Nini kimekupata mbunge wangu Mh. Zitto Kabwe?

AKASINOZO

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
1,225
2,000
Yapata takribani miezi miwili ujaonekana kwenye media ukitupa nondo za maana hasa nyakati hizi ambapo mambo hayaendi vyema mfukoni mwa watu.

Ni majuzi tu mtia nia wa Moro mjini kajiweka pembeni kutoka chamani, je kama kiongozi wa chama unaona hali ni shwari?

Hata Katibu Mkuu wa CHADEMA katokezea kusemea hili swala la madam Dkt @Ziker aliyetumbuliwa wa pale upeponi karibu na mjengo mweupe we umeona sawa?

We ndo ulisimama na kijipambanua pale mjengoni Dodoma kuhusu hii sheria, je haya ya Max Melo hujayaona?

Nini kimekupata mh. Zitto Kabwe (MB)

Nipeni jibu nawasilisha hoja mezani.
 

AKASINOZO

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
1,225
2,000
Ukimya upo kwa viongozi wengi wa upinzani mimi nadhani wametuachia wananchi tuaone wenyewe na tuone umuhimu wao kwa vile tumekuwa tukiwalaumu hasa wale wa chama tawala. Sasa naamini umuhimu wao unaonekana.
Zito ni mtu makini sana hawez kusubiri upepo upite hivi ...kuna jambo au basi anaogopa kuzingirwa kama yuke arusha
 

Tiger One

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
569
225
Naamini sio kila jambo uongee hata ambalo hujawa na uhakikanalo.
Mwache Mh. Zitto atakuja kwa mda wake na kwa hoja zake alizo na uhakikanazo na kuuchangamsha ulimwengu wa kisiasa tena.
Jipange mkuu Zitto usikubali kukimbizwa kwa vishawishi kwani haohao ndowatakucheka ukichemka
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
15,827
2,000
Kuna akaunti ya TUNTEMEKE, inafanya kazi siku hizi. Ilikuwa imesimama kipindi cha nyuma.
---------
Sija elewa dukuduku lako mwanzisha mada...ebu rudia! please.
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
5,628
2,000
Unadhani kuchukuliwa saa tisa usiku unamwacha mke na watoto ni kitu rahisi?Harakati za jinsi hiyo zinatakiwa kufanywa na makapera,kama umeoa lazima mkeo akupe ruhusa kutoa toa maoni,maana huwezi jua,maoni ya mtu mzito kama Zitto yatachukuliwaje iwapo yataonekana kumjaribu asiyejaribiwa
 

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,276
2,000
Ni vizuri kujua kama yupo around maana sikuhizi watu wanapotea kusikojulikana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom