Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Nguruvi...

Tatizo liko wapi wewe si amini kuwa TANU iliasisiwa na Nyerere 1954?

Mimi sikasirishwi na hilo vipi wewe una hamaki mimi nikisema historia ya TANU inanaanza mwaka wa1929?
Achana na neno "KUASISI"
"Nyerere alikuwa Pugu akisomesha na alipelekwa na Joseph Kasella Bantu nyumbani kwa Abdu Sykes.

Mwalimu alipoacha kazi ndiyo akahamia Dar es Salaan"

Hivi Pugu sio Dar es Salam?

Kwa maelezo ya Mzee Waikela (aliyekuwepo wakati huo) Mwalimu alishakuwepo Dar Es Salaama na alishaanza shughuli za kukutana na wengine na kupanga harakati akiwa bado anafundisha.

Kwa maelezo ya Waikela (aliyekuwepo wakati huo) mwaka 1954 hawakuwa na hiyo habari za kuasisiwa kwa chama chochote, bali walijua ya kwamba TAA ikabadilishwa kuwa TANU.

Mzee Said bado hujaweza kuthibitisha bila shaka kile unachojitahidi kulezea.
 
Nguruvi...
Mimi nina shida gani leo ya kuhangaika maana kama kitabu ndicho hicho kipo miaka 22 sasa matoleo matatu Kiswahili na Kiingereza na tunachapa toleo la nne.

Baada ya miaka 22 unakuja kupingana na mimi kwa kitu ambacho kwanza hukijui na pili hakikuhusu na hapa huwaambieni kila siku kuwa shida inayokupateni ni kuwa historia ya wazee wangu imegusa historia ya TANU vinginevyo hapangekuwa na huu ubishani.

Mimi sina sababu kabisa ya kubishana na wewe.
Nibishane na wewe kwa kitu gani?

Nimekuambia kaangalie utangulizi wa kitabu cha Kivukoni utakusaidia la hilo huliwezi kataa kuwa Seaton na Abdul Sykes walikuwepo.

Hili pia limekushinda.

Nimejaribu kuielekeza akili yako kuwa hiyo ni 1950 nikiamini utaelewa nimekusudia nini.

Tatizo liko wapi wewe si amini kuwa TANU iliasisiwa na Nyerere 1954?

Mimi sikasirishwi na hilo vipi wewe una hamaki mimi nikisema historia ya TANU inanaanza mwaka wa1929?
Mohamed kitabu kinaweza kuwepo miaka 100 hilo halifanyi kiwe sahihi. Leo tunasoma vitabu vya enzi za Wagiriki na kuna mambo yanathibitiswa na mengine yanakanushwa.

Hujibu hoja na hapo ndipo wanajamvi wanakuwa na hofu na unawasaidia kuondoa shaka waliyokuwa nayo.
Mimi sihamaki hata kidogo kusikia TANU ilianzishwa 1929 endapo tu kuna ushahidi wa kutosha na si hadithi za mapokeo

Turudi kwenye mada

1. Iwapi katiba ya AA na TAA ambayo Kleist Sykes au Kijana wake Abdulwahidi Kleist Sykes walitengeneza?
Hapa ni miaka 24 ?(1929-1953) ya tawala za Sykes. Hatuhitaji kabrasha tunataka nusu karatasi tu.

2. Ni kiongozi gani mwingine wa siasa aliyewahi kutangaza uwepo wa katiba kabla ya Mwal Nyerere na TANU?

3. Uko wapi ushahidi wa nyaraka ukionyesha ushiriki wa Abdul kunakili katiba ya Seaton? Kumbuka urafiki tu hautengenezi katiba. Ziko wapi nyaraka za kuthibitisha hilo.
 
Mzee Said kila wakati ninaposoma unapomjibu anayetaka kufahamishwa huwa naishia kujiuliza kama ni mimi tu huwa nashindwa kukuelewa.

Kwa mfano kwenye hoja ya Mkuu Nguruvi amehoji kama uandishi wa katiba ya TANU ni matokeo ya urafiki wa Seaton na Abdul, na je wazo la katiba ni la Abdul na Seaton ni mtekelezaji?...jibu ambalo ningelitegemea hapa ni 'kwa mfano' ndio katiba ya TANU ni matokeo ya urafiki wa Seaton na Abdul au Hapana......... badala yako umeanza tena kuhoji kama amewahi kumsikia Seaton akitajwa kwenye historia za TANU.

