Nini kinaendelea kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa mkoani Dodoma baada ya kupatiwa mkopo wa kugharamia ujenzi huo?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,993
144,329
Wakati ujenzi wa uwanja wa mpira kwa ufadhili wa mfalme wa Morocco ukiwa hauelewiki maana hakuna kinachoendelea site, naomba kujuzwa ni nini kinaendelea kuhusu ahadi ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo la Msalato mkoani Dodoma.

Nakumbuka iliripotiwa kuwa mkopo wa shilingi bilioni 625.1 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya kugharamia ujenzi huo ulishaidhinishwa na Benki hiyo ila kinachoendelea site kwa sasa sijui hivyo naomba kama kuna mwenye taarifa ya kuanza kwa ujenzi huo atupatie.

Ujenzi Kiwanja cha Ndege Msalato waiva
 
Kwa serikali hii ya magu hakika ujenzi utafanyika tuu ulizia mengine... Wagogo msipoacha kuomba basi tena mji unajengwa balaa chakuuliza ni waG mnachangamkia fursa zakazi? Au ndo bakuli mwachie nani!?
 
Kwa serikali hii ya magu hakika ujenzi utafanyika tuu ulizia mengine... Wagogo msipoacha kuomba basi tena mji unajengwa balaa chakuuliza ni waG mnachangamkia fursa zakazi? Au ndo bakuli mwachie nani!?
Hatujadili tabia za Wagogo,tunajadili mwenendo wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato,Dodoma.
 
..bora wangejenga VIWANDA wananchi wapate ajira.

..zile hoja kuwa makao makuu lazima yawe katikati ya nchi zilikuwa ni uongo tu.

..kama hoja zile zina mashiko mbona bwana mkubwa kakimbilia kijijini na anadai kitendo hicho hakimzuii kuendesha serikali?

..again, kila kilichojengwa Dodoma tayari kilikuwepo Dsm. Ni afadhali tungewekeza fedha zetu ktk miradi mipya ya maendeleo ktk sekta zinazotoa ajira na fursa kwa wananchi.
 
Serikali ipo kwenye hatua ya awali ya kuwalipa fidia wakazi wote ambao maeneo yao yamepitiwa ama kufikiwa na uwanja wa ndege. Kama wewe ni mkazi mmoja wapo tafadhali fika kwenye ofisi yako ya kata ili kuhakiki jina lako.
 
Hatujadili tabia za Wagogo,tunajadili mwenendo wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato,Dodoma.
Kuhusu ujenzi imeisha iyooo, mm nimeona mbali nkafikiri nje ya box...Dodoma iwaamshe wagogo sio makabila yatawale biz zote kubwa wao wapite na bakuli hku wanasindikizwa na watoto!! Waamke
 
Back
Top Bottom