Nini Kirefu cha CRDB

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Hey wajameni. Ni nini kirefu cha CRDB kwani niliambiwa na wenye beki yao kuwa sio tena COOPERATIVE and RURAL DEVELOPMENT BANK. Hii inanitatiza kidogo; ni kwanini hawaibadili jina kabisa na kuondoa vifupisho wasivyovitumia?
 
Mwanzoni hicho ndo kilikuwa kirefu chake, lakini wamiliki (wenye hisa) walikaa na kubadili katiba yao. Katika katiba mpya CRDB ni jina tu, lisilo na kirefu chochote kama majina mengine tu. Habari ndo hiyo. Vijijini tutafute bank zingine, maybe kupitia saccos.
 
Mwanzoni hicho ndo kilikuwa kirefu chake, lakini wamiliki (wenye hisa) walikaa na kubadili katiba yao. Katika katiba mpya CRDB ni jina tu, lisilo na kirefu chochote kama majina mengine tu. Habari ndo hiyo. Vijijini tutafute bank zingine, maybe kupitia saccos.
Ni kweli kaka, haii hapa chini nimeikuta wikipedia

CRDB Bank was formed when the former Cooperative Rural Development Bank which was wholly government owned was privatized, recapitalized and restructured
 
CRDB kirefu chake ni cooperative and rural development bank.Kwa sa sa inaitwa CRDB Bank limited kwa kufuatana na matakwa ya wamiliki na kuenenda na wakati.CRDB imepitia mabadiliko mbalimbali ya majina.Awali ilikuwa Cooperative bank ambayo ilitaifishwa na serikali kutoka vyama vya ushirika na baadaye miaka ya mwanzo ya sabini baada ya kuvunjwa tena kwa vyama vya ushirika,serikali ya awamu ya kwanza ilianzisha TRDB.tanzania Rural development bank,ikiwa na jukuku rasmi la maendeleo vijijini!Mwaka 1985 TRDB ilibadlishwa jina na kuwa CRDB kufuatia kurejeshwa kwa vyama vya ushirika kwa sheria ya mwaka 1982.Kwa hiyo kuanzia hapo benki imepata transformation mpaka kuitwa CRDB Bank
 
Of kwoz hii sio tena benki ya wavuja jasho au watu wa vijijini, bali waizi wa EPA na wengineo wanaovuna wasipopanda. It makes zero sense kuendelea kuitwa CRDB.
 
Kama wameamua kubaki na CRDB watafute maneno yatakayoendana na hilo sio kuyaacha yananing'ia hewani.
 
ni kama KCB(T) ltd. wanasema wao sio kenya commercial bank bali ni KCB kwa vile wameona the word kenya linawafanya waTZ wachukie kuitumia bank.
KCB TZ inafanya bidii kutotumia neno kenya lakini kibaya zaidi wameweka HQ kwenye harambee plaza

CRDB wamekataa kutumia hicho kirefu ili kuonyesha wateja wao kuwa wao wapo kwa watu wote (wafanyabiashara, wafanyakazi na wakulima).

kwa nyie mnaotaka banki ya wakulima ni vigumu kuwa na bank ya wakulima pekee yake na hiyo bank iwe kubwa kama crdb
 
Back
Top Bottom