Nini kinasababisha shilingi ya kenya kuwa na thamani kuliko Yen ya japan?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,961
13,590
Kwanza nikiri kwamba sijui chochote kuhusu uchumi.Ninavyofahamu mimi ni kwamba uchumi wa nchi unapokuwa mkubwa na ndivyo thamani ya pesa yako inavyokuwa kubwa/imara linapokuja swala la masoko.

Uchumi wa nchi ya Japan ni mkubwa mara nyingi kuliko uchumi wa kenya. Unapotaja nchi za viwanda unazitaja zile g8. Marekani, canada, italia, ujerumani, ufaransa, uingereza na japan. Haya ni mataifa yaliyoendelea kiviwanda na kiuchumi.

Wanauza sana bidhaa zao nje ya nchi (xport). Kenya kama nchi ya Africa nchi zinazoitwa dunia ya tatu ambayo uuzaji wake wa bidhaa nje ya nchi ni mdogo, sarafu yake inaonekana kuwa imara kuliko ile ya nchi ya japan ambayo uchumi wake ni mkubwakuliko ule wa kenya.

Hoja hapa ni uchumi mkubwa unasababisha sarafu ya nchi kuwa imara. Au ni kitu gani haswa kinaangaliwa kuipa thamani sarafu?

Cc: chige
 
Screenshot_20171127-174741.png
 
Sijajua sababu lakin nijuavyo shilingi inavyozid kuwa strong ndo inazid kukuwia vigumu ku export bidhaa nje ndo maana bidhaa za china na asia ni nyingi africa kuliko usa kumbuka japan inategemea exporting sana so yen ikizid kuwa strong itamuwia vigumu ku penya na ndo maana mataifa makubwa yanalalamikia china kutopandisha fedha yake thaman
Wanatumia mbinu hani katika hili sijui sana ila nadhani ni interest rate kutoka central bank ya nchi husika as ukiongeza interest unavutia investors hence currency inapanda thamani na kinyume chake ni sawa so nadhani bapa benki kuu inahusika kwa nchi hizo japan,china na the likes ili sarafu yao ibaki chini kwa kupunguza interest rate
Lakin ngoja tusubiri majibu ya wataalamu
 
Well kuna sababu nyingi.Nikipata muda nitawaeleza.

Italian Lira iko weak ukilinganisha na Sh ya Kenya, lakini wote tunajua uchumi wa Italy ni mkubwa zaidi ya Kenya.

So kuwa na safari imara ni kigezo mojawapo lakini sio conclusive.
 
Nchi yoyote yenye uchumi unaotegemea mauzo ya bidhaa za viwandani(export oriented) kama Japan ni lazima waifanye pesa yao kuwa rahisi thidi ya pesa zingine za kigeni ili kuvutia kuuza bidhaa zao kirahisi..Kwa ujumla central banks za export oriented countries..wana strategies maalum kabisa ya kuifanya pesa yao kuwa weak! i
 
Ahsante kwa majibu mazuri. Kama nitakuwa nimekuelewa japan wanaifanya pesa yao kuwa weak ili kuuza bidhaa zao kwa urahisi. Swali kwenye soko la kimataifa bidhaa zote zinauzwa kwa US$. Nyingi ya bidhaa wanazo export zinakuwa zimewekwa kwa thamani ya $. Mbona kama sielewi? Ufafanuzi zaidi tafadhali
 
Well kuna sababu nyingi.Nikipata muda nitawaeleza.

Italian Lira iko weak ukilinganisha na Sh ya Kenya, lakini wote tunajua uchumi wa Italy ni mkubwa zaidi ya Kenya.

So kuwa na safari imara ni kigezo mojawapo lakini sio conclusive.
Fafanua kuu
 
Wenyewe wanatumia yen..sasa unatakiwa u change toka us dollar $kwenda yen ¥..anayetumia $ always ataona cheap kununua mfano gari toka japan kuliko kununua gari hiyohiyo toka UK ambako always paund£..ipo stronger than $!
 
