Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Mtchoro,
Ndiyo faida ya kuandika.

Umepata na wewe nafasi ya kuchangia histori ya nchi yetu.

Hebu soma hii hapo chini:

GEREZANI FAMILY DAY

Ahsanteni sana Wanagerezani kwa siku nzuri ya hii Jumapili khasa kwa ile biriani ya kumwaga.

Allah atuzidishie mapenzi na mshikamano.

Leo kwa mara yangu ya kwanza nimehudhuria Gerezani Day.

Kwa hakika ni siku ya kupendeza sana ingawa kwa namna fulani kuna majonzi kidogo yanakuja pale unapowafikiria wale ambao ulikuwanao udogoni mkicheza mpira Kidongo Chekundu na wao wametangulia mbele ya haki.

Kidongo Chekundu leo haipo lakini pamejengwa viwanja vya michezo.

Kwangu mimi ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria siku hii na In Shaa Allah naomba iwe narejea na kurejea kila mwaka hadi mwish wa umri wangu.

Laiti kama si kwa kuwa nipo katika Group hakuna ambae angenijua kwa sura ila watu wachache sana pengine wasiozidi hata watano.

Kutoka mwaka wa 1952 nilipozaliwa mimi Mtaa wa Kipata hadi leo miaka mingi imepita.

Kuna baadhi ya watu umri wangu na wengine chini kidogo nimeweza kuwatambua kwa sura zao kuwa zinakuja akilini lakini majina hayaji.

Ngoja nikuchukueni safari yangu ya Gerezani ilivyokuwa na nataka In Shaa Allah niifungamanishe na Dar es Salaam ile ya 1950/60 ambayo naamini wanagerezani wachache sana wanaijua kwani leo pale wengi niliowaona ni vijana sana.

Huenda wengine mimi nimecheza na baba zao.

Nimetokea nyumbani kwangu Magomeni Mapipa nyumba ya kwanza ambayo ina kumbukumbu kubwa kwangu ni pale nilipopinda kona kulia kuingia Mtaa wa Kipata (Sasa Mtaa wa Sykes).

Nimeacha kuitaja ofisi ya CCM ambayo pale ilikuwa ofisi ya African Association iliyojengwa kwa kujitolea kila siku ya Jumapili kuanzia mwaka wa 1929 – 1933.

Nyumba ya kwanza yenye kumbukumbu kubwa kwangu iko mkono wa pili yaweza kuwa ni nyumba ya tatu hivi kutoka Lumumba Avenue na Mtaa wa Sykes.

Leo hapo kuna kituo cha kuuza petroli.

Hii ilikuwa nyumba ya Liwali Abdallah Simba wa Songea ambae nyumba yake nyingine ilikuwa Mtaa wa Somali (Sasa Omari Londo).

Babu yangu aliishi nyumba hii miaka wa ya 1920 ingawa yeye alikuwa na nyumba yake Mtaa wa Mbaruku na Congo jirani na nyumba ya Aziz Ali.

Nyumba hiyo ndipo alipokulia baba yangu.

Umuhimu wa nyumba hii ni kuwa baba yangu kayaona yote ya harakati za uhuru akiwa pale na kanieleza mengi.

Mkabala na nyumba hii ni nyumba ya Kleist Sykes ambae katika video aliyotengeneza Mohamed Ghassani kampa jina, ‘’Mbuyu wa Mzizima.’’

Video hiyo nimekuwekeeni hapa kwenye Group toka jana usiku.

Mtakumbuka kuwa mliponikaribisha kuzungumza nilikuelezeni kuwa harakati za kuiokomboa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza zilianza nyumba hii.

Kleist alikuwa katibu muasisi wa African Association na aliishi nyumba hii na wanae wote walizaliwa hapo.

Ndani ya nyumba hiyo wakati wa TAA Ally Sykes mwaka wa 1953 alificha mashine ya kudurufu ambayo ndiyo aliyokuwa akichapa makaratasi ambayo Waingereza waliita ya ‘’uchochezi,’’ akawa anayatawanya kwa wananchi wajiunge na TAA ili TANU itakapokuja kuundwa mwaka wa 1954 iwe na wanachama wa kutosha.

Historia ya Ally Sykes sote tunaijua.

