Nini kiliwakosanisha watu hawa na Mwalimu Nyerere?

Kaldinali

JF-Expert Member
May 25, 2012
263
144
Wakuu,

Kama kuna anaejue ni nini hasa kilisababisha ugomvi kati ya hawa wazee wafuatao vs. Mwalimu Nyerere naomba atujulishe kwa historia fupi - kwa yoyote uijuayo. Na mwisho wa siku matokeo yalikuwa ni nini? nani alikuwa na haki na yupi alikuwa mkosaji?

Kasela Bantu
Christifer Kasanga Tumbo
Tuntemeke Sanga
Eli Anangisye
Lifa Chipaka
Wilfrem Mwakitwange
Mtemvu
Michael Kamaliza
 
Nasiki Kasanga Tumbo Huwa anasema hatamsahau Nyerere kwani alimfunga alipotoka jela akakuta mke wake ameolewa. Lakini Tumbo nae nasikia alipewa cheo cha ubalozi na Nyerere akenda huko akakaa kidogo akajiuzulu ili arudi nyumbani kuja kuanzisha chama cha upinzani-matokeo yake ndio hayo. Yana ukweli haya?
 
Mbona sijawah kuskia kwamba nyererea alikuwa na ugomvi ma adui na mtu? zaid ya iddi amin?
Oh! pole mamaaa eeh, hao wote walikuwa na mawazo tofauti na Nyerere pasipo kujali kuwa yalikuwa mawazo mazuri au mabaya ila kwa ufupi Nyerere hakupenda kukosolewa au kupingwa, Tumbo na Kasela Bantu walipinga kufutwa au kukomeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1965 tanzania ilikuwa na vyama vingi mpaka 1965. umemsahau Kambona ambaye hakukubaliana na azimio la arusha.
 
Joseph Kasela Bantu alikuwa ni mkuu wa mkoa wa kati ya Tabora au Shinyanga enzi hizo za Mzee Nyerere miaka ya sabini, siku moja aliitisha mkutano wa hazara, moja ya aliyozungumza katika mkutano huo ilikuwa kuhusu wezi wa mifigo na hasa ng`ombe. Alitaja kama kitu kuwasaka hao wezi wa mifugo ambao ilikuwa ni kero kweli kwa wasukuma.

Sasa inasemekana wasukuma na wanyamwezi walimnukuu vibaya huyo mkuu ukitilia maanani kabila hilo walikuwa mbumbu sana enzi na wengi walikuwa ni wapagani.

Baada tu ya mkutano wakatoka na silaha wakaanza kuwauwa hao wezi wa mifigo, wakawauwa wengi kama arobaini hivi, Mzee Nyerere kuuliza wakasema wamaamrishwa na Mkuu wa mkoa Kasela bantu wafanye hivyo. Nyerere alichofanya ni kumtia kizuizini mkuu huyo na ikawa ndiyo mwisho wake.
 
Kweli. Hicho ndicho ninachokumbuka.
 
Tuwaache wapumzike kwa amani.

Miaka mingi ijayo vizazi vijavyo vitakuja kuulizia kwanini Chattle master aligombana na Lissu!
 
John lifa Chipaka na Eliya Dunstan Chipaka walikua ni binamu wa Oscar Kambona. Kambona baada ya kutofautiana na Nyerere na kukimbilia Uingereza inadaiwa alitaka kuorganize coup.

Hawa ndugu zake wawili, John akiwa kepteni wa jeshi na Eliya akiwa luteni (kwa Eliya sipo sure sana) walihusika kurecruit wanajeshi na watu wengine ambao watakua upande wao siku coup ikiwa inafanyiwa kazi.

Walikamatwa kabla coup haijafaulu. John Lifa aliulizwa na hakimu "Mlimaanisha nini katika mpango wenu mlivyoandika 'Kumfuta Nyerere'?" Akajibu "Kumfuta kisiasa siyo kumuua"

Nafikiri hii ni sababu labda kama kuna nyingine.

Edit 1: Eliya ndiye alikua kepteni wa jeshi. Nimeconfirm.
 
Back
Top Bottom