Nini kimemkuta prof. Mwakyusa wa wizara ya afya!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kimemkuta prof. Mwakyusa wa wizara ya afya!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Nov 24, 2010.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kati ya mawaziri wa serikali iliyopita ambao mimi binafsi niliona walifanya kazi zao kwa uadilifu na hawakua na doa ni prof. David Mwakyusa aliyekua waziri wa afya. Nimepigwa butwaa kuona jamaa kapigwa chini. Naomba maoni yenu wadau wa JF.
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Tofauti za kiutendaji, jamaa ni mchapakazi na mshkaji alikua anataka vimeo kama Soooofiiiiiiiiiiiii na yule mwenye jina la vurugu
   
 3. F

  Fareed JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama kuna kosa lolote ambalo Prof. Mwakyusa alifanya. Nahisi kuachwa kwake kwenye cabinet kunatokana na ukweli kuwa tayari Kikwete ameteua mawaziri wawili kutoka mkoa wa Mbeya -- Prof. Mark Mwandosya na Dr. Harrison Mwakyembe. Huenda waliona ingekuwa ngumu kuwa na mawaziri watatu kutoka mkoa huo mmoja. Wakati wa kuteua mawaziri, huwa wanaangalia pia na proportional representation ya kiasi fulani ili angalau isionekane mkoa mmoja umependelewa kupewa mawaziri wengi. That said, nadhani mikoa kama Zanzibar (yes, I call it a region), Kilimanjaro na Morogoro imetoa mawaziri wengi safari hii.
   
Loading...