Nini kiliwapata Wamiliki wa hii Michuma? Tunyamaze hata kwa Dk. 3 kuwakumbuka

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Kwa sisi wazee wa zamani tunakumbuka sana Mabus haya...
1. Fresh ya Shamba
2. Safina
3. Kwacha
4. Zainabu
5. Kiswele
6. Matema
7. Masia
8. Tawaqal

Hawa walikuwa wakongwe wa barabara za nyanda ya juu kusini. Miaka hiyo ya nyuma. Nini kilitokea mpaka wakafirisika na kupotea katika ramani ya dunia?

Nakumbuka magari ya Kiswele yalikuwa yanaozea hapo Mabibo External. Sijui yakaenda wapi tena.

Je matajiri wa sasa wa Mabus kuna kitu wamejifunza toka kwa wakongwe hawa? Anyway...mi nashauri kwa siku moja katika mwaka bus zinazoenda njia hiyo zisimame mikumi kwa dk 3 kama kumbukumbu kwa malejendari hawa wa usafiri wa miaka hiyo
 
Biashara ziko hivyo. Ukishindwa kuendana na wakati unaweza kujikuta uko pembeni. Na biashara inaweza ikagoma ukahamia kwenye biashara nyingine. Kati ya hao uliowataja naamini kuna waliofilisika, kuna waliobadili majina, kuna waliobadili biashara na kuna waliofariki na biashara zao zikafa. Ni mambo ya kawaida katika ulimwengu wa biashara mkuu...
 
Kwacha still zpo wakuu mkoan iringa. Route za pori znafaida kubwa kuliko za kwenda ubungo.ila kiswele and the mentioned above naomba nikili RIP. NB: mmliki wa kwacha alikuwa babu yangu kafariki miaka 2 iliyopita ( ABEID CHARAMILA and group...)
 
Umenikumbusha huyu wa karibu na Lugalo dereva wake mmoja akijulikana Michael (RIP) na wa kule Frelimo mwanae nilisoma nae.Kwacha ilitufaa sana baada ya kuondokana na Railway
 
Kilichoua hizi gari ni kuzichezesha kwenye speed 120-140. Haya mambo ya speed governor yangekuwepo enzi zile hizi gari zikatembea kwenye 85kph, zingedumu mpaka leo..

Mind you, hizi gari kubwa engine zake zimeundwa ku rev kwenye green zone around 1800 rpm.. Ili kuzidi speed 100 ni lazima icheze kwenye rpm ya 2800 huko kitu ambacho kinaua vyuma mapema.

Mabasi ya sasa yatadumu kuliko ya zamani ( provided sio mchina) kwa kuwa hayakimbii sana.
 
Abood, dar express, ngorika ndiyo mabasi ninayoyakumbuka yamedumu kwenye game 30+ yrs. Hood naona kama anapotea, kampuni nyingine zilibadilishwa majina na watoto baada ya wazazi kufariki au kuchoka, mfano BM kulikuwa na basi linaitwa makundi(early 90s) dar Moro.

(Mswahili pekee enzi hizo), Kilimanjaro express ni mtoto wa sawaya express enzi hizo. Akina Osaka ni watoto wa ngorika. Kusini sina kumbukumbu kama kina matema beach, kiswele, nk waliacha legacy.
 
Sumry alikuja kuacha biashara ya mabasi na kulingana na maelezo yake, anasema biashara ilifika mwisho japokuwa alikuwa na mabasi 81 wakati anaifunga na akaamua kubadilisha biashara.

Hitimisho la biashara yake amelielezea katika madereva ambao amesema hawako committed na kazi wanazopewa na ni chanzo cha gari nyingi kupaki mapema.

Pili ameongelea ushindani ambao walikuwa wengi na amedai walikuwa wanashindana na mtu ambae hapigi gharama halisi za kazi, mathalan anapiga mahesabu ya diesel pekee na kufanya kazi hivyo kuumiza kwani nao itawabidi kushusha bei na amedai mpaka sasa nauli inayotumika Mbeya-Dar miaka ya 2000 takribani ni ileile.

Amesema wakati huo magari yalikuwa kidogo nafuu na ushindani haukuwa mkubwa ila sasa ni mkubwa sana na kazi ni ngumu hivyo hata mtu akichukua gari kupitia benki ni kazi sana na kiufupi hatoweza kwani basi haliwezi kuleta zaidi ya milioni 10 kwa mwezi ilhali basi la kichina kwa sasa ni milioni 360 hivyo angalau itahitajika miaka mitatu basi kulipa bila kuleta faida na hapo bado riba ya benki. Amesema kampuni zinabadilishana, inakuja mpya na wakiona changamoto wanatoka na nyingine inakuja. Amemaliza kwa kusema fursa bado ipo mtu akijipanga kwa kuleta mabasi mazuri, menejimenti nzuri na madereva wanaojielewa.

Maelezo haya aliyatoa Salum Sumry kwenye mahojiano Oktoba 2017 baada ya kuhamia kwenye kilimo kutoka kwenye biashara ya mabasi.
 
Abood, dar express, ngorika ndiyo mabasi ninayoyakumbuka yamedumu kwenye game 30+ yrs. Hood naona kama anapotea, kampuni nyingine zilibadilishwa majina na watoto baada ya wazazi kufariki au kuchoka, mfano BM kulikuwa na basi linaitwa makundi(early 90s) dar Moro.

(Mswahili pekee enzi hizo), Kilimanjaro express ni mtoto wa sawaya express enzi hizo. Akina Osaka ni watoto wa ngorika. Kusini sina kumbukumbu kama kina matema beach, kiswele, nk waliacha legacy.
Kumbe Makundi ndo BM aisee nilikuwa sijui..
 
Back
Top Bottom