Nini kilipelekea vijana wa Tanzania kuteka ndege ya ATC 1982 Mwanza?

Hawakujipinga ki ukamilifu, wangekua wamejiandaa vya kutosha wangefanikiwa maana viwanja vyetu vya ndege kipindi hicho kulikua hakuna usalama wa kutosha
 
Gaidi ni gaidi tu hao wanzanzibar waliteka ndege na visu wameishia kukamatwa wakati wakina osama waliteka ndege na visu vya vya mfukoni wameangusha world trade center
 
Mbona hii story niliwasikia clouds fm hawa jamaa na kama sikosei walisema walitua Arusha wakajua washaa fika!

mimi kwa jinsi nilivyo wasikiliza, shida yao kubwa ilikuwa ni kwenda ulaya kwa sababu ya ugumu wa maisha. Tatizo lao ni kutokujua mambo ya ndege matokeo yake rubani akafanya kazi ya kuwazungusha hewani tu. Baada ya hapo waliambiwa kuwa wanatua Adi Ababa ili wajaze mafuta kumbe wanatua Dar. Taa za uwanja zilizimwa na wakadakwa mmoja baada ya mwingine
 
Umechanganya matukio mawili tofauti.

Utekaji wa ndege umetokea mara mbili hapa nchini.

Sijachanganya mkuu, najua wengi wanahisi ni tukio la mwaka 1982

Hili hapa:

Tanzania Jet Hijacked; 2 Are Reported Killed

Published: February 27, 1982


Hijackers demanding the resignation of President Julius K. Nyerere of Tanzania seized a Tanzanian jetliner with more than 90 passengers aboard on a domestic flight Friday. They reportedly killed two hostages and forced the pilot to fly to Kenya and Saudi Arabia.

The Tanzanian Airlines Boeing 737 took off from Jidda early today after refueling and was reported heading for Rome. In Jidda, the hijackers said they were members of the Revolutionary Youth Movement of Tanzania and demanded President Nyerere's resignation, an airport spokesman said.

Foreign Minister Robert Ouko of Kenya said the hijackers had released three women and two children at the Nairobi airport. Mr. Ouko said the hijackers told him that they killed two of the people on the plane. The bodies were still aboard when the jetliner left Nairobi, Kenyan officials said.

It was not clear how many hijackers there were or what weapons they had.

Hijackers: (Leader) Mousa Memba died in 1992 while in jail in Dar es Salaam.

Yasim Memba (brother to Mousa): is a CCM stalwart, in Kawe, Dar es Salaam.
 
yaani baada ya kukamatwa wakaanza kuyamenya maembe yao na visu vyao waanza kuyala

Mkuu unajitafutia BAN ya kufungua mwaka, ngoja nikusamehe kwa leo kwa ku-edit post yako, rekebisha lugha!
 
Mkuu unajitafutia BAN ya kufungua mwaka, ngoja nikusamehe kwa leo kwa ku-edit post yako, rekebisha lugha!

Heshima kwako mkuu, naomba usiunganishe uzi huu na uzi unaozungumzia tukia la Jidda la mwaka 1982, haya ni matukio mawili tofauti!
 
mimi kwa jinsi nilivyo wasikiliza, shida yao kubwa ilikuwa ni kwenda ulaya kwa sababu ya ugumu wa maisha. Tatizo lao ni kutokujua mambo ya ndege matokeo yake rubani akafanya kazi ya kuwazungusha hewani tu. Baada ya hapo waliambiwa kuwa wanatua Adi Ababa ili wajaze mafuta kumbe wanatua Dar. Taa za uwanja zilizimwa na wakadakwa mmoja baada ya mwingine
kumbe serikali ya ccm ilianza zamani kutowatengenezea vijana sera na miongozo ya maisha bora
Miaka hiyo CDM wangekuwepo, wangeshasema ni vijana wa M4C hao ili nchi sitawalike
 
kumbe serikali ya ccm ilianza zamani kutowatengenezea vijana sera na miongozo ya maisha bora
Miaka hiyo CDM wangekuwepo, wangeshasema ni vijana wa M4C hao ili nchi sitawalike

Heheee ccm ya leo isipomtaja chadema haipigiwi makofi
 
Pilot alikuwa Captain Mazula (late) walikua na silaha za ukweli na sio maembe.. mazula alipigwa risasi mkononi lakin aliweza kuendelea na flight mpka wakafika
 
khaaaaaa maembe dodo?
UNAWEZA kuteka ndege bila silaha,ndege ikishakuwa airborne you just have to instill fear by eg claiming there is a bomb on board-hawa watekaji naona wali panic cause hata kama ndege ilitua DAR wange threaten kuua abiria and serikali ingelazimishwa kuiachia iondoke
 
Yericko kama kawaida yake anachanganya madawa.

