eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,227
- 16,178
Kunasemekana huko Tarime kwa mbunge Heche kuna mapambano kati ya police na Raia ambao wanapinga ACACIA kuendelea na shughuli zao wakidai ni wezi kwa mujibu wa Rais Magufuli na hawahitaji shughuli zozote kuendelea mgodini hapo.
Sasa ni vita kati ya Raia na mabomu ya polisi
Idadi kubwa ya watu wamekusanyika leo katika mgodi wa North Mara kwa siku ya pili mfululizo nchini Tanzania kushinikiza walipwe fidia kutokana na kile wanachodai kufanyiwa madhira mabaya kutokana na operesheni za mgodi huo katika eneo la Nyamongo, wilaya ya Tarime nchini Tanzania. Hali hiyo inatokana na kile kinachoolezwa ripoti mbili za madini za hivi karibuni nchini humo kutaja kampuni tanzu inayosimamia mgodi huo ya Acacia kutosajiliwa.
Mwandishi wa DW Swahili Sudi Mnette amezungumza na Chacha Heche ambaye ni Mwananchi na mjumbe wa kamati iliyoundwa na aliyekuwa waziri wa nishati na madini wa Tanzania Profesa Sospeter Muhongo kufuatilia matatizo ya wananchi na mgodi kwa muda mrefu.