Anza kwa kuweka sawa kwanza hoja inayojitokeza kabla ya kuibua hoja yako mpya i naye mwenye hoja awajibike kutoa jibu kwa hoja yako.
May Day,
Ukinifundisha kujibu maswali mtapitwa na mengi.

Mjadala huu una miaka mingi hapa jamvini.

Namuuliza kuhusu Seaton kwa kutaka kujua kama anamkumbuka.

Aliuluza kuhusu katiba ya Kleist Sykes ya mwaka wa 1929 wakati wanaasisi African Association.

Na hili kalikazania sana.

Jibu langu nikamleta Earle Seaton ambae Abdul Sykes alimtia katika TAA Political Subcommittee kuisaidia TAA katika mambo ya sheria.

Hii ni 1950.

Yeye haya hayajui kwani hayapo popote.

Mimi nimeyakuta katika Nyaraka za Sykes.

Yeye anazungumza TANU 1954 na TANU chanzo chake ni TAA na mipango yake ilianza nyuma ya hata hiyo 1950 achilia mbali 1954.

Lakini ninachosema mimi historia hii haina ugomvi na mtu unapenda amini hupendi amini historia ya Kivukoni.
 
Achana na neno "KUASISI"

Kwa maelezo ya Mzee Waikela (aliyekuwepo wakati huo) Mwalimu alishakuwepo Dar Es Salaama na alishaanza shughuli za kukutana a wengine akiwa bado anafundisha.

Kwa maelezo ya Waikela mwaka 1954 hawakuwa na habari za kuasisiwa kwa chama chochote bali TAA alibadilishwa kuwa TANU.

Mzee Said bado hujaweza kuthibitisha bila shaka kile unachojitahidi kulezea.
May Day,
Hakuna neno ndugu yangu kughitilafiana ni silka yetu sisi binadamu.
 
Mohamed kitabu kinaweza kuwepo miaka 100 hilo halifanyi kiwe sahihi. Leo tunasoma vitabu vya enzi za Wagiriki na kuna mambo yanathibitiswa na mengine yanakanushwa.

Hujibu hoja na hapo ndipo wanajamvi wanakuwa na hofu na unawasaidia kuondoa shaka waliyokuwa nayo.
Mimi sihamaki hata kidogo kusikia TANU ilianzishwa 1929 endapo tu kuna ushahidi wa kutosha na si hadithi za mapokeo

Turudi kwenye mada

1. Iwapi katiba ya AA na TAA ambayo Kleist Sykes au Kijana wake Abdulwahidi Kleist Sykes walitengeneza?
Hapa ni miaka 24 ?(1929-1953) ya tawala za Sykes. Hatuhitaji kabrasha tunataka nusu karatasi tu.

2. Ni kiongozi gani mwingine wa siasa aliyewahi kutangaza uwepo wa katiba kabla ya Mwal Nyerere na TANU?

3. Uko wapi ushahidi wa nyaraka ukionyesha ushiriki wa Abdul kunakili katiba ya Seaton? Kumbuka urafiki tu hautengenezi katiba. Ziko wapi nyaraka za kuthibitisha hilo.
Nguruvi,
Unakusudia nirejee kwenye Nyaraka za Sykes nikuonyeshe yaliyomo.

Ndugu yangu yote haya mimi nifanye ili iwe nini?
 
Sawa, naomba unisaidie jibu kuhusu safari ya Mwalimu kwenda Lindi, kama safari ya 1955 ilifuatiwa na safari nyingine yoyote kabla ya 1961?.
 
Yote haya nimeeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mwalimu alirudi tena Lindi mwaka wa 1956.

Safari hii Mwalimu alipokelewa kwa zafa watoto wa chuo cha Sheikh Yusuf Badi wakiongoza msafara wake.

Ili kuitia TANU nguvu Yusuph Chembera na Salum Mpunga walimtia mwalimu wao katika chama.

Sheikh Yusuf Badi alikuwa Sheikh mkubwa sana na kuingia kwake TANU kulibadili haiba ya chama.

