Nini kimepelekea kupungua/kuisha kwa ujambazi na wizi mitaani?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,554
44,723
Hili swali najiuliza sana kwanini matukio ya ujambazi yamepungua sana Kama sio kuisha kabisa.ukisema kwamba jeshi la polisi limeimarisha ulinzi bado haingii akilini kwani maeneo mengi tu hakuna Doria miaka yote mpaka kesho.

Labda tufanye watu hawana hela cash ndio maana majambazi hawajisumbui ila pamoja na hilo tungesikia hata nyumba zinavamiwa Watu wanasepa hata na tv flat wanaenda kuuza maana maisha bado ni magumu.

Au tuseme Mheshimiwa Rais Magufuli amesababisha hii hali ya uhalifu wa kuiba majumbani kwa watu uishe - how? Kwamba ameongeza ajira kiasi wahuni wameamua kuacha ujambazi?
 
Teknolojia imekua sana.

Mipango ya wizi iliyokuwa inafanywa na watu wa ndani inabainika mapema sana.

Na kila mmoja kwa sasa ni muoga kufanya njama ya kufanya uhalifu maana watu hawaaminani.

Nchi nyingi tu uhalifu umepungua. Hata Ugaidi kule Somalia umepungua.

Tumshukuru Mungu kwa kuwaumba wanadam miongoni mwetu wenye uwezo wa kugundua teknojia ya hali ya juu na sasa tunakoelekea kila jambo litakua linabainika kwa haraka zaidi.
 
Waibe nini na kila mtu njaa kali by the way sasahivi wenye vijisenti wanamiliki tunguri na bastola na bunduki ukienda kuiba gari unasinzia, ngombe ndio kabisa utazunguka nao mpaka kunakuchaaa kama unabisha njoo mtaani kwetu Ilagala Uvinza.
 
waibe nini na kila mtu njaa kali by the way saivi wenye vijisenti wanamiliki tunguri na bastola na bunduki ukienda kuiba gari unasinzia,. ngombe ndio kabisa utazunguka nao mpaka kunakuchaaa kama unabisha njoo mtaani kwetu ilagala Uvinza.
Naunga mkono hoja.

Mnapanga kabisa kwenda kuiba nyumba fln, mda unafika wa kwenda, mkifika hilo eneo mnakuta mnaona kichaka tena kinaungua..au mnakuta ni soko na watu wamejaa sana! Inabidi mgeuze.

Kuna majamaa waliiba ngombe wa mzee mmoja kule tabora, ile kutoka tu nje ya ule mji wa yule babu, ng'ombe wakagoma kutembea ni wanalia tuuu halafu wakakaa chini kabisa, piga na wewe wapiii, ni wanalia tu...majamaa ndukiiii!
 
Mbinu bora ya watawala ya kukabiliana na ujambazi nchini... 'kamata haraka haraka'.

Kauli mbiu hii imesaidia sana kushusha kasi ya ujambazi Tanzania.

Sheria zilizopo za kimahakama ni butu sana kudili na kesi za kijambazi na kisha kumtia hatiani, kwanza kupata ushahidi na vielelezo vya kutosha kupelekea jambazi kushindwa kesi ni ngumu kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano, hivyo kumpatia ahueni jambazi katika hukumu na kukandamiza waathirika wenye haki.

Kwa hiyo mbinu iliyopo ni majambazi kuuawa bila ya kufikishwa mahakamani, hiyo inabalansi na inaondoa lawama kwa raia wema kuilaumu serikali.

Hilo siyo jambo la siri tena, ukikutwa na silaha katika tukio la ujambazi, hata uitupe ujisalimishe lazima ufie kwenye geti la hospitali kabla haujafika mapokezi.

Na hiyo ndiyo dawa.

Anayedai haki za kibinadamu, aanze yeye kuwatendea haki za ubinadamu wenzake.
 
Kwenye suala la ujambazi kiukweli kabisa pongezi zangu zimuendee Rais John Pombe Magufuli.

Sera yake ya kuwataka askari wawanyangànye majambazi silaha zao kabla hawajasababisha madhara kwa raia wema imesaidia sana kupunguza matukio ya ujambazi hapa nchini.
 
Wale wajaamaa wanaopuliza dawa (vibaka) na kuingia ndani kuchukua TV flat screen na vito vya thamani ndio wako mtaani kwa wingii.... hawa jamaa washenzi sanaa, wakiingia wanawakuta mko bila kyupiii-teiteii wanatazama na kusepaa.

Kuna miaka ilikuwa ukiamka asubuhi bila kusikia sauti ya "........mlango wa chuma hauna hurumaaa" unajiuliza imekuweje.

Wizi ule wa kukwapuliwa fedha ukiwa umetoka bank nao na muda sijausikia.

Anyway big up to all who have managed to handle the situation.
 
ile 'fyagia fyagia na kuwalaza salama' imeokoa jamii

~ Urahisi wa kufanya ujasiriamali
~ Biashara ya boda boda kwa vijana

Na sera ya 'matajiri kuishi kama mashetani' imefanya nao majambazi waishi kama wako jahanamu so wengine pia wamestaafu
 
Pale mtukufu Rais Magufuli aliposema kila mtu afanye biashara kwa Uhuru bila kupigwa na mgambo ndiyo ulikuwa mwisho wa wizi na ujambazi.

Vijana hela ya kula haiwapigi chenga sana.

Wamebaki mitaa ya ufipa tu ndiyo wenye njaa baada ya kutapeliwa na Lissu.
 
Back
Top Bottom