Nini kimewasibu chama kikuu cha upinzani Tanzania?

Mindi,
Kwa ufupi CCM haina hofu ila tulia uone kitachotokea october mwaka huu. Chadema haikupata ushindi kama unavyosema.

Kale ka umoja ka ukawa ilikuwa assisting pass kufunga goli. Safari hii hakapo hilo ulitambue.
 
Kipimo pekee cha imani hizi ni UCHAGUZI HURU NA WA HAKI. Ikitokea CHADEMA ikapata A CRASHING DEFEAT mbele ya CCM, hapo wala hapatakuwa na ubishi. Lakini kama Katibu Mkuu Bashiru anakiri kwamba bila mbeleko ya DOLA, CCM inaweza kuondolewa madarakani kama ilivyokuwa kwa KANU, hizi kauli za udhaifu wa CHADEMA zitabakia kuwa ni SENTIMENTS.

Anasifiwa CCM kwamba ana mtandao mkubwa, nguvu kubwa za kitaasisi, rasilimali nyingi, uzoefu, ujuzi na maarifa, hekima na busara. Sasa Paskali naomba unijibu. Inakuwaje basi kila mara CCM inahitaji CHADEMA awe kafungwa kitambaa usoni na mguuni kafungwa jiwe, waingiapo ulingoni?
 
Vijana hawa waliokuwa na mapenzi ya dhati na chama wamekatishwa tamaa na uongozi usio na dira hivi sasa hawaonekani tena kupiga deki lami!
tapatalk_1581843241355.jpg
 
Magufuli kawambia hajakataza mikutano km diwani au mbunge anataka mkutano afanye hivyo uchaguz hautahairishwa.


Akili za kuzaliwa zinajenga

Magufuli sio sheria, sheria inaruhusu chama chochote kilichodajiliwa kufanya kazi za siasa ndani ya jamuhuri ya muungano.

Magufuli hawezi kuahirisha uchaguzi maana yeye anafaidika na huu mfumo mbovu wa uchaguzi, na yeye ni namba moja wa kuvuruga na kunajisi chaguzi za nchi hii.

Sasa hizo akili za kuzaliwa sijui zinakwama wapi hapo?
 
Kwa ufupi CCM haina hofu ila tulia uone kitachotokea october mwaka huu. Chadema haikupata ushindi kama unavyosema. Kale ka umoja ka ukawa ilikuwa assisting pass kufunga goli. Safari hii hakapo hilo ulitambue.
Unatoa kauli kwamba CCM haina hofu. Mbona matendo yake ni tofauti kabisa na hiyo kauli yako? Hebu jenga hoja zako kimantiki. Nimekuchambulia hofu ya CCM kwa kauli rasmi ya CCM. Wewe unasema nisubiri? Nisubiri uporaji mungine wa CCM?
 
Unatoa kauli kwamba CCM haina hofu. Mbona matendo yake ni tofauti kabisa na hiyo kauli yako? Hebu jenga hoja zako kimantiki. Nimekuchambulia hofu ya CCM kwa kauli rasmi ya CCM. Wewe unasema nisubiri? Nisubiri uporaji mungine wa CCM?
Hofu ipi fafanua.
 
Ok, nieleze alichomaanisha
Alikuwa anamaanisha kutumia dola ili kukeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.Wala sio kukandamiza wapinzani na vyama vyao. Mfano Takukuru kudhibiti rushwa na ubadhirifu,umeona kwa macho yako. Polisi kulinda raia na mali zao, hilo unalifahamu maana watu wanalala bila woga. Mengine unajua ila unafumba macho.
 
Alikuwa anamaanisha kutumia dola ili kukeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.Wala sio kukandamiza wapinzani na vyama vyao. Mfano Takukuru kudhibiti rushwa na ubadhirifu,umeona kwa macho yako.Polisi kulinda raia na mali zao, hilo unalifahamu maana watu wanalala bila woga. Mengine unajua ila unafumba macho.
Sasa wewe ndio hukumwelewa Bashiru. Sikiliza tena clip ya mahojiano ya kipindi cha KONANI. Bashiru aliulizwa swali kwamba vyama vya upinzani vimezuiliwa kufanya mikutano, wakati CCM wanafanya mikutano waziwazi BILA KUZUILIWA na polisi. Upinzani wakijaribu tu wanakumbana na DOLA. Ndipo Bashiru alipoeleza hiyo SERA kwamba CCM iko madarakani na itautumia DOLA kuendelea kubaki madarakani. Angalia hiyo context.

Pia ishu hii aliwahi kuiongelea Rais Kikwete, pale alipoitaka CCM kuacha kuegemea mno dola katika kukabiliana na vyama vya upinzani. Yeye alitaka matumizi ya hoja badala ya IRON FIST ya dola.

Na ukiangalia hali halisi, polisi wamejifanya kuwa tawi la CCM, au wamefanywa hivyo. Mara nyingi maofisa wa dola wanaponyanyasa wapinzani, wanapata promosheni haraka. Hii inahusisha mahakimu pia. Kuna yule ofisa wa polisi aliyejinasibu hadharani kuipendelea CCM dhidi ya"maadui" wake.

TAKUKURU ipo kwa mujibu wa katiba na hakuna anayeweza hoji utendaji wake mpaka sasa. Kulikuwa tu na ile ishu ya Joshua Nassari, aliyekusanya ushahidi wa Mkuu wa wilaya kutoa rushwa kwa madiwani wa CHADEMA. TAKUKURU walikataa kufanyia kazi ushahidi huo kwa visingizio, lakini ilikuwa ngumu sana kwao kuendelea kupeleleza wakati Rais amempandisha cheo "mtuhumiwa". Huo ni udhaifu mkubwa sana katika utendaji
 
chagu wa malunde,
Umeandika na kujipinda kwelikweli kwa bandiko hili.

Lakini kama kawaida ya watu wa aina yako mnasahau jambo moja tu ambalo huwa hamthubutu kuliongelea kwenye mada kama hizi.

CHADEMA kishakufa, lakini hapo hapo mnawaogopa ile mbaya hata hamtaki waTanzania wachague viongozi wao bila ya mizengwe, kwa nini?

Kwa vile CHADEMA sio tishio tena, na haionekani kuwa kuna chama kingine kinachoibuka haraka kuchukua nafasi yao, inakuwaje muwashikilie wananchi, kana kwamba hawana akili zao wenyewe za kupiga kura zao na hizo kura mzizoe nyinyi bila kuwashurutisha au kuwawekea vikwazo wananchi hawa!

Mada zenu zote za aina hii nguvu zake huishia hapo.

Mimi sijui kama CHADEMA wamekwisha au ndio nguvu imeongezeka, hili silijui kama unavyolijua wewe mtaalamu wa eneo hili. Nakukumbusha tu upungufu huo hapo wa kujitoa akili zenu kama punguani mnapoliandika jambo hili.
 
Mkiambiwa Tume huru ya uchaguzi mnakuwa na kigugumizi,,,,kama mnapendwa wekani tume huru muone moto wake huku wananchiwamechoka kimaisha mnambiwa
 
Back
Top Bottom