Katika nyumba hii ndipo siku chache baada ya kuundwa kwa TANU Ally Sykes na kaka yake Abdul walikaa mchana mmoja kumsubiri Mwalimu Nyerere aje kuwapa habari za usajili wa chama cha TANU.

Alipofika pale Nyerere aliwapa habari mbaya kuwa TANU imekataliwa usajili.

Nyumba ile haipo na badala yake kuna gorofa ndefu.

Jengo hili hili linahitaji kuwekewa kumbukumbu.

Nimeswali Msikiti wa Kipata na ukanikumbusha ule msikiti mdogo wa zamani.

Mkabala wa nyumba hii NO. 18 alikuwa akiishi mama yangu Mkubwa Bi. Mwanaisha Bint Mohamed ambako Nakioze alikuwa na genge lake akiuza mboga na matunda.

Hili jina "Naikioze," alipewa kwa kuwa wateja wake walikuwa wakilalamika kwa ughali wa bei za vitu vyake yeye akiwaambia, ‘’Acha usinunue nakioze.’’

Nyumba hii ilikuwa ya Bi. Mkubwa mmoja akiitwa Bint Salum.

Nakumbuka mwaka wa 1956 wakati Princess Margaret alipokuja Tanganyika.

Siku ile nilikuwa hapa kwa mama yangu mkubwa na kwa kuwa mtaa wa nyuma ni Mtaa wa Kitchwelle alikokuwa anapitishwa akitokea uwanja wa ndege nakumbuka sana kuwa mimi nilisimama mbele ya duka la Toti pamoja na umma mkubwa wa watu na wanafunzi wa shule kumpungia Princes Margaret tukiwa tumeshika, ‘’Union Jack,’’ bendera ya Uingereza.

Naingia Mtaa wa Sikukuu nakata kushoto kutokea Mtaa wa Sykes kulia kwenye kona ndipo ilipokuwapo nyumba ya Mzee Clement Mohamed Mtamila mmoja wa viongozi wa African Association aliyekuwa katika ya TAA na baadae Mwenyekiti wa TANU 1955.

Siku zile TANU ilikuwa na Rais na Mwenyekiti ambae alifanya kazi zaidi kama mwenyekiti wa Halmashauri ya TANU.

Mwalimu Nyerere alipoandikiwa barua ya achague mawili siasa au ualimu, barua ile ilijadiliwa kwenye kikao kwenye nyumba hii na mmoja wa wajumbe alikuwa Bi. Tatu bint Mzee ambae alikuwa anaishi Gerezani Mtaa wa Kirk Street sasa Mtaa wa Lindi.

Jengo hili linastahili kuwekea kumbukumbu.

Nimepita Mtaa wa Lindi kwenye kona kulikuwa na kinyozi Muingereza na pale palikuwa barza kubwa ya wana TANU wakikaa kuzungumza.

Hii ni sehemu muhimu ya kuwekewa kumbukumbu na hivi sasa kuna ujenzi pale wa kujenga ofisi ya CCM.

Ukiwa hapo nyumba ya Bi. Mruguru bint Mussa mama yake Abdul Syks unaiona ile pale na watu wengi wa Gerezani wanakumbuka kumuona Nyerere akipita pale kwa Muingereza kaongozana na Abdul Sykes wanakwenda kumsalimia Bi. Mruguru.

Wazalendo hawa wawili mara nyingine walikuwa wanasiamama hapo kutupiana maneno na wana TANU wenzao na ilipoanza Congress watatupiana makombora na wafuasi wa Zuberi Mtemvu aliyekuwa President wa Congress, kisha hao watapita.

Mtemvu alikuwa akiishi Mtaa wa Somali ambao sasa ni Mtaa wa Omari Londo.

Gereza ni ina kumbukumbu nyingi na ni muhimu sana kumbukumbu hizi zihifadhiwe kwa kizazi kijacho vinginevyo historia ya Gerezani yote itapotea.
Ninakubali mkuu lakini nikisoma Historia na ya kutafuta mwenyewe ni kwamba wakuja hao waliweza tu kuchungulia fursa maana toka Sykes alipoletwa Dar toka Pangani na Effendi Plantan walijiunga kwenye kundi la Wakuja ambalo lilikuwa linajikomba kwa Wahindi.

