Nini kipo nyuma ya Rais Samia kusimangwa hivi?

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
7,562
11,474
Katika hali isiyo ya kawaida kwa mara ya kwanza tumepata Rais wa kikatiba, yaani hajapigiwa kura wala kushindanishwa.

Ilizoeleka miaka kenda Rais lazima afanye kampeni, ashindane na wapinzani wake hali iliyokuwa inapelekea chuki, fitna, malumbano na hata umwagaji damu kati ya makundi hasimu.

Hii hupelekea hata baada ya uchaguzi kuwepo na visa vya hapa na pale ikiwemo chuki. Lakini katika hali hiyo hiyo inasikitisha namna Rais wetu alivyotoka haraka kwenye mioyo ya wananchi wengi, sio wote ila wengi.

Angekuwa kashindanishwa basi tungesema labda wapinzani wake hawakuridhishwa na matokeo na pengine alifanya kampeni chafu.

Sasa kuchokwa huku haraka chanzo inaweza kuwa ni nini?
 
Angalau anasimangwa na wanaomsimanga wapo hai na Wana amani

Kipindi Cha bwana yule ukisimsimanga kesho unaokotwa ununio
Tujikumbushe pia wafuatao;
1.Saed kubenea - tindikali
2.Dr ulimboka - kuteswa kung'olewa meno kwa prize na kutupwa pori la pande.
3. Ndimara Tegambwage - kukatwa mapanga baada ya kuvamiwa ofisi za mwanahalisi.
4. Dr. Silaa - Kupewa mvinyo uliotobolewa chini na kutegeshewa jukwaa hadi kuanguka.
5. Wana Arusha - kutekelezwa kwa ukumbi wa AICC na kujengwa JNICC ili kuwakomoa wana arusha.
6. Absalom Kibanda - kutekwa, kupigwa na kuharibiwa jicho.
7. Neville Meena - kutishiwa kifo.
8. Daudi mwangosi - kupigwa na kisha kufumuliwa utumbo.
9. Sheikh Ponda - kutandikwa risasi ya begani na kutiwa ndani.
10. Mauaji ya wanachama wa chadema arusha.
NB: Haya yalitokea kati ya 2005 hadi 2014
 
Hapo hujataja aliyekufa.
 
Back
Top Bottom