Kuna mtaa Lindi umepewa jina la Sheikh Badi kwa kuthamini mchango wake katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
SHEIKH YUSUF BADI WA LINDI

Inaaminika kuwa hakuna picha ya Sheikh Yusuf Badi popote kwani alikuwa hapendi kupigwa picha.

Juhudi zangu za kupata picha yake hazijafanikiwa hadi hivi sasa.

Rafiki yangu ameweka kibao cha mtaa wenye jina ‘’Sheikh Badi.’’

Mtaa huu uko Lindi.

Nimelisikia jina la Sheikh Yusuf Badi Lindi mjini miaka mingi iliyopita wakati nafanya utafiti wa kitabu cha historia ya TANU kupitia maisha ya Abdulwahid Sykes.

Siku ya kwanza nilianza mahojiano yangu na Salum Mpunga tukiwa tumekaa kwenye kibaraza za msikiti mkubwa wa Lindi mjini ulioko karibu na kituo cha mabasi.

Baada ya mazungumzo yangu na Salum Mpunga siku ya pili asubuhi nikawa na mazungumzo na Yusuf Chembera nyumbani kwake kwenye varanda yake ndogo lakini nadhifu.

Hawa watu wawili Salum Mpunga na Yusuf Chembera ndiyo waasisi wa TANU Southern Province mwaka wa 1955.

Kisa cha wazalendo hawa na jinsi walivyoweza kumleta Mwalimu Nyerere Southern Province ni kisa cha kusisimua sana.

Sasa niko na Yusuf Chembera nyumbani kwake mwezi wa Ramadhani.

Yusuf Chembera anasema Kiswahili kizuri na alikuwa mtu fasaha sana akijua kupanga maneno yake.

Alianza kunieleza historia ya TANU kwa kunitajia maisha yake ya udogoni na hapo ndipo kwa mara ya kwanza nikalisikia jina la Sheikh Yusuf Badi.

‘’Nilipofika umri wa kusoma baba yangu akanipeleka chuoni kwa Sheikh Yusuf Badi kusoma.

Chuo cha Sheikh Badi ndicho kilikuwa chuo kikubwa na yeye mwenyewe alikuwa sheikh akiheshimika kusini nzima.’’

Yusuf Chembera akanieleza yote waliyokutananayo katika kuasisi TANU wakisaidiana na mzee wao Suleiman Masudi Mnonji ambae nyumba yake ndiyo ilikuwa ofisi ya TANU ya kwanza Lindi.

Southern Province kulikuwa na vitisho vingi dhidi ya TANU watu wakitishwa kwa kuambiwa kuwa TANU ni chama cha Waislam ambao wanataka kuleta vita vingine vya Maji Maji.

Uongozi wa TANU Lindi ukaamua kumtuma Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjale Dar es Salaam kumwalika Nyerere aje Lindi ili asafishe hii propaganda na wananchi waiunge mkono TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nyerere akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani walifika Lindi, Mikindani, Masasi na Nachingwea na baada ya ziara hii TANU haikuwa tena na kizuizi ila watu walijiunga na chama kwa wingi.

Hii ilikuwa mwaka wa 1955 na Nyerere alikuwa amekwenda na kurudi UNO safari ya kwanza.

Mwaka wa 1956 Nyerere alirejea tena Lindi na safari hii mapokezi yake yalikuwa makubwa na ya kupendeza.

Katika ile safari ya kwanza serikali ilikataza maandamano ya kumpokea Nyerere mjini.

Ilibidi Nyerere na ujumbe wake upokelewe kijiji cha Mbanji nje ya mji na wanachama wa TANU waingie mjini kimya kimya na wageni wao kama vile wanasindikiza msiba.

Mara baada ya safari ya kwanza ya Nyerere Lindi ili kukipa chama nguvu mwanafunzi wa Sheikh Yusuf Badi, Yusuf Chembera alimfuata mwalimu na sheikh wake Sheikh Badi kumuomba ajiunge na TANU ili chama kipate nguvu.

Sheikh Yusuf Badi alipojiunga na TANU alikuja na jeshi kubwa la na murid wake wa Tariqa Qadiriyya.