Tofauti na wenzao kama Kilwa Association au lile kundi la Wasukuma na Wanyamwezi ambao walikuwa wanataka haki ya weusi.
 
Wapi na lini Askari Mamluki ageuke Mzalendo na Mpigania Uhuru na akumbukwe kwenye historia ya nchi?
Si unajua upole wetu hatujaanza leo ndio maana Mgeni anaweza kuja Tanzania na akatamba sana akatufanya anavyojua. Wazulu na Wanubi walikuwa wanajiona wao ndio wao hapo Kariakoo wanajiweka kundi moja na Waarabu na Wahindi na timu yao Sunderland
 
Mwalimu wangu Sheikh Mohammed Said nimekusoma mahali ukieleza kutaka kuweka tazia ya MwanaMapinduzi na katibu mkuu wa Kwanza wa Afro Shiraz Sheikh Thabit Kombo.

Tafadhali naomba uiweke hapa kwa faida ya baraza.
 
Red...
Ikiwa unafikiri hivyo ni sawa.

Muhimu kwangu ni kuwa nimewapa watu nafasi ya kusoma historia ambayo wengi hawakuwa wanajua kuwa ipo.

Naamini wewe umejifunza mengi hapa jamvini.
Umelisha watu tangu pori kuwa nyerere alipokelewa na abdul.. ndio kutuamini hayo mengine.. wewe ungejikita kuandika kuhusu wazee wako na sio menginenyo.
 
Mzee Said kila wakati ninaposoma unapomjibu anayetaka kufahamishwa huwa naishia kujiuliza kama ni mimi tu huwa nashindwa kukuelewa.

Kwa mfano kwenye hoja ya Mkuu Nguruvi amehoji kama uandishi wa katiba ya TANU ni matokeo ya urafiki wa Seaton na Abdul, na je wazo la katiba ni la Abdul na Seaton ni mtekelezaji?...jibu ambalo ningelitegemea hapa ni 'kwa mfano' ndio katiba ya TANU ni matokeo ya urafiki wa Seaton na Abdul au Hapana......... badala yako umeanza tena kuhoji kama amewahi kumsikia Seaton akitajwa kwenye historia za TANU.

Anza kwa kuweka sawa kwanza hoja inayojitokeza kabla ya kuibua hoja yako mpya i naye mwenye hoja awajibike kutoa jibu kwa hoja yako.
Akishikwa urongo huanza kujitapa mara cambridge mara harvard nakutokujibu hoja husika
 
Mwalimu wangu Sheikh Mohammed Said nimekusoma mahali ukieleza kutaka kuweka tazia ya MwanaMapinduzi na katibu mkuu wa Kwanza wa Afro Shiraz Sheikh Thabit Kombo.

Tafadhali naomba uiweke hapa kwa faida ya baraza.
Thomas...
Ile taazia haifai kuwekwa hapa kwa kuwa muandishi Mlamali Adam alikuwa mkali kwake.
 
Akishikwa urongo huanza kujitapa mara cambridge mara harvard nakutokujibu hoja husika
Inside10,
Hawa Harvard na Cambridge ndivyo vyuo ambavyo ikiwa patatokea elimu mpya wao huitaka kujua kuna kipi kipya.

Kwa kuwa nilikuja na elimu mpya ndiyo wakanifikia si kuwa mimi nimejitapa hapana ni kile kitabu cha Abdul Sykes ndicho kilichowavutia lakini ni miaka mingi imepita.
 
Si unajua upole wetu hatujaanza leo ndio maana Mgeni anaweza kuja Tanzania na akatamba sana akatufanya anavyojua. Wazulu na Wanubi walikuwa wanajiona wao ndio wao hapo Kariakoo wanajiweka kundi moja na Waarabu na Wahindi na timu yao Sunderland
Mtochoro,
Babu yangu Salum Abdallah ni kizazi cha kwanza cha Mmanyema aliyeingia Tanganyika kama mamluki kutoka Belgian Congo.

Babu yangu ameshiriki kuongoza migomo mitatu dhidi ya Waingereza 1947, 1949 na 1960 pia kashiriki katika kuunda Tanganyika Railways African Union (TRAU)1955.

