Nini kimewanyamazisha wabunge wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kimewanyamazisha wabunge wetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FM, Jul 5, 2009.

 1. F

  FM JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wabunge walivalia njuga sana suala la kuanza utekelezaji wa miradi mingine ya barabara kama ule wa Dumila-Kilosa na Korogwe -Handeni na kuacha miradi ambayo imekuwa kwenye ilani ya chama kuanzia Tanu hadi ccm mfano barabara ya Babati-Dodoma -Iringa. Mhe. Diallo kwa msisitizo akawasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya bajeti kwamba fedha zilizowekwa kwenye miradi ambayo kimsingi haina tija zihamishiwe kwenye miradi wa ujenzi wa barabara ya babati-dodoma-iringa na fedha zingine zimalizie kipande cha barabara ya manyoni miradi ambayo kwa mtazamo wangu ndiyo yenye tija. Hoja yake ilikubalika na wabunge na kuwasilishwa mbele ya kamati ya miundombinu.
  Jana wakati m/kiti wa Kamati ya miundombinu akiwalisha maoni ya kamati kuhusu hoja ya mhe. Diallo aliliambia bunge kwamba kamati imetafakari kwa kina hoja ya mheshimiwa na imeona kuwa haitakua busara kuhamisha miradi hiyo kwa sasa kwani kwa kufanya hivyo kutawasononesha sana wananchi wa maeneo husika na kwamba wamewasiliana na serikali ili zitafutwe fedha nyingine kwa ajili ujenzi barabara zilizolalamikiwa sana ikiwemo ya Babati-Dom-Ira. Aidha, wakati akihitimisha hoja yake Mhe. Waziri wa Miundombinu naye akasema serikali imepokea maoni ya Kamati na kwamba itatafuta fedha kiasi cha 40b kutoka kwa wahisani na zikipatikana ujenzi utaanza mara moja. Kwa kauli hiyo tu wabunge wetu wakapiga makofi makubwa. Hata pale Spika alipojaribu kuwajengea mazingira ya kuhoji zaidi wakati wa kamati ya matumizi kwa kurejesha kanuni inayowaruhusu kuuliza zaidi ya mara moja wakagoma. Najiuliza hivi ni kweli wananchi wa dumila wangeweza kusononeka kwa kuikosa barabara ambayo hata hawakuwa na mpango nayo japo kiukweli wanaihitaji? Je, wanajisikiaje wananchi wa maeneo ambako inapita barabara ya Babati-Dom- Ira, Je wanajisikiaje wananchi wa Singida? Je, wanajisikiaje wananchi wa Tbr na Kigoma ambao wamekuwa wakiahidiwa kila mwaka. Je, network ya barabara Korogwe -Handeni na Dumila -Kilosa na ile Babati- Dom- iIa na Sgd hadi Kigoma kimizani zinalinganishwaje ktk kufungua njia za uchumi. Kuna sababu gani basi kutotumia fedha tulizonazo kwa miradi yenye tija na kusubiri hizo za kubahatisha kwa miradi ambayo si ya lazima sana kwa wakati huu. Wakuu naomba mnisaidie!
   
Loading...