Nini kimetokea kwa Melody za CHADEMA kwenye Mitandao ya simu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kimetokea kwa Melody za CHADEMA kwenye Mitandao ya simu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyota Njema, Apr 6, 2011.

 1. N

  Nyota Njema Senior Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau,

  Sasa ni muda mrefu kidogo toka melody za nyimbo za uhamasishaji za CDM kutoweka kwenye mitandao ya simu hasa Airtel bila kutolewa sababu yoyote. Jambo hili limewasikitisha wadau wengi mashabiki wa chama hiki chenye mvuto wa pekee hapa nchini, imefikia mahali wengine wameamua kuweka picha za CDM kwenye simu zao ili simu ikiita picha hiyo itokee kama njia ya kujifariji kutokana na kukosa melody hizi ambazo zilipendwa sana.

  Wadau na hasa wale walioko jikoni (Airtel), tunaomba watujulishe ni nini kimetokea hasa na ikizingatiwa kuwa watumiaji walikuwa wanazilipia pindi zitumikapo, kwa nini wamejinyima biashara hii? Tunajua kuwa mtandao kama Vodacom ambao fisadi RA ana hisa haungeweza kuwa na nyimbo hizi za kiharakati na mapinduzi ya kuleta haki kwa wanyonge ndani ya nchi hii, je Airtel nako kumeingiliwa na hawa mafisadi au mtandao huo umetishiwa na watawala?

  Wadau, naomba michango yenu kwenye hili maana sidhani kama ni haki kuwanyima Watanzania haki yao ya kuonyesha hisia zao na mapenzi yao kwa kile wanachokiamini na kukipenda. Na kama kweli melody za nyimbo haziruhusiwi kwenye mitandao, mbona melody nyingine za nyimbo za kawaida bado zinasikika kwenye simu? Wapenda haki ninawaomba tudai hili ikibidi hata kwa kutumia nguvu ya umma dhidi ya ubabe huu wa kijinga wa hawa watawala wabovu kama itakuwa kweli wamezipiga marufuku kwenye mtandao wa Airtel!
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,724
  Likes Received: 979
  Trophy Points: 280
  Mmh sina hoja hapa
   
 3. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wewe hujui kuwa serikali in hisa airtel? Tafakari, chukua hatua.
   
 4. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ninamfaham pale mtu wa VAS, ngoja nimuulize then nitakujuza mdau!
   
 5. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, nimeongea na jamaa hapa, anaomba sample number ya mtu ambae ameomba hiyo hudumba akashindwa kuipata. kama unaweza nitumie sample mumber moja au mbili za airtel ili nimtumie, then I will tell you what exactly happen
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,486
  Likes Received: 1,850
  Trophy Points: 280
  natumaini wateja wote wa airtel wataitumia hii back ringtone!weka code no yake hapa mkuu
   
Loading...