Sheikh Yusuf Badi aliipa TANU mjini Lindi na pembezoni heshima kubwa.

Mwaka wa 1956 Nyerere alipokuja Lindi hali ya TANU ilikuwa imebadilika chama kikiwa na nguvu kubwa isiyo na kifani.

Katika mapokezi ya Nyerere Sheikh Yusuf Badi alitoka na chuo chake na wanafunzi wake kwa maandamano wanafunzi wakipiga dufu huku wakisoma kasida sauti za matari zikisikika kote.

Hii ilikuwa siku ya shamrashamra kubwa mjini Lindi.

Usiku wake Mtaa wa Makonde nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji Sheikh Yusuf Badi alifanya dua kubwa iliyohudhuria na Waislam aliowachagua yeye sheikh mwenyewe maalum kwa hafla hiyo.

Dua hii ilihudhuriwa pia na masheikh wengine maarufu pale Lindi na kutoka vijiji jirani.

Katika dua hii alikuwapo Bi. Sharifa bint Mzee mmoja wa akina mama waliofanya kazi kubwa kuwavuta wanawake kujiunga na TANU.

Mussa Athumani Lukundu, kiongozi wa Dockworkers Union Lindi aliandaa karamu kubwa kwa heshima ya Nyerere.

Siku ya ukumbusho mkubwa sana mjini Lindi ilikuwa siku ya uhuru, tarehe 9 Desemba, 1961.

Sheikh Badi, ambae alikuwa bingwa wa kutunga mashairi, aliombwa na TANU kuandika hotuba ya uhuru.

Hotuba hii ilisomwa na mwanafunzi wake Yusuf Chembera mbele ya DC akiwa kama mwakilishi wa utawala wa Kiiereza uliokuwa uking’oka.

Hotuba hiyo ya Sheikh Badi iliandikwa kwa Kiarabu na Chembera alinionyesha nikaishika kwa mikono yangu.

Sheikh Badi hakuona kama ipo hotuba yoyote iliyoandikwa na mwanadamu iliyostahiki hafla kama ile ya siku ya kujikomboa kutoka minyororo ya ukoloni.

Sheikh Badi alimsomea mwanafunzi wake Chembera, dua ya kunut ambayo husomwa na Waislam katika kila sala ya alfajir.

Usiku wa manane wa tarehe 9 Desemba, 1961 ulikuwa usiku adhim sana kwa wote wawili, mwalimu na mwanafunzi wake, pale watu walipokusanyika katika Uwanja wa Gofu kumsikiliza Chembera akisoma kunut kupokea uhuru wa Tanganyika.

Maspika yalisikika yakitoa sauti ya Yusuf Chembera akisoma Dua ya Kunut na wananchi wakiitika Amin, Amin, Amin.

Hakuna popote jambo kama hili lilitokea katika kupokea uhuru wa Tanganyika.

Hakika kwa watu wa Lindi hawakukosea kumpa mtaa Sheikh Yusuf Badi.

Sheikh Badi anastahili kukumbukwa na anastahili heshima hii.

Picha ya kwanza Mtaa wa Sheikh Badi, Bi. Sharifa bint Mzee katika utu uzima na wajukuu zake, Yusuf Chembera na Salum Mpunga.
 
Kumbukumbu ya Sheikh Badi Lindi.
Screenshot_20200806-210337.jpg
 
Nguruvi,
Unakusudia nirejee kwenye Nyaraka za Sykes nikuonyeshe yaliyomo.

Ndugu yangu yote haya mimi nifanye ili iwe nini?
Hatuhitaji nyaraka za vikao au mialiko n.k

Tuletee nyaraka moja tu, Katiba. Iwe ya AA ya Kleist au TAA ya Abdul
Kama kuna kipande cha karatasi iwe robo au nusu tuwekee hapa

2. Tuonyeshe kiongozi mwingine wa siasa zaidi ya Mwl Nyerere aliyewahi kutangaza katiba achilia mbali kuwa nayo

3. Tuonyeshe ushiri wa Abdul kuandika katiba ya Seaton! kwa maana kama Abdul alikuwa na 'mkono' ukiachilia urafiki wake na Seaton katika chai na makaimati.

