Nini kimewakumba Maswahiba wa Lowassa; Yusuph Manji na Rostam Aziz?

Wadau, amani iwe kwenu.

Mtakumbuka kuwa, katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, Waziri Mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu kutokana na kashfa za ufisadi wa Richmond, Edward Lowasa, alitengeneza mtandao wa wafanyabiashara ambao ndio waliokuwa wanamfadhili kwenye harakati zake za kisiasa. Maswahiba hao walikuwa wanampa mabilioni ya fedha Edward Lowasa akiwa ndani ya CCM na hata baada ya kuhamia CHADEMA. Hawa ndio walioratibu kauli mbiu ya ULIPO TUPO.

Hata hivyo, baada ya Uchaguzi wa Oktoba 2015, maswahiba hawa inaelekea hesabu zao hazipangiki. Rostam Aziz inadaiwa kuwa amekimbia nchi tangu Septemba 2015 na haijulikani yupo wapi kwa sasa ingawa baadhi ya taarifa zinadai kuwa yupo Uingereza na wengine wakisema yupo Uarabuni na wengine wakisema yupo Marekani. Wengine wanadai kuwa Rostam bado yupo nchini isipokuwa kwa sasa ameamua kujifungia tani kwa vile mambo yake kibiashara yanaenda hovyo. kafulia.

Yusuph Manji, Diwani wa Mbagala Kuu, aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga kabla ya kuachia ngazi hivi majuzi baada ya wazee wa Yanga kushtuka dili la kumkodisha timu kwa miaka 10, inadaiwa kuwa hayupo Tanzania kwa sasa. Manji amelazimika kuondoka nchini kutokana na msuguano ulioibuka ndani ya klabu ya Yanga. Aidha, kabla ya hali hiyo, Yusuph Manji aliamua kujitoa kuongoza Quality Group, kampuni ambayo inadaiwa kutumia mwanya wa Manji kuongoza Yanga kuikopesha timu hiyo mabilioni ya fedha ambapo mpaka sasa timu hiyo inadaiwa Bilioni 5. Baadhi ya wana Yanga wanahoji, inakuwaje mtu ambaye aliahidi kuisaidia Yanga aidai fedha zote hizo? Ina maana kwa miaka yote Manji aliyoongoza yanga, timu haikuwa na mapato yoyote hadi deni limefikia kiasi hicho? Je hilo deni limetokana na nini? Wanachama wengine wameomba TAKUKURU kuchunguza deni hilo.

Kwa ujumla, hawa marafiki wa Lowasa ni dhahiri kwamba walikuwa wanafanya biashara kijanja ujanja na ndio maana walikuwa wanatumia fedha zao hovyo hovyo kufadhili kampeni za fisadi Lowasa.

Kutoweka kwa Manji, Rostam pamoja na akina Karamagi kumeenda sambamba na kufunga mdomo Edward Lowasa. Kwa sasa mwanasiasa huyo hayupo kabisa kwenye ulimwengu wa siasa na hata hizi harakati za CHADEMA kutaka kushika UKUTA Septemba Mosi ameamua kujiweka kando.

Ni wakati sasa wa Lowasa kujitokeza hadharani na kuwaeleza Watanzania nini kimewasibu Maswahiba wake. Maana kule Mbagala Kuu wametapeliwa kwa kumpa Manji Udiwani kwa ahadi hewa. Yanga nao wametapeliwa. Na inawezekana na Lowasa naye katapeliwa.
Siku si nyingi nao watakodi nafasi ya kugombea uraisi kupitia chadema ili Mbowe na genge lake wawasafishe
 
Mkuu Lizaboni, si umesikia hiyo ya watu kufanyiwa uhakiki wa mali kwa mara ya pili?

Maana watu wanampigapiga chenga tu mama Kaganda kama sungura.

Hii ya safari hii ndiyo itatoa picha halisi ya mafisadi walio ndani ya CCM na uhusiano wao na wale walioko nje ya serikali na washirika wao.

The net is closing in, it is intelligence warfare.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Mtakumbuka kuwa, katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, Waziri Mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu kutokana na kashfa za ufisadi wa Richmond, Edward Lowasa, alitengeneza mtandao wa wafanyabiashara ambao ndio waliokuwa wanamfadhili kwenye harakati zake za kisiasa. Maswahiba hao walikuwa wanampa mabilioni ya fedha Edward Lowasa akiwa ndani ya CCM na hata baada ya kuhamia CHADEMA. Hawa ndio walioratibu kauli mbiu ya ULIPO TUPO.

Hata hivyo, baada ya Uchaguzi wa Oktoba 2015, maswahiba hawa inaelekea hesabu zao hazipangiki. Rostam Aziz inadaiwa kuwa amekimbia nchi tangu Septemba 2015 na haijulikani yupo wapi kwa sasa ingawa baadhi ya taarifa zinadai kuwa yupo Uingereza na wengine wakisema yupo Uarabuni na wengine wakisema yupo Marekani. Wengine wanadai kuwa Rostam bado yupo nchini isipokuwa kwa sasa ameamua kujifungia tani kwa vile mambo yake kibiashara yanaenda hovyo. kafulia.

