Nini kilikwamisha Meli kubwa kutia nanga bandari Mtwara?

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
1,067
2,222
Meli kubwa iliyobeba magari ya Dangote imetia nanga bandari ya Mtwara,kiasi kwamba imeshangaza Dunia kuona kwamba,kumbe mbali ya bandari ya Dar, Tanzania tuna bandari nyingine yenye uwezo wa kuingiza meli kubwa zaidi.

Nini kimefanya bandari hii kutotumiwa na meli kubwa kwa miaka yote hii?
 
Meli kubwa iliyobeba magari ya Dangote imetia nanga bandari ya mtwara,kiasi kwamba imeshangaza Dunia kuona kwamba,kumbe mbali ya bandari ya Dar, Tanzania tuna bandari nyingine yenye uwezo wa kuingiza meli kubwa zaidi.

Nini kimefanya bandari hii kutotumiwa na meli kubwa kwa miaka yote hii?
Hata mie nimeshangazwa sana, kwanini meli zisongamane Dar wakati tuna Bandari bora kabisa, kama hili dude lenye urefu wa mita zaidi ya 200 limeweza kutia nanga tena watumishi wake wana ari sana wanashusha malori usiku kucha.
 
Kama ulisoma shule ya msingi miaka ya 90 usingeuliza swali hili. Tulijifunza kuwa BANDARI YENYE KINA KIREFU ZAIDI AFRIKA MASHARIKI NI YA MTWARA. Hili swali nilikuwa silikosi kwenye mtihani. Kabla hawajaleta vimasomo vyenu hivi sijui maarifa ya jamiii, sijui stadi za kazi...

Waliamua tu kutoleta meli kubwa.
 
Ni siasa na ulafi tu wa wapiga dili kila kitu walitaka kifanyike Dar es salaam kwa sababu wao wako Dar es salaam hakuna kingine bandari ya Mtwara ina kina kirefu cha asili.
ni kweli mkuu, warasimu wa dar es salaam walihakikisha dili zote zinabaki bandari ya dar es salaam. kuna kipindi kulikuwa na mpango wa bandari ya mtwara ndio ipokee magari yote ya nchini. warasimu wakazuia
 
Meli kubwa iliyobeba magari ya Dangote imetia nanga bandari ya mtwara,kiasi kwamba imeshangaza Dunia kuona kwamba,kumbe mbali ya bandari ya Dar, Tanzania tuna bandari nyingine yenye uwezo wa kuingiza meli kubwa zaidi.

Nini kimefanya bandari hii kutotumiwa na meli kubwa kwa miaka yote hii?
Zinakujaje bila sababu???, hata hii ilokushangaza yaani km cyo Dangote via Magufuli wetu hadi ungerudi kwa Sir God usingelilijua hill la ukubwa was Bandari ya Mtw. NAHISI YAPO MENGI TUTASHANGAA UNDER MAGUFULI LEADERSHIP. SAMAHANI KM NIMEKUKWAZA.
 
Meli kubwa iliyobeba magari ya Dangote imetia nanga bandari ya mtwara,kiasi kwamba imeshangaza Dunia kuona kwamba,kumbe mbali ya bandari ya Dar, Tanzania tuna bandari nyingine yenye uwezo wa kuingiza meli kubwa zaidi.

Nini kimefanya bandari hii kutotumiwa na meli kubwa kwa miaka yote hii?

Sasa utaziona nyingi Mtwara, hiyo bandari iliboreshwa na Kikwete.

Na kwa jitihada za Kikwete alizozifanya bila kuchoka kutuletea watafuta gesi na mafuta tutashuhudia mengi mapya kwa Mtwara na Tanzania nzima kwa ujumla.

Kikwete tutakukumbuka daima.
 
Sidhani kama ni kweli.Kina kirefu ni asili yake si sayansi ya mwanadamu.Tatizo kila kitu tunataka kifanyike Dar siku tukitambua kila Mkoa au Wilaya kuna fursa kede kede tutapiga hatua kubwa kuliko hali ilivyo sasa.
 
Kina pekee si kinachofanya meli kubwa kufunga gati. Kumbuka hilo.
 
Tatizo ilikuwa ni uamuzi wa mamlaka husika hakuna jingine.
Nakubaliana na wewe. Inafahamika bandari ya Mtwara ina kina kirefu, lakini TPA badala ya kutumia faida hiyo ikang'ang'ania meli zirundikane bandari ya Dar. Kwa vyovyote beneficiaries walikua ni TPA wenyewe.
Kwa hili nampongeza Mh JPM na Mh MKM-PM!
Figisu zilikua ni nyingi, haishangazi hata korosho bei ya kutupwa ilikua ni kwa makusudi. Kwa hili nawapa Big Up JPM na Waziri Mkuu.
Endeleeni kuinyoosha nchi hii.
 
Kwan anayeamua mzigo ushukie wapi c ni mwenye mzigo mwenyewe!!?
Siyo kweli, ni mazingira tu yaliwekwa na wapiga dili ili kuleta ugumu. Haiwezekani mzigo ukae week2 wakati bandari nyingine ungeweza kutoa mzigo baada ya masaa24, ukipima uwiano pqmoja na umbali wa Dar hadi Mtwara,bado ni afadhali ugharamie umbali lakini muda ukiwa mfupi.
Ni ukiritimba wa makusudi ili wapiga dili wafanye yao. Leo meli hii imewaumbua.
 
Kama ulisoma shule ya msingi miaka ya 90 usingeuliza swali hili. Tulijifunza kuwa BANDARI YENYE KINA KIREFU ZAIDI AFRIKA MASHARIKI NI YA MTWARA. Hili swali nilikuwa silikosi kwenye mtihani. Kabla hawajaleta vimasomo vyenu hivi sijui maarifa ya jamiii, sijui stadi za kazi...

Waliamua tu kutoleta meli kubwa.
Tatizo ni ukiritimba wakutaka kila kitu kiwe dar, Wakubwa makampuni yao yako dar na wanaishi dar. NI kweli mtwara ina kina kirefu kwa asili sawa sawa na lake Tanganyika.
 
Back
Top Bottom