Hatuhitaji kitu kingine chochote kile, ni hayo matatu tu hapo juu
 
Ndiyo nakuuliza baada ya miaka 30 kutoka nilikokuwa naandika maisha ya Abdul Sykes na kitabu kuwako sokoni kwa miaka 22 na baada ya kitabu kuchapwa mara nne unanitaka nirejee kwenye Nyaraka za Sykes nikakutafutie nyaraka moja.

Kinachonishangaza mimi ni kuwa nihangaike kwa hayo yote mimi kwa kutaka nini?
 
Fictitious Sykes papers plus author's own imaginations fuelled by some evil intentions.
Nanren,
Prof. Haroub Othman hakuamini yaliyokuwa yanamfungukia katika kitabu cha Abdul Sykes.

Alitafuta taarifa zaidi kutoka kwa Ahmed Rashad Ali.

Bahati mbaya sana kwake kenda kuukata mti kule ulikolalia.

Picha kulia ni Sheikh Ahmed Islam, Ahmed Rashad Ali na Prof. Haroub Othman.

(Ed) Modern Tanzanians (1973) paper unazosema ni ''fictions,''
zipo Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana, Kleist Sykes yuko katika Iliffe (Ed) ''Modern Tanzanians, '' Kleist Sykes The Townsman,'' (1973) yuko katika Dictionary of African Biography (DAB) Vol. 6 (2011).

ATTACH=full]1529284[/ATTACH]
 
Attachments

  • PROF. HAROUB OTHMAN, AHMED RASHAD NA SHEIKH AHMED ISLAM.jpg
    PROF. HAROUB OTHMAN, AHMED RASHAD NA SHEIKH AHMED ISLAM.jpg
    18.7 KB · Views: 2
Wewe Mzee hujui kuandika kwa kuanza na introduction?
"WE MZEE!" LUGHA YA DHARAU, KEJELI NA VITISHO

Baada ya uhuru zilipoanza kauli ya kukashifu TAA na yeye mwenyewe Abdul kuwa hakuwa anaongoza chama cha siasa bali chama cha starehe mmoja wa marafiki zake aliyekuwa anaumizwa na maneno yale alikuwa Ahmed Rashad Ali.

(In Shaa Allah nitaweka historia ya Ahmed Rashad hapa kwa faida yetu sote).

Ahmed Rashad akawa anamuomba Abdul aeleze historia ya TANU kuanzia jinsi baba yake alivyoanza harakati kupitia African Association mwaka wa 1929.

Abdul Sykes alikataa akimwambia kuwa kama tatizo ni nani kaunda TANU yeye hilo halimshughulishi na hakika Abdul hakufungua kinywa chake hadi anaingia kaburini.

(In Shaa Allah nitakuwekeeni hapa yale aliyoandika Daisy kuhusu vipi baba yake alikabiliana na fitna hii katika kipindi hiki).

Nilipokuwa nasafiri kuwatafuta hawa wazalendo ilikuwa tukimaliza mazungumzo nataka kunyanyuka kuondoka wananambia nisubiri tupige fatha, yaani tufanye dua.

Wakisema kuwa hili jambo nililokuwa nalifanya ni kubwa sana linahitaji msaada wa Allah.

Baadhi ya wazee hawa wengi walifariki kabla kitabu hakijatoka na wengine nilibahatika kuwapa nakala ya kitabu kwa mkono wangu ingawa kilikuwa kwa Kiingereza na wasingeweza kukisoma.

Moyoni walikuwa wanasononeka kuwa mchango wao katika kupigania uhuru haukuzaa matunda waliyotegemea.

Leo nafarajika ninaposoma jina la Abdul Sykes lililofutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika lilivyorejea na sasa limekuwa maarufu watu wakibishana kuhusu yeye.

Kleist Sykes mtoto wa Abdul Sykes alikuja ofisini kwangu Tanga kunishukuru baada ya baba yake na baba yake mdogo Ally Sykes, kutunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kleist alinipa mkono huku akibubujikwa na machozi.

Leo ninaposona lugha za "We mzee," lugha za dharau na kejeli na wakati mwingine vitisho dhidi yangu sikasiriki.

Wale wazee waasisi wa TANU walinambia hii kazi niliyoamua kufanya ni nzito.

