Nini kingetokea endapo Mwarabu ndio angekuwa Kiranja wa dunia na mwenye Teknolojia kubwa?

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,145
11,186
Nnapozungumzia kiranja wa Dunia nazni wengi mnaelewa kuwa ni taifa Kubwa lenye nguvu kiuchumi, Kijeshi na kwenye maswala ya Ushawishi. Kwa sasa taifa lenye nguvu ulimwenguni ni United States Of America (USA), ikifuatiwa na RUSSIA na CHINA

pmijdiwETpfphb7OOCKDOgjq-UsJI_ZdxfYQXCixeKQ.jpeg


984567-army-1446566383-129-640x480.jpeg

sasa hebu tufanye vise vesa kama Saudi arabia na waarabu wengine ndio wangekuwa na nguvu zaidi kiuchumi na kijeshi nini kingetokea, Dunia ingekuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mambo yangekuwa Shwari tu ila Tungepewa sisi Wabantu tungelazimisha kuwaf*ra wañanchi wa dunia hii hadharani.
 
Nnapozungumzia kiranja wa Dunia nazni wengi mnaelewa kuwa ni taifa Kubwa lenye nguvu kiuchumi, Kijeshi na kwenye maswala ya Ushawishi. Kwa sasa taifa lenye nguvu ulimwenguni ni United States Of America (USA), ikifuatiwa na RUSSIA na CHINA

View attachment 1009952

View attachment 1009953
sasa hebu tufanye vise vesa kama Saudi arabia na waarabu wengine ndio wangekuwa na nguvu zaidi kiuchumi na kijeshi nini kingetokea, Dunia ingekuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
hqdefault (2).jpg
maxresdefault.jpg
hqdefault (1).jpg
 
Nnapozungumzia kiranja wa Dunia nazni wengi mnaelewa kuwa ni taifa Kubwa lenye nguvu kiuchumi, Kijeshi na kwenye maswala ya Ushawishi. Kwa sasa taifa lenye nguvu ulimwenguni ni United States Of America (USA), ikifuatiwa na RUSSIA na CHINA

View attachment 1009952

View attachment 1009953
sasa hebu tufanye vise vesa kama Saudi arabia na waarabu wengine ndio wangekuwa na nguvu zaidi kiuchumi na kijeshi nini kingetokea, Dunia ingekuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app

Dunia ingelikuwa sehemu salama kabisa, Pasingekuwa na vita.

2singeona madada wakitembea na vimini/uchi, kujitoboa ulimi, mdomo na kuachia minywele yao holela kadamnasi.

Vile vile kusingekuwepo na wanaume wanaovaa heleni, kujichora tatoo, kuvaa heleni kwenye ulimi na mahanithi/wasenge/mashoga pia wasingekuwepo.

Na lugha moja tu ingetumika, ALLUGHATIL-A'ARABIYYA.

Namuomba Mungu anijaalie niijuwe vizuri hii lugha, ni lugha ambayo nimetokea kuipenda sana sana, na hata kaburini 2taulizwa kwa lugha ya kiarabu, cku ya Qiyamah pia 2taongeleshwa kwa lugha hiihii.


Wa upande flani najua mtakwazika tu 😀 huu ndo ukweri wenyewe.
 
na je mwafrika angekuwa kiranja dunia nzima na ananguvu za kiuchumi na kijeshi namaswala ya ushawishi. ingekuwa bora ya waarabu kwanza dunia yote ingeharibika ulaya yote watu wangekuwa wanapanga biashara barabarani ulaya yote vinyesi vingekuwa kila sehemu alama za barabarani vingeng'olewa watu wangekuwa wanakojolea kwenye chupa za maji ya kunywa wanatupa ovyo.uzalishaji ungepungua watu wangekuwa ni kukaa kwenye kahawa tuu story za wasaniii na mipira dunia ingebadilika kwa dakika kumi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Na lugha moja tu ingetumika, ALLUGHATIL-A'ARABIYYA.
Namuomba Mungu anijaalie niijuwe vizuri hii lugha, ni lugha ambayo nimetokea kuipenda sana sana, na hata kaburini 2taulizwa kwa lugha ya kiarabu, cku ya Qiyamah pia 2taongeleshwa kwa lugha hiihii.

