Nini kinazuia Tanzania isitumie Nuclear energy?

NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
Tatizo la umeme Tanzania ishakua ka wimbo wa "maua mazuri yapendeza"
Swali langu, ni nini kinachozuia Tanzania isitumie nuclear energy kuendesha shughuli zote zinazohusika na energy? Kuna article nilisoma Tanzania inataka kumpita Canada kua producer wa pili duniani kwa madini ya Uranium, na hiyo ni muda kidogo sasa hivi my guess hilo lishatokea, then kwa nini tusiharvest nuclear energy, tusiseme hatuna wataalam, au zile story mnasikia ati bongo aliyesomea nuclear physics ni moja, hizo ni story tu, ninafahamu watanzania baadhi wenye PhD in nuclear physics , najua wapo wengine wengi wasomi kwenye hii sector, na am confident na wasomi wa Tanzania, nlipozunguka duniani vyuoni wapo watanzania wanaweka majina mazuri tu..

Hili swala lingepigiwa kelele sana lingeweza kupeleka nchi hii kwenye level nyingine ya development, mfano Tanzania sasa hivi najua ukitaka kuweka kitu kama train ni either zitafutiwe njia yake ya umeme au umeme uzimwe jiji zima kuwasha train.. Afu still tukiweza kua na umeme wa nuclear hata nchi jirani tunaweza kuwauzia umeme pia, kama producer mkubwa wa Uranium duniani ni aibu hatuitumii sisi wenyewe. Mtanzania kutumia jiko la umeme ni nadra sana, majiko kama ya induction yanapika msosi haraka sana, sema sijawahi ona mtanzania antumia simply coz umeme gharama, huku UK, Asia watu wanachezea umeme tu, Kuna tangazo nililiona nilipokua asia walikua wanaitania Africa kua haina umeme, wajinga afu watu walikua wanacheka, mtu inabidi ufiche sura..
 
Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,239
2,000
Nafikiri gharama za kufanikisha mradi kuanza kazi ndio shida tulio nayo na pili kwa kuwa hatutaweza ku-develop technology sisi wenyewe tutalazimika kuwapigia magoti Marekani, Urusi, Uchina au france ili kuweza kujenga mtambo. Ni safari ndefu ambayo inahitaji malengo na nia mahususi za kisiasa (political will).
 
Tewe

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
884
1,000
Nini kinachokufanya ufikirie nuclear wakati Tuna source kama stigra gaoge (correct me if im wrong) ziwezazo kuzalisha hhad 3000MW Avery sage, tunayo déposition kubwa tu Ya makaa Ya mawe , why nuclear energy which requires vers sofiscated handling?
 
ndupa

JF-Expert Member
Jan 25, 2008
4,411
0
Dreson4 unadhani kama tuna gesi tunashindwa izalisha wenyewe je nuclear energy ambayo mu-iran anasumbuliwa nayo tutaweza!??? Nakuunga mkono kabisa...ila siamini wala sitaki kuamini kama wataalam hatuna!! Kuna shida nyingine tunayo ya kukopa nje, je unadhani hii mikopo inalipwa vipi??? Kama sio kutoa miradi kwa wageni wakati wataalam na uwezo wa kuzalisha tunao???? Inauma asee!!!
 
Last edited by a moderator:

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,409
2,000
Germany pamoja na kuwa na teknolojia ya hali ya juu wanaikimbia sisi tunaikimbilia.

Tanzania hatujajiandaa kwa hili labda miaka 500 ijayo, sie tuchimbe tu na kuwauzia wenye uwezo.

Chernobyl na Fukushima somo tosha.
 
NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
Germany pamoja na kuwa na teknolojia ya hali ya juu wanaikimbia sisi tunaikimbilia.
Tanzania hatujajiandaa kwa hili labda miaka 500 ijayo, sie tuchimbe tu na kuwauzia wenye uwezo.
Chernobyl na Fukushima somo tosha.

Germany is Germany, Tanzania pia ni Tanzania, si lazima kufata mtu fulani kafanya nini, na germany navojua hadi leo wanatumia nuclear energy.... there are some nations wanali-handle hili swala vizuri mno, kuna nchi kama South Korea, UAE, mi nadhani kama jamaa alivosema hapo juu kuna nchi wanalimit maana naona hadi nchi kubwa zishaanza kuleta longolongo bongo ati itaharibu mazingira etc.. ila mbona wao wanafanya, hizi ni limit tu tunawekewa wakijua fika kua inaweza ikawaletea negative impact wao sio sisi... Swala la Chernobyl miaka ya themanini errors kama hizo zishaangaliwa na bado Japan disaster ya earthquake am sure hilo ni tatizo Tanzania haina.....
Kungekua na mtu humu JF ambaye alishafanya research kuhusiana na nuclear Tanzania nadhani angetupa data nzuri
 
Highlander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
3,094
1,195

sidhani kama kuna anayepinga matumizi salama na sahihi ya nuclear kwa malighafi ya urania. walalamikaji wengi wanatumia ugumu wa handling yake kuwa kigezo cha kupinga uchimbaji na matumizi ya urania. binafsi nakubali kuna smart alecks wa ulaya wanaweza pia wakatumia hayo kufanikisha agenda ya kukandamiza nchi fulani katika nyanja ya uchumi, kwa hiyo ni vizuri kuwa na watu wazalendo na makini kuchekecha pumba na chuya katika hoja hatua zinazochukuliwe ziwe na faida kwa nchi. Inadaiwa ni gharama kubwa sana kuyafanya matumizi ya urania kuwa salama, kuanzia kwenye uchimbaji hadi kwenye matumizi yake. tatizo kubwa ni hilo.

hebu ukipata muda pitia mkeka huu hapa: Lung cancer, leukaemia, genetic deformation listed among uranium diseases | TZ Business News
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,409
2,000
Germany is Germany, Tanzania pia ni Tanzania, si lazima kufata mtu fulani kafanya nini, na germany navojua hadi leo wanatumia nuclear energy.... there are some nations wanali-handle hili swala vizuri mno, kuna nchi kama South Korea, UAE, mi nadhani kama jamaa alivosema hapo juu kuna nchi wanalimit maana naona hadi nchi kubwa zishaanza kuleta longolongo bongo ati itaharibu mazingira etc.. ila mbona wao wanafanya, hizi ni limit tu tunawekewa wakijua fika kua inaweza ikawaletea negative impact wao sio sisi... Swala la Chernobyl miaka ya themanini errors kama hizo zishaangaliwa na bado Japan disaster ya earthquake am sure hilo ni tatizo Tanzania haina.....
Kungekua na mtu humu JF ambaye alishafanya research kuhusiana na nuclear Tanzania nadhani angetupa data nzuri

Tuna gesi, upepo, mawimbi, maji, makaa ya mawe, kwanini tukimbilie nyuklia?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom