Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Haijawahi kutokea Tanzania yetu ikashuhudia haya yanayoendelea. Kwamba uchaguzi unaisha mwezi mzima hakuna Cabinet? Baraza la Mawaziri! Hili sio ndio Serikali?
Mkuu wa kaya anataka kutuambia mawaziri au Serikali haina umuhimu tena? Kwamba Waziri wa fedha mgawa fungu ndio ana umuhimu? Waziri wa mambo ya nje ndio ana umuhimu kurekebisha kama wadau wa misaada wanazingua?
Je, tujiulize toka tumepata uhuru ilishawahi kutokea kuwa rais ambaye hana Cabinet kwa mwezi mzima?
Kama ni ukata mimi sikubali, sababu hata enzi za mzee Mwinyi ukata ulikuwepo lakini sikushuhudia hiki ninachokiona.
Au sasa hivi ndio kusema hakuna majembe ya uhakika bungeni kiasi hata cha kushindwa kuunda safu ya askari wa miavuli?
Naona kama wabongo wengi wameshangaa na hawajui nini hatima ya lini serikali itayowatumikia itaundwa!
Ngoja tusubili, lakini je mawaziri hawana umuhimu? Kama ni hivyo mbona awamu zilizopita cabinet ilikuwa inaundwa haraka!