Yusuph Manji, Diwani wa Mbagala Kuu, aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga kabla ya kuachia ngazi hivi majuzi baada ya wazee wa Yanga kushtuka dili la kumkodisha timu kwa miaka 10, inadaiwa kuwa hayupo Tanzania kwa sasa. Manji amelazimika kuondoka nchini kutokana na msuguano ulioibuka ndani ya klabu ya Yanga. Aidha, kabla ya hali hiyo, Yusuph Manji aliamua kujitoa kuongoza Quality Group, kampuni ambayo inadaiwa kutumia mwanya wa Manji kuongoza Yanga kuikopesha timu hiyo mabilioni ya fedha ambapo mpaka sasa timu hiyo inadaiwa Bilioni 5. Baadhi ya wana Yanga wanahoji, inakuwaje mtu ambaye aliahidi kuisaidia Yanga aidai fedha zote hizo? Ina maana kwa miaka yote Manji aliyoongoza yanga, timu haikuwa na mapato yoyote hadi deni limefikia kiasi hicho? Je hilo deni limetokana na nini? Wanachama wengine wameomba TAKUKURU kuchunguza deni hilo.

Kwa ujumla, hawa marafiki wa Lowasa ni dhahiri kwamba walikuwa wanafanya biashara kijanja ujanja na ndio maana walikuwa wanatumia fedha zao hovyo hovyo kufadhili kampeni za fisadi Lowasa.

Kutoweka kwa Manji, Rostam pamoja na akina Karamagi kumeenda sambamba na kufunga mdomo Edward Lowasa. Kwa sasa mwanasiasa huyo hayupo kabisa kwenye ulimwengu wa siasa na hata hizi harakati za CHADEMA kutaka kushika UKUTA Septemba Mosi ameamua kujiweka kando.

Ni wakati sasa wa Lowasa kujitokeza hadharani na kuwaeleza Watanzania nini kimewasibu Maswahiba wake. Maana kule Mbagala Kuu wametapeliwa kwa kumpa Manji Udiwani kwa ahadi hewa. Yanga nao wametapeliwa. Na inawezekana na Lowasa naye katapeliwa.

Duh! Kumbe na Manji naye ni team Lowasa? Nilikuwa najua Rostam Azizi tu, kwa hiyo kama Lowasa angeshinda ufukwe wetu wa Coco Beach sasa hivi ungekuwa mali ya Manji? Kweli Mungu mkubwa kila siku anazidi kutuonyesha jinsi tulivyolikwepa tufe kubwa kwa kuitosha Team Lowasa!
 
Umbea,majungu,wizi,unaa,na ushoga unazaliwa ,unapikwa na unatengenezwa ccm.Chama cha vijana majizi na mafisadi by Uvccm
 
Duh! Kumbe na Manji naye ni team fisadi Lowasa? Nilikuwa najua Rostam Azizi tu, kwa hiyo kama fisadi Lowasa angeshinda ufukwe wetu wa Coco Beach sasa hivi ungekuwa mali ya Manji? Kweli Mungu mkubwa kila siku anazidi kutuonyesha jinsi tulivyolikwepa tufe kubwa kwa kuitosha Team Mafisadi Lowasa!
Sahihi kabisa Mkuu. Ndio maana Manji anaweweseka sana. Hesabu zake hazijakaa sawa
 
Duh! Kumbe na Manji naye ni team fisadi Lowasa? Nilikuwa najua Rostam Azizi tu, kwa hiyo kama fisadi Lowasa angeshinda ufukwe wetu wa Coco Beach sasa hivi ungekuwa mali ya Manji? Kweli Mungu mkubwa kila siku anazidi kutuonyesha jinsi tulivyolikwepa tufe kubwa kwa kuitosha Team Mafisadi Lowasa!

Raisi aliliongelea suala la Coco Beach katika moja ya hotuba zake za mwanzo kabisa baada ya kuapishwa.

Hivyo hili suala lilijitatua lenyewe kwenye zile hatua za mwanzo.
 
Mzee Makamba alisema "Anamwaga mapesa makanisani, misikitini, akiulizwa mapesa unayatoa wapi, anadai marafiki zake wanampa, hawa marafiki wakupe pesa wewe ni shemeji yao umewaolea dada yao".
yule jamaa kutoka genge la kijani aliyegawa cash kutoka kwenye briefcase kwenye Iddi na mwenzake mdogo ambaye hivi juzi hapa kaahidi kuwakatia Bakwata bakuli lililojaa 5B, nao ni mashemeji siyo?

poa.
 
Huwa mimi siwashangai sana watu wa ccm kwani huko kuna watu wa aina mbili wapo watu wajanja saana na wapo wajinga sana na ni kundi kubwa la wajinga lisilotambua chochote lenyewe limekaa kusikiliza maongezi ya wajanja na wao kuyatoa kwa wengine kama yalivyo bila kujua wakati wenzao wanaongea kama porojo wao huchukulia kweli na kujifanya wajuaji.ukitaka kujua hili hebu angalia huu uzi anasema rostam kafulia sasa la kujiuliza rostam alikuwa anamiliki kampuni gani na ngapi?je hizi kampuni zimekufa au bado zipo.Rostam anahisa kwenye makampuni ya uchimbaji madini nje na ndani ya nchi ana kwenye kampuni ya vodacom anabiashara kubwa kubwa nje ya nchi na alishakuwa katika kumi bora ya matajiri africa eti leo anatokea mtu anasema kafulia kweli ukiwa ccm ni lazima ujitie uchizi ndio uishi
 
Mzee Makamba alisema "Anamwaga mapesa makanisani, misikitini, akiulizwa mapesa unayatoa wapi, anadai marafiki zake wanampa, hawa marafiki wakupe pesa wewe ni shemeji yao umewaolea dada yao".
Duh! Badilisheni sasa hata ubeti,maana huu wimbo Lowassa Lowassa sasa unachuja!
 
Back
Top Bottom