Kuwa yeye baba yake alitokea Congo hakukumzuia kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Of course hayawezi kuwa na maana kwako kwasababu hayalingani na lengo lako.
Haya ninayoandika yanamaana sana kwa wasomaji.

Nina uhakika Prof Shivji na Prof Saida, watakaa kitako kufikiri ikiwa kauli waliyosoma kwako kwamba Abdul alimpokea Nyerere ni upotofu . Sidhani kama wanaweza kusimama mahali na kuitetea!
Wewe unaweza kwasababu huna aibu, sijui kama wao wanaweza

Kwa Wanajamvi, hasa vijana haya yana maana sana kwao.
Kwanza , wanajifunza kusoma kwa kufikiri na kuunganisha mtiririko wa habari
Pili, inawakinga kumeza uongo bila makosa , kwamba, umri wao unatumika tu kuwa 'exploit'

Tatu, inasaidia pia 'wafuasi' wako wasome maandishi kwa uangalifu, kinyume chake wanaweza kuangukia pua
Sasa kama umeshindwa kuthibitisha uwepo wa katiba ya AA na TAA ya Abdul, wao wanaweza nini?

Muhimu zaidi ni kueleza jinsi Abdul Sykes alivyokuwa overrated na vitabu vyako katika jitihada za kumdunisha Nyerere. Kwa vigezo vyote Nyerere atabaki kuwa Nyerere na sifa zake na Abdul atabaki kuwa na sifa zake.

Huwezi kumfanya Abdul awe zaidi kwa kumnyanyasa au kumdhalilisha Nyerere

Nyerere anatetewa na historia, ambayo haiandikwi , kubumbwa au kufinyangwa.
Ni historia inayojidhihiri kwa muda na matokeo.
Ndiyo maana miaka 20 tangu afariki bado '' historia inamtetea'' akiwa amelala kaburini tuli

Kwamba alilishwa mayai kwa Sykes, na alivaa Kaptula au alipewa pesa za kununua ng'onda, au alikwenda sokoni na kikapu bila pesa, hayo hayaondoi ukweli mwingine wowote katika kuongoza harakati za uhuru

Ni Nyerere aliyebadilisha siasa za barazani na kuzipeleka majimboni , Tanganyika na UN. Siyo Abdul Sykes

Tena tukichimba zaidi, kubwa la Abdul ni kuongoza genge la wahuni kwenda kutandika wazee wake ili achukue utawala wa baba yake.

Hakuandika Katiba wala baba yake hakuandika. Hawakupeleka siasa mikoani zaidi ya Tandamti na Agrey.

Historia si hisia, tenzi au simulizi. Si mahoka au ngano, ni mtiririko wa matukio usiohitaji nakshi au uvumba.

Nawahi Magila, leo tunamuoza mtoto wa baba shangazi.
Hakika ww ni bingwa wa kusamabaratisha harakati za tandamti na aggrey
 
Hakika ww ni bingwa wa kusamabaratisha harakati za tandamti na aggrey
Inside,
Ikiwa umepima mjadala huu na umeona mimi nimesambaratishwa ni vizuri hapana neno ila ningependa kukufahamisha kuwa kuna vipindi 9 vitarushwa In Shaa Allah kwa njia ya video kuhusu historia hii.

Kipindi # 1 hicho kipo mtandaoni na kimevutia watazamaji wengi kuliko tulivyotazamia.
 
Nguruvi3 angekubali kuonekana ni vyema mngefanya mnakasha wa laivu.. hakika ungepat aaibu KUU
 