Daisy anaeleza chokochoko zilizivyoanza karibu ya kupata uhuru na zikaendelea baada ya uhuru:

‘’...uhuru ulipokuwa dhahiri sasa unapatikana na ulipopatikana ulikuja na changamoto nyingi ambazo naamini baba hakuzitegemea.

Haitakuwa sawasawa ikiwa sitaeleza upeo wa juu wa baba yangu katika wema, huruma na unyofu aliokuwanao.

Hata nilipokuwa mtoto nilipata kushuhudia na kuona chokochoko na chuki dhidi yake bila shaka kwa ajili ya hasad kwani baba kwa kiwango chochote kile alikuwa mtu aliyefanikiwa na kwenye ngazi nyingi wengi hawakuthubutu hata kuota kukanyaga, lakini sikumuona baba kukasirika wala kutaka kulipiza kisasi.

Katika unyofu wa hali ya juu aliendelea na maisha yake...’’

Katika kipindi hiki Abdul Sykes alikuwa anatembelea Mercedes Benz 220 SE.

Kijana mwingine Dar es Salaam aliyekuwa na gari kama hii alikuwa kijana wa Kiarabu Abbas Abdulwahab.

Huenda maisha kama haya ndiyo yaliyosababisha hasad na wivu dhidi yake na Abdul alikuwa hata hajafikisha miaka 35.

Kuna msemo wa Kiarabu unaosema kuwa, ''Sababu huondoa ajabu.''

Jibu tunalo kwa nini magazeti TANU ya chama alichoasisi na kukifadhili kwa miaka mingi hayakuweza kumpa Abdul Sykes ile heshima ndogo aliyostahili katika umauti wake.

Kuchapa taazia yake ndani ya magazeti ya Uhuru na The Nationaist na kueleza yale aliyoyafanya kwa Nyerere na TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni kumnyanyua juu katika sifa na heshima isiyo kifani.

Maadui wa Abdul Sykes walitaka jina lake lipotee kabisa katika ramani ya historia ya Tanzania.

Lakini Brendon Grimshaw alipochapa taazia ya Abdu Sykes katika Sunday News (20 October, 1968) kichwa cha taazia ile ilikuwa katika wino mweusi uliokoza: ''ABDUL SYKES WAS A TANU PIONEER.''

Hiyo picha ni siku watoto wa Abdul Sykes waliponiita nikaione Medali aliyotunukiwa baba yao (posthumous) katika kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Aliyevaa nguo nyekundu ni Daisy na kushoto wa kwanza ni Kleist.
 
Nguruvi,
Ndiyo nakuuliza baada ya miaka 30 kutoka nilikokuwa naandika maisha ya Abdul Sykes na kitabu kuwako sokoni kwa miaka 22 na baada ya kitabu kuchapwa mara nne unanitaka nirejee kwenye Nyaraka za Sykes nikakutafutie nyaraka moja.

Kinachonishangaza mimi ni kuwa nihangaike kwa hayo yote mimi kwa kutaka nini?
Kwanini unahangaika kutuletea hata tusiyo uliza? Kwanini unahangaika kurudia hadithi na pich zile zile kila siku ? Halafu unashindwa kutupa nyaraka moja tu, KATIBA

Mohamed kama hakuna katiba ya AA au TAA sasa ni wakati useme wazi.

Wanajamvi, hapa tumefika katika hatua nyingine

Hatua ya kwanza: Tume prove beyond doubt kuwa Abdul Sykes hakumpokea Nyerere Dar es Salaam
Kwa maneno mengine Mohamed amelisha umma UONGO!

Lakini pia maefanikiwa hata kuwachuuza maprofesa Shivji na Saida. Haiwezekani aandike maandishi miaka 20 halafu adai uthibitisho upo katika kitabu cha maprofesa hao cha mwaka 1. Ni UONGO.

Hatua ya Pili: ni wazi kuwa Kleist Sykes na Abdul K Sykes Waliendesha siasa za makundi na si za chama.
Ushahidi ni kuwa kwa miaka 24 kuanzia 1929 hadi 1953 wakati wa tawala zao hakukuwepo na muongozo unaoitwa KATIBA. Kwa maneno mengine kila kitu kilifanyika kwa utashi tu. Mohamed ameshindwa kuthibitisha hili na madai kwamba Seaton na Abdul waliandika katiba ni UONGO.

