omary khamis
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 402
- 77
Aloo!!!! Nimevutia sanaaaaaa na maandishi yako aseeKatika maisha yangu hadi sasa nilichojifunza ni kuwekeza kwa watu, kujenga urafiki na kufahamiana na watu wengi kadri unavyoweza.
Katika hili nikiri kuwa mm ndilo limenisaidia sana tena sana.
Mimi nimefanikiwa katika scenarios zifuatazo;
1. Kuna rafiki yangu anafahamiana na watu wengi sanaaa, alinishtua siku moja kuna kazi imetangazwa Bank moja lkn ni Tangazo la ndani, akampigia simu mama mmoja akamwambia nina rafiki yangu amemaliza chuo (akakitaja) anaweza kufanya ile interview?
Maza akamwambia aje kesho mchana kuna interview.
Nikaenda mzee nikapewa PC hapo imetegeshwa timer, nikaelekezwa cha kufanya, pale lilikuwa swali linakuja unalijibu ukichelewa kujibu linapotea, ukiwahi kujibu una-opt nxt question hivyohivyo linafuata lingine.... so nikavuka pale... ikaja oral kesho yake nikatusua after 2 weeks nikaanza kazi.
Ikapita kama 2 years akaja rafik wa yule jamaa aliyeniungia job Bank, akaomba mkopo nikamuhudumia vzr akapata mkopo katika kipindi kifupi, akawa mshkaji wangu. Siku moja tukiwa tunapiga story akaniuliza wewe hutaki kazi serialini, nikamuuliza kwa nafasi ipi akanieleza....akaniuliza qualification nikamwambia..... basi ikapita kama miezi miwili hapo tayar nilikuwa nimefungua stationery akaja stationery akaniamba nimtengenezee (customization) tangazo la.nafasi ya kazi ili alipeleke gazetini...nikafanya hvyo baadae akaniambia kama unaweza omba hy nafasi moja wapo lkn tu kama upo interested na kazi serikalini.
Nikaomba baada ya miezi mingi kupita nikaitwa interview, nakumbuka tulikuwa watu kama 90 na walikuwa wanataka nafasi moja kwa position yangu. Nikapiga fresh interview baada ya muda wakaita nika report, basi nika resign Bank nikaanza kazi pale....
Wakati fulani nikawa nataka kuhama ofc hiyo nihamie nyingine, kule nilikoomba nihamie wakampigia simu yy kwa sbb ndo alikuwa HR jamaa akani-recommend vzr na hatimaye nikahamia sehemu nyingine nzr zaidi na sensitive sana!!!
2. Kupitia network ambayo ninayo nimeweza kusaidia pia ndg zangu... nakumbuka kuna mdogo wangu alipata kazi mkoa fulani kwa sbb tu niliweza kuongea na washikaji na washikaji wakawa na access ya kufanikisha ajira ile ya dogo.
Kifupi mimi naamini hata matajiri ili wafanikiwe wanahitaji kwa mtaji wa watu, then mtaji wa pesa unafuata... and this is a practical katika maisha kwa ujumla wake.