1. Hii ni aina ya Fikra dumavu kabisa kuwahi kuisikia kwa mwanadamu. Kufikiri kwa aina hii ni kufikiri kwa kuchelewa kuwahi kutokea duniani.

2. Mungu Mwenye uwezo wote,anayefahamu kila kitu ikiwemo mpaka lugha ya kimatumbi na Kikurya, achague siku ya Kiyama kuhukumu watu kwa Kiarabu?

3. Ikiwa siku ya hukumu, Mungu atatumia Kiarabu je,wale ambao hawakifahamu Kiarabu watakuwa wana-respond vipi dhidi ya charges zao? Au watapatiwa Tuition ya Vodafasta na Malaika?
 
Ukweli tu ni kuwa dunia ingelazimishwa Kusilimu.

Mungu apishe mbali uwezekano huo.

Sent using Jamii Forums mobile app

UNASEMA DUNIA INGELAZIMISHWA KUSILIMU . WEWE UNAJUA IRAQ NI NCHI YA KIARABU JE UNAJUA KUNA WAIRAQ WAKRISTO MILLION NGAPI MBONA HAWAJALAZIMISHWA KUSILIMU WANAISHI PAMOJA- JE UNAJUA SYRIA NI NCHI YA KIARABU NA KUNA WASYRIA MILION NGAPI WAKRISTO MBONA HAWAJALAZIMISHWA KUSILIMU- MISRI EGYPTY NI NCHI YA KIARABU KUNA WA EGYPTY WANGAPI WAKRISTO MBONA HAWAJALAZIMISHWA KUSILIMU NA WENGINE NI VIONGOZI KATIKA NCHI ZAO- PALESTINE NI NCHI YA KIARABU UNAJUA KUNA WAPALESTINA WENGI NI WAKRISTO NA WANAISHI NA WAISLAM PAMOJA - LEBANON NI NCHI YA KIARABU KUNA WA LEBANON WAKRISTO WENGI KULIKO WAISLAMU MBONA HAWAGOMBANI KWA AJILI YA DINI AU KUKASHIFIANA NA HAWALAZIMISHANI- YEMEN NI NCHI ZA KIARABU MBONA KUNA WA YEMEN WANA DINI SAWA NA WAISRAEL MBONA HAWALAZIMISHANI - HALAFU WOTE HAO NILIOKUTAJIA WANAISHI MAISHA YA RAHA KULIKO NYINYI MPO TANZANIA. Uislamu ni dini kubwa na ndio dini mungu anaitambua hata ipigwe vita vipi watu ndio wanazidi kumiminika kuingia: mfano rais george bush wa marekani kawauwa raia wengi wa afghani stan lakini majuzi watoto wake wakike na wakiume wamesilimu mtasema mtachoka dini ni ya allah poleni sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Naona waarabu wanaishi vizuri kuondoa tu zile nchi zenye vita..pia kwa Afrika wao ndio wana maisha mazuri Misri,Algeria, Tunisia ukiondoa Libya iliyo alibiwa na ukienda Saudia,Qatar,Oman,Emirates, Barahin,Kuwait.. Tatizo kama wangeongoza uchumi mkubwa maana yake wangetumia njia hile hile kunyonya resource za nchi maskini..Ebu tuangalie awa ambao ndio vilanja wa uchumi usipofuata Sera zao kuruhusu ushoga Demokrasia wanayotaka wao wanakuwekea vikwazo..Machafuko yote ya vita wanasababisha wao huko Kongo Libya..Wanapandikiza vibaraka madarakani...
 
