Nini Kinawafanya vijana kuwa mashoga?

Mongoiwe

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
523
250
MACHI 13 MWAKA HUU, Jeshi la polisi lilimnasa kijana Rajabu Ismal (20) maalufu kwa jina la Anti Rama, mkazi wa Buyekele mjini Bukoba baada ya kukamatwa akiwa na vijana wawili usiku amevalia mavazi ya kike.

Kijana huyo alikamatwa usiku majira saa 5:14 mtaa wa Mtoni Mabatini jijini Mwanza akiwa jirani na nyumba ya diwani wa viti maalum Tausi Maftah (CCM) baada ya kutiliwa shaka na diwani huyo.

Kijana huyo alikuwa amevalia viatu virefu vya kike, cheni, sketi fupi, blauzi ya juu fupi (Kitop) alikuwa amesuka nyele zake na kufunga kitambaa mikononi akiwa na bangili ambaye alionekana rangi yake kuwa iliyotiwa mkorogo.

kikubwa kilichonifanya kulileta kwenu wana Jf ni kutaka kujadiliwa kwa hili, kwani mpaka sasa sijaelewa tatizo ni nini hapa mpaka kijana avae kike? au aamue kuwa shoga?
 
MaxShimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,814
1,250
Na Nora Damian

KISIWA cha Unguja, kinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mashoga wanaoishi na virusi vya ukimwi.


Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na Dk Subilaga Kasesela-Kaganda wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), alipokuwa akizungumza katika kongamano kuhusu maambukizi ya ukimwi kwa wafanyabiashara ya ngono, mashoga na watumia dawa za kulevya.

Alisema Zanzibar ndio eneo lenye mambo ya ushoga hapa nchini na kwamba asilimia 12 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika Kisiwa cga Unguja ni wale wanaojishughulisha na mambo hayo.

Alisema baadhi ya sababu zinazochangia kukua kwa tatizo hilo ni vishawishi, wazazi kuwa mbali na watoto wao, yatima wanaokosa malezi mazuri, watoto wa kiume kulelewa na mama kwa kipindi kirefu na mtoto wa kiume kupenda kuvaa mavazi ya kike.

Alisema sababu nyingine zinazochangia tatizo hilo ni mazingira ya shule za bweni, ambazo baadhi yake zina wanafunzi wa kiume pekee, mwanaume kuwa na homoni nyingi za kike na wanaume wengi kukaa sehemu moja kama jeshini na magerezani.

“Na wanawake wanaopenda kufanya ngono ya haja kubwa wanapaswa nao kujua kuwa ina hatari zaidi, kwa maana ya kupata maambukizo kuliko njia ya uke,”alisema Dk Kaganda.

Alisema utafiti uliofanywa mwaka 2007/2008 umeonyesha kuwa asilimia sita ya Watanzania wanaishi na virusi vya ukimwi, wanawake wakiwa ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo.

Dk Kaganda alisema tatizo hilo liko zaidi katika maeneo ya mijini na ligawagusa mno watu wazima na wanawake wenye uwezo wa kufanya ngono na watoto wadogo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la TAWIF lililoandaa kongamano hilo, Fransisca Matao alisema jamii inachangia kwa kiasi kikubwa watoto wengi kuwa mashoga kufuatia kuwanyanyapaa na kuwatenga.

Imetoka: Gazeti la Mwananchi
 
Bluray

Bluray

JF-Expert Member
Mar 25, 2008
3,456
1,225
Maria Nyerere aliiona hii kabla au vipi?
 
MaxShimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,814
1,250
Itakapokuwa state huru, naona nchi nzima itajaa mapopo bawa. lol
 
Sonara

Sonara

JF-Expert Member
Oct 2, 2008
728
195
wache wapukutike maradhi ya kujitakia hayapewi pole.
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
49,612
2,000
Ngoja wajitenge waone!!! itakuwa balaa
 
Chimo

Chimo

JF-Expert Member
Aug 31, 2008
698
500
Kumbukeni Ni juzi tu huko US Wamepewa Haki ya kuweza kuwa Maaskofu Na Lesbian kuwa Watawa
 
JoJiPoJi

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,827
2,000
Wadau kuna ukweli wowote hapo, hii nimeipata hapa michenzani sasa hivi
 
Buchanan

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
1,500
Wadau kuna ukweli wowote hapo, hii nimeipata hapa michenzani sasa hivi
Inaonekana huna uhakika na ulichokiandika. Kama ndivyo title ungeiweka kama swali!
 
Fidel80

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,964
1,225
Yawezekana kweli na vile yawezekana si kweli= tetesi
 
Caroline Danzi

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,618
1,225
Men why? Mimi siamini kama hiii ni tatizo. Wamejitakiwa wao acha wajizike wenyewe. Inauma sana wanaume tunaowategemea kutuongoza sasa ni mashoga.
 