Kuna vitu vitatu ambavyo kila kimoja kinajitegemea
1 Maendeleo
2 Uchumi
3 Nguvu ya sarafu

Kwa vile.Umezungumzia nguvu ya sarafu
Kuna njia mbili za kuona au kujua thamani ya fedha yako
1 Kupitia kubadilisha fedha yako dhidi ya fedha za nchi nyingine
2 Kupitia nguvu yake sokoni hasa katika manunuzi ya bidhaa

Tukizungumzia Exchange rate yaani kiwango ambacho sarafu moja inabadilishwa kuwa sarafu nyingine. Kuna aina mbili za kiwango cha ubadilishaji
1 Fixed exchange rate
2 Flexible exchange rate

Kuanguka na kupanda kwa thamani ya sarafu inaitwa Appreciation na Depreciation kupanda kwa thamani ya fedha au kushuka kwa thamani ya fedha ni kutokana na mahitaji ya soko lenyewe kwani Nguvu ya soko ndio uamua thamani ya bidhaa au huduma sokoni

Yote kwa yote inatokana na Sera za Benki Kuu katika (kudhibiti viwango vya riba, kununua na kuuza fedha katika soko la kimataifa

Vile vile kushuka kwa thamani husababishwa na kuingia kwa wingi fedha za nje ya nchi ndani ya nchi ambazo upunguza thamani ya sarafu kutokana na mahitaji ya hiyo fedha ya nje ndani ya nchi kitu kingine kinachoshusha thamani ya fedha ni mfumuko wa bei

Kingine uagizaji mkubwa wa bidhaa nje ya nchi(Import) ambapo tunatumia fedha za kigeni kununua hizo bidhaa kifupi zipo sababu nying tu lakini kuna nchi zinaweza kuamua kushusha thamani ya fedha yake yani Devaluation

Tatizo la Japan fedha yake kuwa dhaifu lilianzia kwenye vita vya pili vya dunia baada ya serikali ya Japan kuamua kuprint fedha nying kwa ajili ya matumizi na gharama za vita na kufanya 360 yen kuwa sawa na US dollar. 1 kumbuka exchange zote.Duniani zinafanya kwa Usd zipo sababu za kwa nini wanatumia Usd kupima thamani dhidi ya fedha nyingine lakini yote ni kutokana na mfumo wa Global financial system chini ya Federal Reserve System iliyaanziswa December 23, 1913 chini ya sheria ya (federal reserve system act ya mwaka 1913) mfumo ambao unafanya kazi kwenye mabank yote kasoro ya Iran,North Korea na Cuba sababu kubwa ni kutrace na kumonitor fedha zao under Secret Service protection

Thamani ya Yen iliendelea kuwa chini mpka mwaka 1971 ambapo Japani ilianza kupata maendeleo makubwa kuanzia kiuchumi na viwanda ambapo 12/8/1971 Bank kuu ya Japan na serikali ya Japan waliamua kupandisha thamani ya Yen na mpaka kufikia mwaka 1995 thamani ya Yen ilikuwa ni Yen 80 kwa Usd 1 na imekuwa ikipanda mpaka kufikia Yen 100 kwa Usd 1 lakini Japan na China wanachofanya ni Devaluation kwa fedha yao nikipata time nitakuja kuelezea kwa nini wanafanya hvyo pia faida na hasara zake kufanya Devaluation
 
Well kuna sababu nyingi.Nikipata muda nitawaeleza.

Italian Lira iko weak ukilinganisha na Sh ya Kenya, lakini wote tunajua uchumi wa Italy ni mkubwa zaidi ya Kenya.

So kuwa na safari imara ni kigezo mojawapo lakini sio conclusive.
Lira zishafutwa siku nyingi mkuu waitaliano wana euro€!
 
Ahsante kwa majibu mazuri. Kama nitakuwa nimekuelewa japan wanaifanya pesa yao kuwa weak
HAPANA... Yen ni Floating Currency. Floating Currency ni currency ambayo bei yake inakuwa determined by market force. Kwa maana nyingine there's no government intervention linapokuja suala la bei ya Yen.