Wapiganaji wanaojinasibu kama waislaamu wenye msimamo mkali huua watu wote wasioamini ktk uislaamu . Hilo tu latosha kukuaminisha kutaka dunia nzima isilimishwe

Sent using Jamii Forums mobile app

Umejuaje hao ni waislamu?


Tuhuma ya kuhalalisha kumwua asiye mwislamu

600600p2216EDNmainimg-SSSWWW.jpg

Kundi la Daesh limezitegemea dalili zifuatazo kutoka Qurani Tukufu ili kuhalalisha kuwaua wasio waislamu na kila anayehitilafu nao.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema :{ Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu}. (Al-Baqarah: 193)
Mwenyezi Mungu Amesema: {Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia}. (Al-Tawbah: 4)

Jibu:
Uislamu ni dini ya kimataifa inayohimiza amani, kuziheshimu dini zote na kuharamisha kumwaga damu, na kwa kuzichambua dalili zinazotegemewa na kundi hilo la kigaidi, tutaona kuwa wanakata aya kutoka muktadha yake, na wanaitumia katika mahali pengine wakisahaulika aya zilizo kabla na baada ya aya hiyo, kwa mfano wanategemea kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina} kama ni dalili ya kuhalalisha kuwashambulia wasio waislamu chini ya jina la Jihadi bila ya kuangalia aya iliyoitangulia, ambapo Mwenyezi Mungu amesema: {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui} aya hiyo inabainisha kwamba mapigano hayakuruhusiwa isipokuwa kwa ajili ya kulinda nafsi dhidi ya maadui, na sio kwa ajili ya kuwashambulia watu.
Mwenyezi Mungu Amesema {wala msianze uadui}, na Uislamu haukuja kwa ajili ya kuwalazimisha watu waufuate, Mwenyezi Mungu amesema: {Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae}, bali amri inahusiana na (ahadi na mikataba) uliofanyika baina ya Waislamu na Wasio Waislamu, na rai ya Wasio Waislamu kuhusu ahadi na mikataba hiyo, na jambo hilo limethbitishwa na aya za Qurani, lakini kwa sharti ya kutokata aya kutoka muktadha yake, hivyo imetubidi tuangalie vizuru aya zilizo kabla na baada ya aya hizo zinazotegemewa na kundi hilo.
Hakika sheria imewagawanya wasio waislamu kuhusu kufanyika mikataba kwa aina sita:
Kwanza: wasio waislamu waliopewa ahadi na hawakushambulia waislamu:
Aya zote zimekuja zikibeba uhuru wa itikadi na uhuru wa kufuata dini yoyote, Mwenyezi Mungu Amesema: {hakuna kulazimisha katika dini}(Al-Baqarah:256), {Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?}, (Yunus:99), {Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari}, (Qaaf:45), {Wewe si mwenye kuwatawalia}, (Al-Ghashiyah:22), { Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae} ([Al-Kahf:29), {wala msianze uadui} (Al-Baqarah:190).
Pili: wasio waislamu hawakupewa ahadi na wamewashambulia wengine:
Kauli yake Mwenyezi Mungu: { Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui. Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipokutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri. Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu}, (Al-Baqarah:190,193). Na amri ya kwanza ilikuwa kwa kusamehe na kuvumilia maudhui, kisha Mwenyezi Mungu ameruhusu kutetea ili washambuliaji wasimamishe uadui wao katika kauli yake: {Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia} (Al-Hajj:39), kisha imekuja katika sura ya Al-Tawbah aya inayoamuru kuwauwa kila waliovunja ahadi yao uliofanyika pamoja na Mtume (S.A.W), amri hiyo kwa kuua ilikuja kama adhabu juu ya kuvunja ahadi yao na kwa kutowasameh hata wakisimamisha mashambulizi yao isipokuwa wakitubu na wakasimamisha swala na wakilipa zaka.
