ya taifa thabiti kiuchumi, kijamii na kisiasa. Slaa ameshaingia katika historia ya nchi hii kama mtu aliyeleta mageuzi ya kweli. Kuingia Ikulu si kigezo kikubwa kama hicho alichofanya. Mafisadi/Mamafia wanao uwezo wa kumweka yeyote hata asiye na uelewa au mpuuzi ndani ya Ikulu. Kumbuka Mobutu na Marekani. Sasa mapambano yaendelee viwanjani (bungeni + halmashauri) kwa kishindo zaidi ili waelewe wenye nchi yao wako macho masaa 24!

ni kweli mkuu hata punda huwezi kumlazimisha kunywa maji...dhamira ya watu ni ngumu kuibadilisha
 
Back
Top Bottom