Nini kilikusaidia kupata kazi?

Katika maisha yangu hadi sasa nilichojifunza ni kuwekeza kwa watu, kujenga urafiki na kufahamiana na watu wengi kadri unavyoweza.

Katika hili nikiri kuwa mm ndilo limenisaidia sana tena sana.

Mimi nimefanikiwa katika scenarios zifuatazo;

1. Kuna rafiki yangu anafahamiana na watu wengi sanaaa, alinishtua siku moja kuna kazi imetangazwa Bank moja lkn ni Tangazo la ndani, akampigia simu mama mmoja akamwambia nina rafiki yangu amemaliza chuo (akakitaja) anaweza kufanya ile interview?
Maza akamwambia aje kesho mchana kuna interview.

Nikaenda mzee nikapewa PC hapo imetegeshwa timer, nikaelekezwa cha kufanya, pale lilikuwa swali linakuja unalijibu ukichelewa kujibu linapotea, ukiwahi kujibu una-opt nxt question hivyohivyo linafuata lingine.... so nikavuka pale... ikaja oral kesho yake nikatusua after 2 weeks nikaanza kazi.

Ikapita kama 2 years akaja rafik wa yule jamaa aliyeniungia job Bank, akaomba mkopo nikamuhudumia vzr akapata mkopo katika kipindi kifupi, akawa mshkaji wangu. Siku moja tukiwa tunapiga story akaniuliza wewe hutaki kazi serialini, nikamuuliza kwa nafasi ipi akanieleza....akaniuliza qualification nikamwambia..... basi ikapita kama miezi miwili hapo tayar nilikuwa nimefungua stationery akaja stationery akaniamba nimtengenezee (customization) tangazo la.nafasi ya kazi ili alipeleke gazetini...nikafanya hvyo baadae akaniambia kama unaweza omba hy nafasi moja wapo lkn tu kama upo interested na kazi serikalini.

Nikaomba baada ya miezi mingi kupita nikaitwa interview, nakumbuka tulikuwa watu kama 90 na walikuwa wanataka nafasi moja kwa position yangu. Nikapiga fresh interview baada ya muda wakaita nika report, basi nika resign Bank nikaanza kazi pale....

Wakati fulani nikawa nataka kuhama ofc hiyo nihamie nyingine, kule nilikoomba nihamie wakampigia simu yy kwa sbb ndo alikuwa HR jamaa akani-recommend vzr na hatimaye nikahamia sehemu nyingine nzr zaidi na sensitive sana!!!

2. Kupitia network ambayo ninayo nimeweza kusaidia pia ndg zangu... nakumbuka kuna mdogo wangu alipata kazi mkoa fulani kwa sbb tu niliweza kuongea na washikaji na washikaji wakawa na access ya kufanikisha ajira ile ya dogo.

Kifupi mimi naamini hata matajiri ili wafanikiwe wanahitaji kwa mtaji wa watu, then mtaji wa pesa unafuata... and this is a practical katika maisha kwa ujumla wake.
Aloo!!!! Nimevutia sanaaaaaa na maandishi yako asee
 
Nilitaka niandike Uzi kuhusu Maswala ya Ajira etc..

Mie ni kijana bdo.

Wakat nasoma nilitamani kuajiriwa nikiwa BADO nikiwa nasoma Chuo.
Nilikosa kazi.. kwa miaka miwili mwaka wa pili ilikuw ni semester ya mwisho lazima Tufanye FIELD.

Nikaitumia hiyo FURSA.. kujijengea JINA, CONNECTION na UAMINIFU. ktk Taasisi nyeti niliyoenda kufanya Field.

Sikufichi.. wenzangu niliosoma nao Asilimia 70% walienda kufanya Field ilimradi wakamilishe Field report yao basi.. ila hawakuwaza mbele..