Wanajamvi,
Abdul Sykes hakuwahi kufanya mkutano wa hadhara popote pale nje ya Tandamti na kidongo chekundu
Na huo ndio ukweli mchungu kuwa...
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes aliwahi kuchaguliwa kuiongoza TANU tangu kuasisiwa kwake hadi uhuru unapatikana.
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes, aliwahi kusimama jukwaani akiinadi TANU tangu kuasisiwa kwake hadi uhuru unapopatikana.
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa TANU katika ngazi ya taifa, Jimbo, Wilaya hadi Kata (pamoja na mtaa wa Gerezani)
Ila ziko kumbukumbu ya Abdulwahid Sykes katika mambo matatu...
  • Kujitwalia madaraka kimabavu baada ya kuvamia ofisi za TAA mwaka 1948 na kuwatimua wazee wake kwa ngumi na mateke.
  • Kama mtoto wa mjini kuwania uongozi wa TANU mwaka 1953 akipimana nguvu na wakuja na kugalagazwa vibaya na Mwl. Nyerere.
  • Kumlisha mpwa wake hizi porojo za kuwataka Watanganyika kuwaenzi hawa walowezi kwamba ndio waliopigania uhuru wa taifa lao.
Inasikitisha kuwaona baadhi ya Watanzania wanameza hizi ngano za Mohamed Said akiitumia dini kama kinga kuficha ukweli wa historia ya Wazalendo waliojitoa mhanga kutetea maslahi ya Watanganyika dhidi ya Wakoloni.

Wengi anaowatajataja Mohamed Said kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika hawakuwa wazawa nyakati hizo na ama walikuwa ni walowezi au askari wa Wakoloni waliokodiwa kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika.

Mohamed Said anafanya hivyo akiamini kuwa uongo ukirudiwarudiwa siku nenda rudi kuna siku (over our dead bodies) unaweza kugeuka ukawa ukweli na miongoni mwa wazee wake wazawa wa iliyokuwa Tangayika ni wachache sana.

Mohamed Said hataki katakata kumpa heshima stahiki mwanzilishi, kiongozi na Rais muasisi wa AA mwaka 1929, msomi Mwl Cecil Matola, Mtanganyika, Mkristo na Myao moja ya makabila mahiri ya kusini mwa Tanzania.

Mohamed Said hamtaji kabisa, msaidizi wa Rais wa AA aliyepokea kijiti baada kifo cha ghafla cha Mwl Cecil Mtola na huyo si mwingine bali ni Ramadhani Ali , Mfanyabiashara, Muislaam na Mtanganyika kutoka kabila la Wazaramo.

Badala yake Mohamed Said kwa hila na makusudi na akijua fika anaeneza uongo, anadai muasisi wa AA alikuwa baba yake Abdulwahid Sykes, Kleist Sykes askari wa Wakoloni kutoka Afrika Kusini wa kabila ya Wazulu.

Hivyo hivyo Mohamed Said hampi umuhimu wowote mwanzilishi na Rais muasisi wa TAA mwaka 1948, msomi Dr Vedasto Kyaruzi, Mtanganyika, Mhaya ambaye ilibidi apewe uhamisho kutoka jijini Dar ili atengwe na wenziye.

Badala yake Mohamed Said anatutaka tumpe hashima zote mjomba na mtoto wa Kleist Sykes, Abdulwahid Sykes, Mzulu na askari wa KAR kama muasisi wa TAA, kisa? Kuwatimua wazee wake ofisini kwa ngumi na mateke.

Hivyo hivyo Mohamed Said hataki kumpa heshima stahiki Mtanganyika na msomi Dr. Julius Nyerere, Rais muasisi wa TANU na Baba wa Taifa aliyetuunganisha Watanganyika kwa umoja na mshikamano hadi tukapata uhuru mwaka 1961.

Badala yake Mohamed Said anataka tumuenzi mlowezi kutoka Afrika Kusini kwamba bila yeye TANU haingeasisiwa na madai ya uhuru yasingefanikiwa...shame, shame, shame kwa Mohamed Said na wote wanaomeza hizi porojo zake.

Hata hivyo nampongeza Mohamed Said kwani katengeneza sana hela na hizi porojo zake na kawateka wengi kweli kweli. Sasa naomba aeleze bayana ni kwa nini baada ya vita hawa Wazulu wakaamua kulowea Tanganyika.
 
Na huo ndio ukweli mchungu kuwa...
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes aliwahi kuchaguliwa kuiongoza TANU tangu kuasisiwa kwake hadi uhuru unapatikana.
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes, aliwahi kusimama jukwaani akiinadi TANU tangu kuasisiwa kwake hadi uhuru unapopatikana.
  • Hakuna ushahidi wowote kwamba Abdulwahid Sykes aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa TANU katika ngazi ya taifa, Jimbo, Wilaya hadi Kata (pamoja na mtaa wa Gerezani)
Ila ziko kumbukumbu ya Abdulwahid Sykes katika mambo matatu...
  • Kujitwalia madaraka kimabavu baada ya kuvamia ofisi za TAA mwaka 1948 na kuwatimua wazee wake kwa ngumi na mateke.
  • Kama mtoto wa mjini kuwania uongozi wa TANU mwaka 1953 akipimana nguvu na wakuja na kugalagazwa vibaya na Mwl. Nyerere.
  • Kumlisha mpwa wake hizi porojo za kuwataka Watanganyika kuwaenzi hawa walowezi kwamba ndio waliopigania uhuru wa taifa lao.
Inasikitisha kuwaona baadhi ya Watanzania wanameza hizi ngano za Mohamed Said akiitumia dini kama kinga kuficha ukweli wa historia ya Wazalendo waliojitoa mhanga kutetea maslahi ya Watanganyika dhidi ya Wakoloni.

Wengi anaowatajataja Mohamed Said kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika hawakuwa wazawa nyakati hizo na ama walikuwa ni walowezi au askari wa Wakoloni waliokodiwa kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika.

Mohamed Said anafanya hivyo akiamini kuwa uongo ukirudiwarudiwa siku nenda rudi kuna siku (over our dead bodies) unaweza kugeuka ukawa ukweli na miongoni mwa wazee wake wazawa wa iliyokuwa Tangayika ni wachache sana.

Mohamed Said hataki katakata kumpa heshima stahiki mwanzilishi, kiongozi na Rais muasisi wa AA mwaka 1929, msomi Mwl Cecil Matola, Mtanganyika, Mkristo na Myao moja ya makabila mahiri ya kusini mwa Tanzania.

Mohamed Said, hamtaji kabisa, msaidizi wa Rais wa AA aliyepokea kijiti baada kifo cha ghafla cha Mwl Cecil Mtola na huyo si mwingine bali ni Ramadhani Ali , Mfanyabiashara, Muislaam na Mtanganyika kutoka kabila la Wazaramo.

Badala yake Mohamed Said, kwa hila na makusudi na akijua fika anaeneza uongo, anadai muasisi wa AA alikuwa baba yake Abdulwahid Sykes, Kleist Sykes askari wa Wakoloni kutoka Afrika Kusini wa kabila ya Wazulu.

Hivyo hivyo Mohamed Said hampi umuhimu wowote mwanzilishi na Rais muasisi wa TAA mwaka 1948, msomi Dr Vedasto Kyaruzi, Mtanganyika, Mhaya ambaye ilibidi apewe uhamisho kutoka jijini Dar ili atengwe na wenziye.

Badala yake Mohamed Said anatutaka tumpe hashima zote mjomba na mtoto wa Kleist Sykes, Abdulwahid Sykes, Mzulu na askari wa KAR kama muasisi wa TAA, kisa? Kuwatimua wazee wake ofisini kwa ngumi na mateke.

Hivyo hivyoMohamed Said hataki kumpa heshima stahiki Mtanganyika na msomi Dr. Julius Nyerere, Rais muasisi wa TANU na Baba wa Taifa aliyetuunganisha Watanganyika kwa umoja na mshikamano hadi tukapata uhuru mwaka 1961.

Badala yake Mohamed Said anataka tumuenzi mlowezi kutoka Afrika Kusini kwamba bila yeye TANU haingeasisiwa na madai ya uhuru yasingefanikiwa...shame, shame, shame kwa Mohamed Said na wote wanaomeza hizi porojo zake.

Hata hivyo nampongezaMohamed Said kwani katengeneza sana hela na hizi porojo zake na kawateka wengi kweli kweli. Sasa naomba aeleze bayana ni kwa nini baada ya vita hawa Wazulu wakaamua kulowea Tanganyika.
Mag...
Raha niipatayo ninaposoma huu uchambuzi ni huu.

Kwa miaka mingi mlikuwa mkisomeshwa historia siyo na mkawa kimya pengine ukimya wenu ni kutokana na kutoijua historia ya kweli.

Nimeandika kitabu nimeisahihisha historia yote.
Baada ya kusoma kitabu changu mnanishambulia.

Ilikuwaje miaka yote mkawa kimya?
Juu ya hayo yote mimi sina tatizo na fikra zenu.
 