Hatua ya Tatu
Mohamed ameshindwa kutaja kiongozi mwingine aliyetengeneza katiba ukimwacha Nyerere. Iwe katiba ya kukopi au ya kuandika ni Mwalimu Nyerere ndiye aliyebadili siasa za Familia ya Sykes kuwa siasa za Nchi.
Madai kwamba Nyerere hakuandika katiba ni UONGO, hajaeleza nani mwingine kwa ushahidi

Hatua ya nne
Kwamba TANU ilianzishwa na Abdul kuna utata. Ikiwa ni hivyo kadi ya Abdul ni 3 na Nyerere ni 1
Hata kama jina lilikuwepo, mtu aliyeliweka hadharani ni Mwana wa Kambarage si awaye kutoka familia ya Sykes

Hatua ya Tano
Ni nyerere aliyesambaza chama nchini. Ushahidi ni Sheikh Bad na akina Chembera waliokuja kumwalika Nyerere kwa mujibu wa Mohamed. Hakuna mahali nje ya Tandamti na kidongo chekundu ambapo Abdul Sykes aliwahi kuhutubia,. Mohamed ameshindwa kuthibitisha na hivyo madai kuwa Uhuru umepiganiwa na Familia ya Sykes yana utata lakini zaidi kuna haufu ya UONGO

Tutaendelea kubumburua marejeo ya kauli za Uongo kwani uongo ukirudiwa sana hugeuka kuwa ukweli.
 
Kwanini unahangaika kutuletea hata tusiyo uliza? Kwanini unahangaika kurudia hadithi na pich zile zile kila siku ? Halafu unashindwa kutupa nyaraka moja tu, KATIBA

Mohamed kama hakuna katiba ya AA au TAA sasa ni wakati useme wazi.

Wanajamvi, hapa tumefika katika hatua nyingine

Hatua ya kwanza: Tume prove beyond doubt kuwa Abdul Sykes hakumpokea Nyerere Dar es Salaam
Kwa maneno mengine Mohamed amelisha umma UONGO!

Lakini pia maefanikiwa hata kuwachuuza maprofesa Shivji na Saida. Haiwezekani aandike maandishi miaka 20 halafu adai uthibitisho upo katika kitabu cha maprofesa hao cha mwaka 1. Ni UONGO.

Hatua ya Pili: ni wazi kuwa Kleist Sykes na Abdul K Sykes Waliendesha siasa za makundi na si za chama.
Ushahidi ni kuwa kwa miaka 24 kuanzia 1929 hadi 1953 wakati wa tawala zao hakukuwepo na muongozo unaoitwa KATIBA. Kwa maneno mengine kila kitu kilifanyika kwa utashi tu. Mohamed ameshindwa kuthibitisha hili na madai kwamba Seaton na Abdul ni UONGO

Hatua ya Tatu
Mohamed ameshindwa kutaja kiongozi mwingine aliyetengeneza katiba ukimwacha Nyerere. Iwe katiba ya kukopi au ya kuandika ni Mwalimu Nyerere ndiye aliyebadili siasa za Familia ya Sykes kuwa siasa za Nchi.
Madai kwamba Nyerere hakuandika katiba ya Mohamed ni UONGO, hajaeleza nani mwingine kwa ushahidi

Hatua ya nne
Kwamba TANU ilianzishwa na Abdul kuna utata. Ikiwa ni hivyo kadi ya Abdul ni 3 na Nyerere ni 1
Hata kama jina lilikuwepo, mtu aliyeliweka hadharani ni Mwana wa Kambarage si awaye kutoka familia ya Sykes

Hatua ya Tano
Ni nyerere aliyesambaza chama nchini. Ushahidi ni Sheikh Bad na akina Chembera waliokuja kumwalika Nyerere kwa mujibu wa Mohamed. Hakuna mahali nje ya Tandamti na kidongo chekundu ambapo Abdul Sykes aliwahi kuhutubia,. Mohamed ameshindwa kuthibitisha na hivyo madai kuwa Uhuru umepiganiwa na Familia ya Sykes yana utata lakini zaidi kuna haufu ya UONGO

Tutaendelea kubumburua marejeo ya kauli za Uongo kwani uongo ukirudiwa sana hugeuka kuwa ukweli.
Nguruvi,
Ndugu yangu mimi sina tatizo na unavyoichukulia historia ya TANU hayo pia ni mchango katika kuelewa historia hii.

