Nini kinashindikana kwa serikali ya JK kuondoa Magari ya gharama (landcruiserVX n.k)? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kinashindikana kwa serikali ya JK kuondoa Magari ya gharama (landcruiserVX n.k)?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, Jun 17, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Jamani wana JF mimi hili linaniumiza kichwa kila siku hivi kweli ni nini kinashindikana kwa serikali kuamua kuyauza magari yote ambayo yanaliingiza hasara taifa na kubakiza gari moja kila idara la aina hiyo kwa kazi maalum?

  Wiki jana nilikuwa India, nikaenda chuo kikuu kimoja kaskazini mwa nchi, Nilicho kiona ni kuwa mkuu wa chuo anatumia gari aina ya toyota carina saloon. Chuo kina gari moja kubwa saizi ya landcruiser ambayo hutumika kama kuna haja ya kwenda labda NewDelhi au kwingineko mbali.

  Ukiangalia maofisi yetu mengi ni aibu, chukulia vyuo vikuu vyetu kila mtu ni Landcruiser VX/GX au Nissani Patrol je kuna tatizo gani hapo?

  Naombeni wanaJF tusaidiane kulieleza hili na wale ambao mko karibu na mh. kawambwa aulizwe ni nini kinashindikana? Mbona magufuli aliweza kurudisha gari zote katika himaya ya serikali na nakumbuka Prof. Mshana wa UDSM wakati akiwa CADO enzi hizo alishushwa kwenye land criuser lake na polisi pale ubungo na likaenda kubadilishwa namba, kawambwa anashindwa nini?

  Naombeni mawazo yenu
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu unajua viongozi wetu wengi ukiacha hawa ambao wazazi wao walikuwa viongoziwame kulia katik hali ya chini au ya kawaida. Mara nyingi mtu aki bahatika kutajirika au kupata nyadhifa nzito hujisahau sana. Sidhani kama kuna asiependa kuishi kifalme na ndivyo wanavyo fanya wao. Lakini nchi yetu masikini kwa hiyo siyo vizuri wakuu kutumia hela za walipa kodi kufacililate life style zao huku wananchi wa kawaida wana teseka. Kwa kujibu swali lako, kinacho tushinda ni kuwa na viongozi wenyewe will power ya kuji zuia kulewa madaraka. Wanakua sawa sawa na mwanaume anaye shindwa kuji vuia amuonapo mwanamke mrembo.
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ivi waliokutwa wamebadilisha numba za magari walifunguliwa mashtaka? Mimi leo nikibadilisha numba za gari langu, sio nimevunja sheria? Bongo...naipenda sema ndo basi tena!
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Unauliza nini kimeshindikana. Jibu ni hakuna kilichoshindikana. Hawataki, na sio kwamba wameshindwa.

  Juzi katika bajeti ya Kenya wameamua serikali yao haitanunua magari yenye cylinder capacity ya zaidi ya 1800 cc. Huo ni uamuzi mzuri.

  Sijui kama umesoma kitabu cha Shamba La Wanyama (Animal Farm). Viongozi wetu ni kama wale walioko kwenye kitabu hicho. Wanadai lazima watumie magari makubwa na ya bei mbaya "kwa faida yetu". Na yako mambumbumbu ambayo bado yatawapa kula zao.
   
 5. TRACE

  TRACE Member

  #5
  Jun 17, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 91
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli inauma sana kwani hawajali kabisa hali duni za mwananchi wa kawaida.Kimawazo yangu naona tunahitajika kubadilika kimtazamo sasa.Hivi ni kipi tukifanye au tuwaambieeje wananchi kuhusu matumizi na mipango mibovu ya Serikali yetu ambapo viongozi wenyewe wakae wakijua kuwa wananchi wao wanachukizwa na tabia zao mbovu?
   
 6. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere alikua kichwa. Na alikua muadilifu. Hizi sifa zilimpa 'moral authority' katika jamii yetu. Hakuhitaji mahekalu na maVX ili tuutambue 'ukubwa' wake.

  Hawa watawala wetu wa sasa tutawajuaje kwamba ni 'wakubwa'? Ukiacha pesa na mali, wana njia gani nyingine ya kutuonesha 'ukubwa' wao?
   
 7. BabaBabuu

  BabaBabuu Member

  #7
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  nakuunga mkono mkuu Moshi. ukiwauliza what is the rationale behind of having these 4500CC cars, jibu lao ni lilelile tu kwamba sababu kuu ni miundombinu mibovu. sasa nani wa kuirekebisha hiyo miundombinu?
  jawabu hapa ni kutengeneza hiyo miundombinu na sio kununua hizo 100mil @ shangingi cars. [​IMG]
  kama mkapa alivyojisemea kwamba tatizo letu kuu ni UVIVU WA KUFIKIRI, mwe!!!!!!!!!!!!!!![​IMG]
   
 8. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hakuna kinacho shindikana kama wakiamua na kama hawataki kuamua ni sisi wananchi tuseme au tuamue katika kura zetu.
  Kitendo cha wananchi kukataa kwa utaratibu huo,hata kama atakayeingia atakua na
  tabia hiyo,atapunguza kwa kuhofia kuondolewa na wenye nchi na hivyo basi wananchi kunufaika walao kidogo.
   
 9. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukosefu wa kuwa na msimamo na pia kuogopana... Nakumbuka sababu zilizotumiwa kuwa kutokana na safari ndefu anazofanya Mkuu wa wilaya basi anahitaji top of the range Land cruisser..... swali ni kwamba wakati wa Land Rover 109 na wakati huo barabara zilikuwa mbovu mbona walisafiri???

  lakini kama kuna point hapo kwa nini wasijiulize wakati wa shida ya barabara mbovu na magari ya zamani mbona viongozi walisafiri sana tu magari duini?? Sasa wanashindwa mpaka wapewe top of the range luxury cars,...... UMRI MAY BE??, AU UKAKAMAVU?? unajua zamani tulikuwa na viogozi damu zinachemka na miili kakamavu, lakini sasa hivi....... haya yetu macho....
   
Loading...