Mie nilitarget sehem ambay itaniwezesha kubaki kuendelea kufanya kazi.. na nikajituma kias kwamba siku nakamilisha Field yangu.. OFISI/IDARA nzima inasikitika.. wanatamani nibaki.

Inshort.

Fursa namba moja ukitaka uajiriwe.. ITUMIE FIELD vzr... Piga KAZI kweli kweli.

Pili.. Usiwe MTu wa kuwaza HELA.. yaan unataka ULIPWE ukishagundulika hivy wakat wa Field.. imekula kwako.

Tatu.. SOFT SKILLS.. ukiachia hizo skills kitu kingine cha muhimu UJUZI ulio nje ya kile unavhofanyia field.

Mfano. mimi wakat nafany Field kina baadhi ya wafanyakazi walidhani mimi ni IT wa IDARA.. kumbe siyo Profession yangu... Bali nilitumia vzr skills zangu za IT na kutatua changamoto mbalimbali.. kitu ambacho kilinipa Credit sana..

Kuwa mtulivu.. smart.. na mnyenyekevu.

After kumaliza Field KWA Kuwa MABOSS nishawafanya marafiki na wameona Utendaji kazi wangu.. after one week nikavutiwa WAYA... nikaripot SOMEWHERE.. ndipo nipo kwa SASA natumikia TAIFA.

Tatizo utamwambia nini mtu anauakika wa kula na kulala,eti umwambie fanya kazi bila kulipwa upate ujuzi,ukiwaambia hivyo wata kutukana na kukudharau ila akishajionea kitaa ndio wanapata akili,akili zao zina watumaga ukiwa chuo,ukimaliza tayari unakazi.

Wengi wao kipindi cha field wanawaza kulipwa hela waje kulingishia kwamba wanalipwa hata akifanya kitu ambacho sio fani anayoisomea, yeye anataka awe analipwa tu.

Mwisho wake akimaliza chuo ndio wanaanza kulala mika life tyt.

Wengi wangekuwa wanajitolea vizuri kwenye kipindi cha field au Baada ya kumaliza chuo wangekuwa wanapata kazi mapema sana tu,ila sasa ndio hivyo wanasubiria connection mwaka wa 4 sasa. Nenda kajitolee miezi kadhaa utakuwa umejua vitu vizuri,hawawezi kumwita mtu kwenye interview mwenye cv asiyeweza kufanya kazi au responsibilities za kazi hazipo kwenye cv yake yaani hawezi kufanya hiyo kazi.

Hata ungekuwa wewe huyo mtu ofisini anakuja kufanya nini,cv na job responsibilities hazifanani.halafu hapo hapo anataka mshahara mkubwa ili aweanawaambiA na wenzake nalipwa hela nyingi.

Wanaojitambua walishashtukia mchezo mapema wanaenda kujitolea ili kupata ujuzi wa kazi interview moja mbili kazi tayari.wako kimya wanakula maisha ,walikubali kusota kwa muda.

Mtu unajua kazi yako yaani uko vizuri kwenye kazi wanakuachaje? Wamchukue ambae hawezi kufanya kazi kabisa yaani kila sehemu wewe unaweza kazi vizuri wakuache kila ofisi wawewanachukua wasio jua kazi wakuache wewe miaka 4 sasa?.
 
Pakujitolea pia ni tatizo siku hizi
 
Huu uzi nataka uwe chachu ya watu kutusua, tunatakaa kupitia hapahapa sisi tupeane michongo mbalimbali, siku zote connection hutengenezwa, naamini kukutana hapa ktk uzi huu basi iwe n chachu ya connection mbalimbali... Hakuna ajuae kesho tupeane michongo maisha yaendeleee. Mm binafs iwe fursa yyte ile ata ya kuingiza buku kwa siku nitaileta hapa

'Maendeleo hayana chama'
 
Connection mkuu,chance ndogo zinazotokea. 5 years bila ajira it's hell living
 
Habari wana jf,

Mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 28, Ni mhitimu wa chuo kikuu, Bachelor Degree in Human Resource Management mwaka 2019, Nina ujuzi Mkubwa wa kutumia computer katika program za word, excel, PowerPoint.