Kama vile mimi nilivyoona upungufu mkubwa katika historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni na wewe una haki ya kutoa fikra zako kwa historia hii niliyoandika.

Zote hizi ni historia za TANU na wasomaji watazisoma na wataamua wenyewe.

Hii ndiyo faida ya kuandika.

Nimeandika kitabu mmekisoma na mmeamua kutoa fikra zenu.

Laiti nisingeliandika msingewajua hawa wote ambao walifutwa katika historia - Abdul Sykes mwenyewe na Ally Sykes mdogo wake, Hamza Kibwana Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Schneider Abdillah Plantan, Bi. Tatu bint Mzee kuwataja wachache.

Uhuru ulipopatika wakaja watu kuwafitini Yusuf Chembera, Salum Mpunga, Ali Mnjale na Sheikh Yusuf Badi kuwa hawana elimu na "wanachanganya dini na siasa," na walioiandika historia ya TANU na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika, wakawafuta katika historia hii.

Mohamed Said ndiyo aliyewatafuta na kuwarejeshea heshima yao.

Hayo mengine nimeyaacha hayana maana sana kwangu kuyasemea.
 
Of course hayawezi kuwa na maana kwako kwasababu hayalingani na lengo lako.
Haya ninayoandika yanamaana sana kwa wasomaji.

Nina uhakika Prof Shivji na Prof Saida, watakaa kitako kufikiri ikiwa kauli waliyosoma kwako kwamba Abdul alimpokea Nyerere ni upotofu . Sidhani kama wanaweza kusimama mahali na kuitetea!
Wewe unaweza kwasababu huna aibu, sijui kama wao wanaweza

Kwa Wanajamvi, hasa vijana haya yana maana sana kwao.
Kwanza , wanajifunza kusoma kwa kufikiri na kuunganisha mtiririko wa habari
Pili, inawakinga kumeza uongo bila makosa , kwamba, umri wao unatumika tu kuwa 'exploit'

Tatu, inasaidia pia 'wafuasi' wako wasome maandishi kwa uangalifu, kinyume chake wanaweza kuangukia pua
Sasa kama umeshindwa kuthibitisha uwepo wa katiba ya AA na TAA ya Abdul, wao wanaweza nini?

Muhimu zaidi ni kueleza jinsi Abdul Sykes alivyokuwa overrated na vitabu vyako katika jitihada za kumdunisha Nyerere. Kwa vigezo vyote Nyerere atabaki kuwa Nyerere na sifa zake na Abdul atabaki kuwa na sifa zake.

Huwezi kumfanya Abdul awe zaidi kwa kumnyanyasa au kumdhalilisha Nyerere

Nyerere anatetewa na historia, ambayo haiandikwi , kubumbwa au kufinyangwa.
Ni historia inayojidhihiri kwa muda na matokeo.
Ndiyo maana miaka 20 tangu afariki bado '' historia inamtetea'' akiwa amelala kaburini tuli

Kwamba alilishwa mayai kwa Sykes, na alivaa Kaptula au alipewa pesa za kununua ng'onda, au alikwenda sokoni na kikapu bila pesa, hayo hayaondoi ukweli mwingine wowote katika kuongoza harakati za uhuru

Ni Nyerere aliyebadilisha siasa za barazani na kuzipeleka majimboni , Tanganyika na UN. Siyo Abdul Sykes

Tena tukichimba zaidi, kubwa la Abdul ni kuongoza genge la wahuni kwenda kutandika wazee wake ili achukue utawala wa baba yake.

Hakuandika Katiba wala baba yake hakuandika. Hawakupeleka siasa mikoani zaidi ya Tandamti na Agrey.

Historia si hisia, tenzi au simulizi. Si mahoka au ngano, ni mtiririko wa matukio usiohitaji nakshi au uvumba.

Nawahi Magila, leo tunamuoza mtoto wa baba shangazi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom