Nini kimetokea kati ya Kenya na South Sudan?

Mkataba umeandaliwa adis Ababa kumbuka Ethiopia imo katika harakati ya kufungua uchumi wake na Kenya ni jirani mhimu Sana katika uchumi wa Ethiopia ,nyie pambaneni na hali yenu tumewawachia Burundi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesahau kusema kuwa mlituachia deal la mabilioni ya dola la EACOP na Railway link to Rwanda. SGR to UG na yenyewe kuna dalili mnaeza tuachia pia. Lately Kenya mmekua na roho nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kenya na South Sudan ni kati ya mataifa mawili yanayo share muingiliano mkubwa wa watu na mipaka baina yao kwa upande wa kaskazini mwa Kenya, nafikiri pia kuna Jamii moja inayopatikana pande zote mbili kama kwa maasai upande wa Tanzania na Kenya
View attachment 1034127
Baada ya kupata kujitenga na Sudan na kua Taifa lingine, South Sudan ilikua beneti sana na Kenya kwa kila jambo pia Kenya imeshiriki pakubwa kuisaidia South Sudan kujitegemea na mpaka viongozi wa South Sudan walikua wakiishi Kenya Nairobi kwa kipindi kirefu wao pamoja na jamaa zao wakati na baada ya kutengana na Sudan pia kuna idadi kubwa tu ya wakimbizi wa South Sudan wanaoishi Kenya

Wananchi wa South Sudan wanamiliki vitega uchumi vingi tu nchini Kenya lakini siku za hivi karibuni nchi hizi mbili zimeonekana kupunguza ushirika wao kwa kasi ya kutosha au labda tuseme Kenya ina migogoro na kila jirani, Uganda hawako sawa sababu ya Migingo na uhusiano umekua mbaya kiasi la kuwanyima bomba la mafuta na reli ya SGR , Somalia ndio kama mjuavyo wanachukua bahari almost robo ya Kenya na mgogoro umefikia hatua ya kufukuza mabalozi, kule Ethiopia wamekiuka mkataba waliowekeana kwa Ethiopia kukataa kutumia bandari ya Mombasa na bandari waliyoandaliwa ya Lamu kwa Ethiopia kukimbilia Eritrea na Djibouti wazi wazi.
View attachment 1034128
Nini kimeipata Kenya na majirani zake, ni kwanini kila jirani hawapo kwenye good terms na Kenya na wote wanaonekana kutaka isolation na Kenya na sio Kenya isolated them, nimetafakari kwa kina nikagundua Kenya ina matatizo makubwa sana ambayo yanaigharimu pakubwa kiuchumi na kisiasa vibaya mno.

Ni jana nashangaa kuona ujumbe mzito kutoka South Sudan ukikimbilia Tanzania na kuiruka Kenya pua na mdomo kwa kuja kutaka msaada wa Tanzania kwa masuala ambayo Kenya wanayaweza vizuri mno

Ujumbe huu mawaziri wa South Sudan umetenga millions of dollars kwaajili ya wataalam wa Tanzania kwenye masuala ya elimu, kilimo, diplomacy, mazingira, utamaduni na amani, wameahidi donge nono na maslahi mapana kwa wabobezi wa kitanzania kwenye hizo kada waende South Sudan mwezi ujao kuhudumu kwenye sector nyeti hizo kwa mamia.

Baada ya kuliona hili ndipo nilipo rejea diplomacy situation kati ya Kenya na majirani zake, nini tatizo?
Wameona Tanzania pia ni nchi yenye big pontential ususani kwenye swala la usamabazaji wa chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebwanaee nimeangalia clip naona hili deal litanifaa sana vipi tunafikaje huko me napenda sana adventure nafikili naweza kupata hii chance huko Juba

Mradi kama upo sawa kwa fani yako na wakati huohuo uwe ‘fluent in written and spoken English’ basi usiwe na shaka nafasi zipo. Hii ni kwa sababu bila Kiingereza safi, hakuna kupeleka mguu wako kule!!!!!hatutaki kuiambisha nchi yenye maelfu ya wasomo wa ngazi ya chuo kikuu!! Just be on your marks, get set and wait for the order “go”!
 
Museveni akiwa mugwana hata mafuta ya SS yatapita uganda hadi tanga.
Hongera SS & TZ. HAKUNA mtu aliye na akili timamu anaweza piga dili kama hizi na fisadi kama kenyatta

Ni aibu kusema Mhe Kenyatta ni fisadi wakati anaongoza nchi democratically na ameweza kufanya shillingi ya Kenya kuwa imara duniani, Kshs. 99.00(ninety nine)= dollar 1(one dollar) wakati Tz shs 2400.00(two thousand four hundred) = One dollar(1)!!!empty tins make a lot of noise literarily means debe tupu hupiga kelele)!
 
Wakenya wanapenda kuwaringia Watanzania sana.
Sasa swali nyeti ni je SS hutumia Kiswahili au kingereza juu hapo Wakenya na Waganda wametuchapa kama mbwa msikitini.
 
Ni aibu kusema Mhe Kenyatta ni fisadi wakati anaongoza nchi democratically na ameweza kufanya shillingi ya Kenya kuwa imara duniani, Kshs. 99.00(ninety nine)= dollar 1(one dollar) wakati Tz shs 2400.00(two thousand four hundred) = One dollar(1)!!!empty tins make a lot of noise literarily means debe tupu hupiga kelele)!
Wewe huna unalojua Kuhusu uchumi, kuimarika kwa shilingi kuna maana gani kama exports zako zinazidi kupungua na imports zinazidi kuongezeka?.

Kenya unemployment inazidi kila mwaka, wananchi wanazidi kukamuliwa kwa kutozwa kodi, nchi inazidi kukopa ili kulipa madeni ya nyuma, uwezo wa kujilisha unazidi kupungua hadi rais wao analalamika, rushwa inazidi kushika kasi, hali ya usalama nchini.

Unafahamu kwamba shillingi ya kenya ni "managed" kwa mujibu wa taarifa ya IMF? Shilling ya Tz ni free market floating
 
Hivyo viwanda ambavyo mtamiliki 50/50 atajenga nani!? Ethiopia wakina Mo na Bakhressa wao ni wachina. Yani kama Kenya mnaona wa Ethiopia nima industrialist basi wote mmelewa kama raisi wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Do you know how free trade areas work ? Kampuni yoyote ikijenga kiwanda hapo iraruhusiwa kuuza bidhaa ndani ya Kenya na ndani ya Ethiopia bila kulipa tarrif yoyote zaidi... Ni Kampuni gani itakataa kujenga kiwanda mahali ambapo wako na mguu mmoja Ethiopia na mwengine Kenya... Yani itakua hakuna haha ya Kampuni za Kenya kujenga kiwanda Ethiopia (kama Ile Kampuni ya kutengenezwa biscuits ilivyofanya, itakua inajenga hapo moyale na Una supply Ethiopia na Kenya....

Tukicheza hii game vizuri tunaweza hata tukaweka free dry port hapo (kama vile Dubai) na bidhaa za hapo zone bei ya Chini kabisa
 
Wewe huna unalojua Kuhusu uchumi, kuimarika kwa shilingi kuna maana gani kama exports zako zinazidi kupungua na imports zinazidi kuongezeka?.

Kenya unemployment inazidi kila mwaka, wananchi wanazidi kukamuliwa kwa kutozwa kodi, nchi inazidi kukopa ili kulipa madeni ya nyuma, uwezo wa kujilisha unazidi kupungua hadi rais wao analalamika, rushwa inazidi kushika kasi, hali ya usalama nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umesahau Kenya inatoa kila mwaka wasomi wazuri wa hali juu na kwa sababu ya msingi mizuri ya shule zao, maelfu kwa maelfu ya Wakenya wanafanya kazi nchi za nje, home remittance kutoka Ughaibuni inazidi total income zinazongizwa na Watalii Tanzania! Hii inaonyesha kuwa Kenya ina export brain sana mpaka wengine ni Wabunge kule Australia!!!! Zaidi ya Wakenya millioni moja wanafanya kazi Mashariki ya kati na namba kubwa zaidi ya hiyo wanafanya kazi Marekani ya Kazikazini(North America)!! Linganisha sasa upendavyo wewe!
 
Mkenya na lifake id la 30
 
Back
Top Bottom