Nini kinaendelea kwenye uchumi wa urusi. Tokea hii wiki ianze ruble imeshuka thamani kiasi kwamba benki kuu imezuia ununuzi wa hii currency

dogman360

Member
Oct 15, 2018
95
156
20241126_201445.jpg
20241128_071633.jpg
 
Next month lazima benki kuu ipandishe interest rate kwenye 23%
Sasa hivi wapo 21% tangu mwezi wa kumi.

Kwa mikopo rate ya benki kuu ni 17% kwa mwaka, ambapo mabenki ya biashara yanaongeza 3.5% to 4% juu. Kwahiyo Mrusi kwa miezi mingi sasa akikopa mkopo wa kibenki analipa juu ya 20% riba kwa mwaka. Rate kama kausha damu

Na kwa collaterals, mabenki ya Urusi sasa hawatoi mkopo zaidi ya thamani ya 50% ya asset. Tuseme mfano ukiwa na nyumba ya milioni 100 za kibongo, hamna benki inakupa mkopo zaidi ya milioni 50.

Interest ya 21% inafanya makampuni yenye export contracts za muda mrefu yale hasara. Kampuni kama Rostec yenye mikataba ya silaha ambayo inatumia muda mrefu kuwa delivered nina imani itaacha kabisa kufanya delivery kwanza.

Wakati huo, sekta ya reli kwa Urusi haifanyi vizuri kwa muda mrefu sasa.

Hata hivyo Russia wako very resilient. Wana mazingira fulani yanawawezesha kuhimili na kuvumilia hizi changamoto na sekta yao ya uchumi na fedha ni sekta ninayoamini ina watu wenye akili sana. Huwa wanakuja na solutions za maana.
 
Putin kwa sasa anaficha machungu ya uchumi wake, ila subirini miaka 3 au 5 ijayo muone show.

West siyo wajinga, ukichunguza utagundua vita ya Ukrain wanaipeleka hatua kwa hatua. Muda ambao Putin anafikiri ndio anawawin Ukrain wao West wanaongeza gia, mambo yanaanza upya.

Sasa hivi kila shilingi anayo pata inabidi aitumbukize vitani.
Economic analyst wa NATO kutoka NKUHUNGU - Dodoma
 
Putin kwa sasa anaficha machungu ya uchumi wake, ila subirini miaka 3 au 5 ijayo muone show.

West siyo wajinga, ukichunguza utagundua vita ya Ukrain wanaipeleka hatua kwa hatua. Muda ambao Putin anafikiri ndio anawawin Ukrain wao West wanaongeza gia, mambo yanaanza upya.

Sasa hivi kila shilingi anayo pata inabidi aitumbukize vitani.
Na Ujerumani ambayo viwanda vinafungwa kila siku kwa sababu ya kushindwa kujiendesha na yenyewe imepatwa na nini?
Urusi anatumia$3.5bilion kila Mwezi kwa ajili ya vita ya Ukraine wakati huo anaingiza zaidi ya $60 bilion kila Mwezi kutokana na gesi na mafuta bado hujaweka mauzo ya bidhaa za viwandani ,bidhaa za chakula na mbolea,bado makusanyo ya ndani.

Hivi unadhani Urusi inangozwa na watu wenye akili ndogo kama mungu wako jiwe na chawa wake akina msiba?
 
Kila siku?

Mkuu, hii ni chumvi sasa, unaweza kututajia viwanda vilivyofungwa juzi, jana na leo mkuu..!

Karibu
 
Back
Top Bottom