Riskytaker
JF-Expert Member
- Mar 14, 2024
- 473
- 2,076
Tanzania, mara nyingi, ajira zinatangazwa na waombaji hutakiwa kusubiri kwa wastani wa miezi 2 kabla ya kuitwa kwenye mahojiano.
Baada ya mahojiano, waombaji wanapaswa kusubiri tena miezi kadhaa kabla ya kuripoti kazini. Hali hii imekuwa kama desturi katika utumishi wa umma.
Kwa mfano, ajira zilizotangazwa katika kada ya afya mwezi wa 6, ambapo mahojiano ya mdomo na ya maandiko yamefanyika, lakini hadi leo bado hawajatoa majina ya waombaji.
Pia, ajira zilizotangazwa mwezi wa Februari katika sekta ya maji, waombaji waliweza kuripoti mwezi wa Agosti.
Hali ni hiyo hiyo kwa ajira za walimu zilizotangazwa mwezi wa Julai; hadi leo kimya, nadhani hata mahojiano hayajafanyika.
Je, ni kweli kwamba wanatangaza ajira bila kufanya utafiti wa eneo lililo na uhitaji?
Au je, utumishi haina wafanyakazi wa kutosha na vifaa vya kazi?
Kuna nini kinachofanya kuchukua muda mrefu, wastani wa miezi 4, au kuna watu maalumu wanaotafutwa kwenye orodha?
Au ni desturi tu kwamba wanajiamulia kasi ya kufanya maamuzi?
Kwa nini wasitoe rasmi mlolongo mzima wa mchakato?
Utumishi, tafadhali mju na majibu.