Violet

Violet

Member
Nov 17, 2008
99
0
Sidhani kama kwa wote ni tatizo la kujitakia. Kuna watu wamekuwa kwenyaestreets, (watoto yatima)wamekuwa raped, njaa, umasikini anajikuta anafanya mambo ambao hakudhamiria. Kwa wao ni njia rahisi sana ya kujipatia hela kama wanawake( prostitutes) Je ni kila mtu anaweza pata fifanyio-kununua au bure? Je ni kila mtu anajua juu ya ukimwi najinsi inavyoambukiza? Last month nilikutana na mtu, age 35 hajui ukimwi unavyoambukiza, very sad.
 
M

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,413
1,195
Kweli ushoga ni tatizo kubwa Z'bar. Inafahamika kwamba kuna viongozi wakubwa pia wanajihusisha na uchafu huu na ndio maana haukemewi huko Visiwani. Wao kwao ni kama utamaduni.
 
J

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,333
1,225
Nyinyi mnaoingiza ushabiki kwenye sensitive issue kama hii mnashangaza kweli, Ukimwi unamaliza nchi baada ya kuhjadili tatizo ni nini tunaingiza ubaguzi.

Tatizo hapa ni ukosefu wa kazi na hakuna kingine kwani vijana badala ya kufanya kazi wanakaa vijiweni muda mrefu sana bila kazi matokeo yake wanaanza tabia za kishoga, njia sahihi ni kurekebisha sera za serikali kuhusu vija na sio kuwakashifu kwani hata bara kuna pocket za ukimwi zinatisha sana.

Tafuteni data za nyamongo mara, baadhi ya pocket za TANZAM Highway na Visiwani Ukerewe muone ni jinsi gani nchi inateketea wakati nyinyi mnashangilia
 
A

adventure

Member
Apr 20, 2009
17
0
Hivi zanzibar: pombe na ushoga kipi haramu kwao..maana nasikia hawataki kabisa kusikia pombe mpaka timu zao hawataki zivae nembo ya makampuni ya pombe inakuwaje hili la mashoga wameshindwa kulizibiti...
 
rmashauri

rmashauri

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
3,010
1,195
Mheshimiwa Gavana uko wapi? hebu njoo uote comments zako hapo. Nilikuambia siku kadhaa zilizopita sasa data hizi hapa. Je wasemaje hapa?
 
J

JUZAMO

Member
Apr 12, 2009
41
0
siamini na utafiti huu wa huyo dokta uchwara wa kitanganyika.
sikatai zanzibar kama kuna mashoga lakini kusema ndio sehemu inayoongoza kwa mashoga hapa Tanzania sikweli tena sikweli.
Jamani kuweni wa kweli mbona hamuwi wa kweli kila kitu mnasukumwa na dini najua uyo dokta ansumbuliwa na ukabila na ugalatia nani asiejua kama Dar es salaam na Arusha zina mashoga mara zaidi 1000 kuliko zanzibar jamai acheni upuuzi katika tafiti mnafanya ufisadio mpaka taaluma Mungu awalani kwa hili.TUWENI WA KWELI KWA MASHOGA WATANGANYIKA MNAONGOZA KULIKO WAZNZ.
 
N

Nahene

Member
Feb 18, 2008
32
0
JUZAMO
siamini na utafiti huu wa huyo dokta uchwara wa kitanganyika[/I].
Ehe,Juz hebu leta utafiti wa dokta Mtg aliye maridadi tuuone.


Jamani kuweni wa kweli mbona hamuwi wa kweli kila kitu mnasukumwa na dini najua uyo dokta ansumbuliwa na ukabila na ugalatia
Ehe kumbe utafiti wa docta unauhusiana na dini? Leta data zako kudhibitisha huo utafiti-udini.


Juz, mtafiti anapoongelea data za kulinanisha analinganisha na idadi ya watu waliopo eneo lile, inawezekana idadi ya mashoga Tz bara ikawa kubwa kuliko Znz. lakini ulinganisha kwa asilimia ya watu unakuta Tz bara ni ndogo kuliko Znz. Hapa ni hesabu ya gawiwo ndo inafanya kazi, yaani kwawiwo kubwa asilimia ndogo na gawiwo dogo asilimia kubwa. hivyo fikiri kabla ya kunena. Huyo Docta mchwara unayemwita ametumia hesabu rahisi tu ya kugawa.

Juz, jikumbushe hesabu za darasa la nne na tano ambako wengi wetu tumepitia.

Alamsiki
 
Top Bottom