Tatu: wasio waislamu waliopewa ahadi na hawakushambulia lakini hawakutekeleza, na wakajaribu kuwaridhisha waislamu kwa midomo yao ilhali nyoyo zao zinakataa kataa, basi kauli ya Mwenyezi Mungu inawajumuisha: { Itakuwaje iwepo ahadi na washirikina mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake}, na kauli yake: {Itakuwaje! Nao wakikushindeni hawatazami kwenu udugu wala ahadi. Wanakufurahisheni kwa midomo yao tu, na nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wapotovu. Wamenunua thamani ndogo kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakazuilia watu na Njia yake. Hakika hao ni maovu waliyokuwa wakiyatenda}, na kauli yake: { Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yaokwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini. Wala wasidhanie wale walio kufuru kwamba wao wametangulia mbele. La, wao hawatashinda. Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari}, maana msiwashambulie kwa farasi , bali {ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua}, na kauli yake: {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu}, na kuli yake: {Basi wakitubu na wakashika Sala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazichambua Aya kwa watu wajuao}.
Nne: wasio waislamu waliopewa ahadi na wakatekeleza
Mwenyezi Mungu Anasema: {Isipokuwa washirikina ambao mliahidiana nao kisha wasikupunguzieni chochote, wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi hao watimizieni ahadi yao mpaka muda wao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha-Mungu}, (Al-Tawbah:4), na kauli yake: {ila wale mlioahidiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu wanakwenda nanyi sawa, nanyi pia nendeni sawa nao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu},
katika kauli yake: {Itakuwaje iwepo ahadi na washirikina mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake, ila wale mlio ahidiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu wanakwenda nanyi sawa, nanyi pia nendeni sawa nao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu. Itakuwaje! Nao wakikushindeni hawatazami kwenu udugu wala ahadi. Wanakufurahisheni kwa midomo yao tu, na nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wapotovu. Wamenunua thamani ndogo kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakazuilia watu na Njia yake. Hakika hao ni maovu waliyo kuwa wakiyatenda. Hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi; basi hao ndio warukao mipaka}, basi wasio waislamu wote waliofanya ahadi pamoja na Mtume (S.A.W) walikuwa baina ya waliokataa kutekeleza ahadi yao wakitangaza kukataa kwao, na baina ya waliojificha wanaowaridhisha waumini, lakini nyoyo zao zinakataa.
Tano: wasio waislamu waliopewa ahadi kisha wakavunja ahadi yao pamoja na Mtume (S.A.W).
Basi kauli ya Mwenyezi Mungu imewajumuisha: {Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu}, (Al-Tawbah:5).
Sita:
wasio waislamu walioahidi kisha wakavunja ahadi yao pamoja na waumini baada ya kufa kwa Mtume (S.A.W).
Basi kauli ya Mwenyezi Mungu inawajumuisha: {Na wakivunja viapo vyao baada ya kuahidi kwao, na wakatukana Dini yenu, basi piganeni na waongozi wa ukafiri. Hakika hao hawana viapo vya kweli. Huenda (kwa hayo) wakaacha}, maana kama hawakutubu na wala hawakuvunja ahadi basi: {Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari}.
Mwenyezi Mungu Amesema: "Basi mnapowakuta waliokufuru wapigeni shingoni mwao" basi hukumu hiyo inawahusu waislamu wanaopigana na makafiri katika uwanja wa mapigano, basi hao wameamriwa kuwapiga maadui pigo za kuuwa, na hukumu hiyo inakuwa wakati wa vita tu, ama vita ikiisha basi mwislamu hana haki ya kuanza uadui wake au kumwua mmoja wa makafiri akikutana naye pamoja na kupata nafasi ya kumwua. Basi heshima ya asiye mwislamu imehifadhiwa, na damu yake imeharamishwa kumwagiwa, haijuzu kwa mtu kumdhuru, kwani ni jengo la Mwenyezi Mungu na yeye ndiye peke yake aliyemleta hapa duniani na akamjaalia kuwa khalifa yake, na kwa sababu hiyo akaihifadhi damu yake.
 
Back
Top Bottom