Anachanganya hijacking ya kina Kisoda na ya kina Membe.
 
viwanja vyetu vya ndege vinausalama wakutosha?
ndio, viwanja vina usalama wa kutosha na teknolojia ya hali ya juu ndio maana makachero waliokuwa uwanjani walipata taarifa kwamba ndege imetekwa na inarudi Dar na wakajiandaa na kuwatuliza watekaji bila tukio, na ma pilot nao walikuwa very well trained kiasi cha kumfanya mtu ajisikie kwamba safari ya masaa manane inakuwa supplanted na safari ya dakika 45 (arusha Dar) bila watekaji kushtukia!

Well, unless story ni ya kutunga.
 
Bora wangeteka yenye dhahabu au pembe za ndovu wangekuwa mashujaa wa Taifa
 
Linatajwa kuwa moja ya majaribio yenye kustua vyombo vya dola vya nchi hii na linafananishwa na tukio la mnamo February 27, 1982 mjini Jidda lililoongozwa na Mousa Memba aliyekuja kufariki mwaka 1992 akiwa jela hapa Dar es Salaam


Japokuwa hadithi hubadilika badilika kila mtu akikusimulia, lakini kisa kinaelezwa hivi:

Vijana wanne wakizanzibar
waliovamia safari ya ndege ya Tz kutoka Zanzibar kuelekea Arusha, waliamua kuiteka ndege hiyo kabla ya kutua Arusha na kumwamuru rubani wa ndege hiyo awapeleke Ulaya,

Kutokana na kipigo, rubani alikubali na kuanza safari ya Ulaya,

Kinyume chake rubani aliwaleta Dar, akawaambia wapo nchi ya Ulaya huko na mafuta wameishiwa hivyo anatua ili wajaze mafuta,

Baada ya ndege kutua uwanja wa ndege Dar ulikuwa tayari upo chini ya ulinzi mkali, na wale vijana walikamatwa kama kuku kwani hawakuwa na silaha yoyote zaidi ya kisu, maembe dodo ambayo waliyatumia kama mambomu na bastola za bandia

Kiasi kwamba vijana walifanikiwa kuwatisha abiria wote nao wakaamini kuwa vijana wale walikuwa na mabomu na bastola kumbe matoi tu!

Japokuwa propaganda za kimagharibi zilibadili malengo ya watekaji ya kutaka kupelekwa Ulaya, sasa wao leo wanasema kuwa vijana waliiteka ndege ile ya Tz kwa lengo la kutaka Mwalimu Nyerere ajiuzuru wadhifa wake:

Hili linarudisha fikra zetu tujiulize kuwa viwanja vyetu vya ndege vinausalama wakutosha?

Hapo juu umetaja jaribio lilifanywa na Mussa Memba...hili halikuwa jaribio bali ni utekaji nyara wa mwanzo wa ndege ya ATC na ulifanikiwa..watekaji waliichukua ngege mjini Mwanza Tanzania na sio Jedah
waliiteka kuanzia mwanza na kuilazimisha kwenda London..huko hawa vijana walitaka Nyerere ajiuzulu....ndio watawaachia abiria...
kutokana na mazungumzo...ya hapa na pale walikubali kuwachia wale abiria wale abiria hawajawahi kwenda London na kutokana na hali ilivokua huku nyumbani ya kufunga mkanda mpaka kitobo cha kuongeza walipata cjisenti pale kuwasaidia na kununua angalau colgate na sabuni za kufulia ilikua siku kuu kwao...lakini inasemekana walipo fika airport walinyanganywa.....moja ya mazuri ya wakati wa enzi za zake....hawa jamaa walifungwa kule baadae wakaachiwa na kupata hifadhi ya kisiasa baada ya kuonekana kweli huko Tz hakuna haki za binaadamu
so haya ni moja katika matukio yaliyojaribiwa kumuondoa nyerere ikiwa ni pamoja na jaribio la kina Hanspope la kufanya mapinduzi
Juzi mmoja ya walifanya jaribio hilo Harry hanspope amefariki huko Canada..yeye aliposamehewa na Mwinyi alichagua kuishi huko
vijana kuna mambo mengi yamepita lakini yanafichwa ...lakini ni muhimu kuyajua kwani ndio historia na ni vema kila kitu kikajulikana ili vizazi nyetu vijue tumefikaje hapa tulipo
 
Hao watekaji walishindwa hata kuchungulia madirishani kuona wako wapi?

They were fools.

Sure, but we are greater fools. Anyway, hili lilikuwa tukio la pili la utekaji ndege . La kwanza "limefanikiwa" ndege imetuwa Heathrow airport, watekaji wamenyeshewa mvua kumi na judge mzungu hapo old Bailey. Mwalimu kapigwa butwaa, washenzi kweli hawa.
 
Back
Top Bottom