So, why it's weak?

Kwanza sio sahii sana kusema Yen ni weak currency. Kuwa na bei ndogo haiwezi kuwa enough determinant kuita sarafu husika ni weak especially kama hiyo bei ndogo ni stable.

Tunasema Currency X ni weak pale inapokuwa inashuka thamani over time... kwa mfano, shilling yetu inavyoshuka thamani time to time ndipo unaweza kusema TZS ni weak currency but I don't think kama hicho ndicho hutokea kwa YEN.

Na ingawaje sijaangalia trend ya Kenyan Shilling vs Yen lakini ni matumaini yangu ukiangalia bei ya KSH vs JPY kwa miaka 5 iliyopita; sina shaka utakuta ni KSH ndiyo inashuka thamani dhidi ya JPY. The same for US $ vs JPY. Sina shaka miaka 5 iliyopita mtu alitakiwa kulipa more Yen for 1$ kuliko ilivyo hivi sasa thus concluding JPY is Appreciating/Inapanda thamani even against USD na sio kushuka! Hiyo nayo ina-conclude JPY sio weak currency kwa sababu uchumi wa Japan unatosha sana kuifanya sarafu yake kuwa strong.

In short, Yen ni moja ya sarafu imara sana duniani ingawaje bei yake ( I hate to say thamani yake) ipo chini sana!

So, kwa ajili ya mjadala huu wacha tutumie neno Cheap Currency.

In short, source ya sababu cheap ni very historical. First factor ni kushuka kwa thamani ya Silver takribani karne moja iliyopita.

By the time, thamani ya YEN ilikuwa inakuwa quoted by silver value na kwahiyo thamani ya silver iliposhuka; thamani ya Yen nayo ikashuka!

Later on, ikaja Vita Kuu ya Pili ya Dunia na Japan alikuwa mdau mkuu wa ile vita.

Baada ya vita kwisha; uchumi wa Japan ukaathirika sana na hivyo kuifanya Yen kuendelea kuporomoka!

Miaka kadhaa baadae, uchumi wa Japan ukaanza kukaa vizuri to the point ikafika wakati Yen nayo ikaanza ku-recover na kuwa stable though still ilikuwa bado cheap kulinganisha na sarafu zingine!

From time to time ikaanza kupanda thamani just by the influence of market force na sio kama ambavyo walifanya akina Nyerere!

Lakini vile vile tusisahau zamani nchi nyingi zilikuwa zina-interfere thamani ya sarafu yake! Tanzania ya Nyerere kwa mfano, ingawaje uchumi ulikuwa mbovu lakini shilingi ilikuwa very expensive... hayo yalikuwa matunda machungu ya government intervention.

Inavyoelekea, Japan hawakutaka ku-intervene sarafu yao na kama walikuwa wanafanya basi ni kwa kiwango cha chini sana lakini kwa kiasi kikubwa waliiacha YEN ipambane na nguvu ya soko huku serikali ikijikita kuimarisha uchumi wake kama factor kuu ya kuchochea thamani ya sarafu ya nchi husika!

Na kwavile uchumi wake ulishaanza kutengemaa, bila shaka walishaanza kuyaona matunda ya kuwa na cheap currency huku production ikiwa juu!

REMEMBER, YEN sio WEAK Currency but ni among the STRONGEST Currency ingawaje ni very CHEAP!

Aidha, sarafu kuwa imara haimaanishi kwamba bei yake ni kubwa! Sarafu inaweza kuwa very cheap na still ikawa considered ni strong currency provided ipo bei yake hai-fluctuate hovyo hovyo...

Yuan kwa mfano, ni very expensive ukilinganisha na Dollar lakini hata forex traders wanaikwepa kwa sababu hawafahamu serikali ya China itafanya nini kuhusu Yuan katikati ya trading session!
 
Ahsante kwa majibu mazuri. Kama nitakuwa nimekuelewa japan wanaifanya pesa yao kuwa weak ili kuuza bidhaa zao kwa urahisi. Swali kwenye soko la kimataifa bidhaa zote zinauzwa kwa US$. Nyingi ya bidhaa wanazo export zinakuwa zimewekwa kwa thamani ya $. Mbona kama sielewi? Ufafanuzi zaidi tafadhali
Japo bei zipo kwa US$ bado ukibadilisha kwa Yuan/Yen utapata bidhaa nyingi toka Japan/china
 
Kuna vitu vitatu ambavyo kila kimoja kinajitegemea
1 Maendeleo
2 Uchumi
3 Nguvu ya sarafu

Kwa vile.Umezungumzia nguvu ya sarafu
Kuna njia mbili za kuona au kujua thamani ya fedha yako
1 Kupitia kubadilisha fedha yako dhidi ya fedha za nchi nyingine
2 Kupitia nguvu yake sokoni hasa katika manunuzi ya bidhaa

Tukizungumzia Exchange rate yaani kiwango ambacho sarafu moja inabadilishwa kuwa sarafu nyingine. Kuna aina mbili za kiwango cha ubadilishaji
1 Fixed exchange rate
2 Flexible exchange rate

Kuanguka na kupanda kwa thamani ya sarafu inaitwa Appreciation na Depreciation kupanda kwa thamani ya fedha au kushuka kwa thamani ya fedha ni kutokana na mahitaji ya soko lenyewe kwani Nguvu ya soko ndio uamua thamani ya bidhaa au huduma sokoni

Yote kwa yote inatokana na Sera za Benki Kuu katika (kudhibiti viwango vya riba, kununua na kuuza fedha katika soko la kimataifa

Vile vile kushuka kwa thamani husababishwa na kuingia kwa wingi fedha za nje ya nchi ndani ya nchi ambazo upunguza thamani ya sarafu kutokana na mahitaji ya hiyo fedha ya nje ndani ya nchi kitu kingine kinachoshusha thamani ya fedha ni mfumuko wa bei

Kingine uagizaji mkubwa wa bidhaa nje ya nchi(Import) ambapo tunatumia fedha za kigeni kununua hizo bidhaa kifupi zipo sababu nying tu lakini kuna nchi zinaweza kuamua kushusha thamani ya fedha yake yani Devaluation

Tatizo la Japan fedha yake kuwa dhaifu lilianzia kwenye vita vya pili vya dunia baada ya serikali ya Japan kuamua kuprint fedha nying kwa ajili ya matumizi na gharama za vita na kufanya 360 yen kuwa sawa na US dollar. 1 kumbuka exchange zote.Duniani zinafanya kwa Usd zipo sababu za kwa nini wanatumia Usd kupima thamani dhidi ya fedha nyingine lakini yote ni kutokana na mfumo wa Global financial system chini ya Federal Reserve System iliyaanziswa December 23, 1913 chini ya sheria ya (federal reserve system act ya mwaka 1913) mfumo ambao unafanya kazi kwenye mabank yote kasoro ya Iran,North Korea na Cuba sababu kubwa ni kutrace na kumonitor fedha zao under Secret Service protection

Thamani ya Yen iliendelea kuwa chini mpka mwaka 1971 ambapo Japani ilianza kupata maendeleo makubwa kuanzia kiuchumi na viwanda ambapo 12/8/1971 Bank kuu ya Japan na serikali ya Japan waliamua kupandisha thamani ya Yen na mpaka kufikia mwaka 1995 thamani ya Yen ilikuwa ni Yen 80 kwa Usd 1 na imekuwa ikipanda mpaka kufikia Yen 100 kwa Usd 1 lakini Japan na China wanachofanya ni Devaluation kwa fedha yao nikipata time nitakuja kuelezea kwa nini wanafanya hvyo pia faida na hasara zake kufanya Devaluation
Somo nzuri wengine blablaa tuu
 
Back
Top Bottom