Lakini pia nina ujuzi katika research kwenye data collection, data analysis kutumia excel, presentation, Leadership, Report writing Na nina uwezo mzuri wa kutumia lugha ya kiingereza.

Natafta kazi either ya kujitolea au temporary kwenye taasisi yoyote hata kwenye business sector naweza kufanya Kama customer, HR, Administrator, etc.

Nahitaji msaada wenu nduguzangu Kwa yeyote mwenye kazi au connection yoyote itakayo niwezesha kufikia lengo langu nitashukuru sana.

Nipo Tanga lakini naweza kusafiri mahali popote nafasi itakapo patikana.

Asanteni sana wakuu .
 
Mimi niliandika uzi humu wa kutafuta kazi ,nashukuru nilipata responses za kunipa matumaini, nikawatumia watu CVs then nikapata sehemu nikafanya for a year,nikiwa pale nikaona tangazo kwenye group flani la WhatsApp la ajira, nikaapply nikapata kutokana na experience niliyoipata kwa Boss wangu wa humu jf. Much respect to him👏
Hivi hayo magrupu yapo?
Humu hamna wenye group la watsap la kazi?
 
Moja kwa moja kwenye mada...

Vijana wengi wanamaliza vyuo kila mwaka ilihali wengine bado tuko mtaani hatujui hatima ya maisha yetu.Mimi binafsi nimehitimu miaka kadhaa imepita nilipomaliza chuo nilikuwa na haraka sana ya kutafuta kazi miaka inasonga ni kama zile nguvu zimeisha nahisi uchungu kusikia mtu anaongelea mambo yanahusu kazi ilihali wengine tunahangaika sana..

Kwa kweli nimeitwa interview kadhaa lakini naona kama danganya toto tu walio na iyo kazi wapo tayari wengine tunapoteza tu muda..nimefikiria kila mtu anayeweza kunipa connection lakini nako hakuna matumaini.

Sasa wandugu wewe uliwezaje kupata kazi tupeane mbinu jamani stress zinazidi
Kama ningepewa nafasi niandike hii thread ningeandika kama ilivyo bila kuacha neno hata moja ....
sababu ndio hali nlio-nnayo ipitia Kwa sasa.....
 
Ni kumwomba mungu sana kwa kuwa sasaivi kuna Secretariat ya ajira ktk utumishi Wa umma hata juzi mh mkuchika amesema wale waliozoea kuingia kazini NA vimemo muda huo hamna tena lazima upitie process through mtandao sio bahasha kama zamani unajisajili portal.ajira.go.tz- unakuwa NA profile yako huko
 
Unamwamini mwanasiasa kwa asilimia ngapi??
Ulisha kutana na mtoto wa kigogo kwenye interview hata moja Mkuu??
 
Ni kumwomba mungu sana kwa kuwa sasaivi kuna Secretariat ya ajira ktk utumishi Wa umma hata juzi mh mkuchika amesema wale waliozoea kuingia kazini NA vimemo muda huo hamna tena lazima upitie process through mtandao sio bahasha kama zamani unajisajili p
Kama ulisikiliza vizuri katibu wao pia alisema kuna' watumishi wasio waamifu wewe unadhani watumishi hao wamekosa uaminifu kwenye nini?
 
Mwenye connection kazi za usimamizi wa mauzo na masoko mkoa wowote naenda experience ya kutosha kutoka katika kampuni tofauti nne za kimataifa kwenye mikoa tofauti hapa Tanzania.

Natanguliza shukran zangu kwa mwenye connection ntamshukuru Sana.
Next time ukiweka tangazo kama hili weka na contacts direct Ili mtu akupate kiurahisi
 
Back
Top Bottom