MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,011
- 16,748
Nimeshangaa sana kusikia Mabasi yaendayo Mkoani Mwanza yakitoka Dar es Salaam Saa 12 Asubuhi yanafika Mwanza Saa 5 na hata Saa 6 za Usiku.
Mwaka 2006, 2007, 2008 na 2009 nimesafiri sana na Mabasi kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza ( tena wakati huo Barabara ilikuwa na Matatizo baadhi ya maeneo ) ila tulikuwa tunafika Nyegezi Kituoni Mwanza Saa 1 za Usiku na wapo ambao walikuwa wakifika hata Saa 12 za Jioni.
Nilidhani kwa sasa baada ya Barabara nyingi za Tanzania kuwa Mkeka ( Lami tupu ) Asante kwa Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kuzijenga vyema alipokuwa Waziri chini ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete basi Mabasi yaendayo Mikoani yatakuwa yanawahi Kufika badala yake sasa ndiyo yanachelewa hadi Kero.
Napenda mno Mabasi yaendayo Kasi ( Spidi ) huko Mikoani au yakija Dar es Salaam na ndiyo maana nikiwa nisafiri nikienda kukata Tiketi Kwanza huwa nayaulizia Mabasi yaendayo haraka na yenye Madereva Mabandidu na Masela au yale ambayo huwa yanawakosakosa sana Ng'ombe, Mbuzi, Punda, Kuku na hata Watu ( Waendesha Baiskeli au Pikipiki ) au wale wanaopenda Kuvuka Kiholela ( Kizembe ) na nikiyapata ndiyo huwa nayapanda.