Mohamed Said, wewe umesimuliwa na sana sana umesimuliwa na mjomba kibarazani. Sisi wengine mengi ya haya tumeyashuhudia, hatukusimuliwa kama wewe. Sasa nakuambia, mengi ni uongo. Uongo umekupa kula yako, endelea kuwadanganya lakini kaa chonjo usije ukatia mkate wako mchanga, umri unakwenda.
 
Poise,
Maiti hazitaabiki kwa kufanyiwa tabaruku.

Somo la historia ni somo linalovutia sana.

Nimepongezwa na watu wengi sana kwa video hiyo.

Bahati mbaya sana wewe inakutaabisha.
Una matusi ya rejareja na dharau kubwa sana we Mzee Mzushi

Nimekuelewa ulivyocomment hapa kwenye maandishi ya Poise na nimegundua umemtusi vibaya sana Poise labda yeye hajatafakari maneno hayo
 
Mag...
Kwa miaka mingi mlikuwa mkisomeshwa historia siyo na mkawa kimya pengine ukimya wenu ni kutokana na kutoijua historia ya kweli.Nimeandika kitabu nimeisahihisha historia yote.Baada ya kusoma kitabu changu mnanishambulia.
Ilikuwaje miaka yote mkawa kimya?
Come on! Mo '' two wrongs don't make a right''
Kitabu chako ni sehemu tu ya vitabu hakifanyi ulichoandika kuwa sahihi.

Tumekuonyesha matundu, na moja ni hili la Abdul Kumpokea Nyerere Dar es Salaa, bahti mbaya Profesa Shivji na Pro Saida walighafilikiwa na sasa unawatumia kufanya ''justification'' bila kujua walinukuu hoja zako.

Kwahiyo maisha ya vitabu viwili, chako na cha Prof Shivji ni ''symbiotically''

Kwamba, Prof na wenzake walipokea hoja ya Nyerere kutoka kwako, na wewe unawatumia kama Maprofesa kuthibitisha hoja. Tatizo ni umri wa kitabu na utetezi.

Pili, Mag3 kaweka hoja, sasa wewe uliyesoma makabrasha zitetee hoja zako.

Uwepo wa kitabu kingine chochote hauwezi kutetea hoja za kitabu chako.
Kwani kuna tatizo gani ukisimama katika kitabu chako na kukitetea kwa hoja?

Tatu, wapi Abdul Sykes alisimama na kuhutubia mkutano nje ya Tandamti, Kipata na Agrey ?

Jambo la muhimu sana kwa Watanzania si ukombozi wa Wazulu.

Wazulu wanatakiwa WAOMBE radhi kwa kuwa mamluki dhidi ya Wazalendo , halafu waombe radhi Waislam kwa unyama waliowatendea. Hakuna mahali Kleist au Abdul Sykes wameomba radhi

Kwavile wamepewa nishani ya Uhuru, nishani hiyo pia inakuja na kuwajibika.

Ni wito sasa kwa Familia ya Sykes ijitokeze na kuomba Watanzania radhi , kisha Waislam kwa unyama walioutenda.

Familia ya Sykes iombe radhi kwa unyama uliofanywa na wazazi wao kwa Watanganyika na Waislam.
 
Nguruvi...
Kama ninavyokueleza kila siku kuwa mimi sina tatizo na sihangaiki.

Kitabu kipo sokoni sasa mwaka wa 22 na tunakwenda toleo la 4.
Wiki hii umeniona niko hewani kufanya series za historia hii vipindi 10.

Unahitaji ushahidi gani zaidi ya huu kukithibitishia kuwa historia hii imewavutia wasomaji wengi?

Kitabu changu hakijapata kuwa sehemu ya kitabu chochote.
Hiki ni kitabu cha pekee sana.

Sasa tumetoka katika kitabu tumehamia kwenye documentary.
Namshukuru Mungu.

Maktaba yangu ni kati ya maktaba tatu bora zilizohifadhi historia ya Julius Nyerere.
Hili sikusema mimi wamesema walioandika Wasifu wa Julius Nyerere.

Mimi wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes sikuwaza hata kwa mbali kama kitanifikisha hapa.

Hivi unajua publishers wangapi wananitafuta?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom