Nini kilifanya CAG aliyepita, Profesa Assad kuondolewa katika nafasi ile?

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Kama tunakumbuka vizuri, ripoti ya kwanza ya CAG Assad baada ya kuingia kwa awamu ya 5 pamoja na ubadhirifu mwingine ilionesha ufisadi wa kiasi cha pesa 1.5 Trilioni ambacho hakikuoneka wapi kilienda.

Baada ya ripoti hiyo, CAG alishambuliwa sana na serikali na Chama wakiwemo mawaziri, Spika, makada na wafuasi wa Chama na Rais aliyekuwa madarakani.

Ufisadi huo ulikuwa hata ukijumlisha ufisadi na kashfa za Meremeta, Kagoda, Ununuzi wa Radar, Buzwagi na RICHMOND hazikufika kiasi cha 1.5 T. Na huo ndio ulikuwa mwaka wake wa kwanza tu wa Bajeti.

Ni vile tu vyombo vya habari viliminywa na kutishiwa huku matukio ya watu kutekwa, kupotea yakishamiri bila yeyote kusema au kuwajibika. Kulikuwa na hofu kubwa sana.

Ripoti ile haikupewa nafasi kuwasilishwa kwa Rais wala bungeni haikujadiliwa. Rais hakuwahi kuizungumzia hata kidogo kanakwamba 1.5 T ni kiasi kidogo.

Baada ya kelele kuwa nyingi za wapinzani na wananchi kuhusu 1.5 T ziko wapi ndio akaibuka Polepole makao makuu madogo 'akipiga' hesabu kutuonesha ilipo 1.5 T.

Misukosuko ilimfuata Prof Assad mpaka kutolewa katika nafasi yake. Kuna kipindi hadi kulizuka tetesi za kutekwa kwake.

Wenye akili tukajua hakukuwa na dhamira ya kweli kupambana na wizi na ufisadi bali ilikuwa ni hadaa na danganya toto huku viongozi wakijinadi kwa Uzalendo.

Sasa leo wale wapenzi na wakereketwa wa mtu mmoja badala ya Taifa mnashangazwa nini na ripoti huru ya CAG wa sasa? Ambayo hazifiki 1.5 T.

Kipi kinachowashangaza mpaka mnaleta chuki kwa CAG, spika na hata Rais Samia. Lazima tuelezane ukweli ili tusonge mbele, hizo ndege mlitaka hasara ifike ngapi? Yani hakuna mipango, madeni yanaongezeka tu, ndege haziruki kwenda nje na hasara kila siku bado mnataka tuendelee kisa tu ndio mradi wake pekee huku watumishi hawapandishiwi madaraja na kuongezewa mishahara kwa miaka mitano sasa na wastaafu mlikuwa mkiwazungusha na uhakiki mpaka leo.

Si alikuwa akisema msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Sasa kwa nini mnataka CAG asiseme ukweli? Wapinzani wamekuwa wakisema mara kadhaa kuhusu baadhi ya mambo mkawaita wahaini, wasiopenda nchi yao, wanatumiwa na mabeberu. Tulieni
 
... ripoti za CAG ni public documents. Ni muda sahihi sasa wa kuiweka report ile public ili ijadiliwe na umma, asasi, mashirika, media, mitandao, n.k. bila hofu wala kificho. Taifa linahitaji kujua kilichomo kwenye Ripoti ya Profesa Assad; ripoti iliyomfukuzisha kazi kibabe! Prof. Asad aombwe kuifafanua kwenye platforms tofautitofauti. Bila uwazi na kuelezana ukweli kama taifa hatutoboi hata aje malaika kuongoza nchi hii!
 
Nadhani alimaliza muda wake.

Ripoti yake ilitolewa Kwa uma, lakini haikuwa yenyewe. waliiedit nasikia
 
... ripoti za CAG ni public documents. Ni muda sahihi sasa wa kuiweka report ile public ili ijadiliwe na umma, asasi, mashirika, media, mitandao, n.k. bila hofu wala kificho. Taifa linahitaji kujua kilichomo kwenye Ripoti ya Profesa Assad; ripoti iliyomfukuzisha kazi kibabe! Prof. Asad aombwe kuifafanua kwenye platforms tofautitofauti. Bila uwazi na kuelezana ukweli kama taifa hatutoboi hata aje malaika kuongoza nchi hii!
Na haikuwekwa Public ile taarifa ya CAG
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Hii ripoti ya CAG imetuonyesha,kutufundisha na kutuonya kuwa tunahitaji taasisi imara na siyo mtu mmoja mwizi na fisadi anaejidai na kujinadi imara.

Kwa ushahidi wa ripoti hii ya CAG Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi,fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda ili kuaminika.
 
Kama tunakumbuka vizuri, Ripoti ya kwanza ya CAG Assad baada ya kuingia kwa awamu ya 5 pamoja na ubadhirifu mwingine ilionesha ufisadi wa kiasi cha pesa 1.5 Trilioni ambacho hakikuoneka wapi kilienda.

Baada ya ripoti hiyo, CAG alishambuliwa sana na serikali na Chama wakiwemo mawaziri, Spika, makada na wafuasi wa Chama na Rais aliyekuwa Madarakani

Ufisadi huo ulikuwa hata ukijumlisha ufisadi na kashfa za Meremeta, Kagoda, Ununuzi wa Radar, Buzwagi na RICHMOND hazikufika kiasi cha 1.5 T. Na huo ndio ulikuwa mwaka wake wa kwanza tu wa Bajeti.

Ni vile tu vyombo vya habari viliminywa na kutishiwa huku matukio ya watu kutekwa, kupotea vikishamiri bila yeyote kusema au kuwajibika. Kulikuwa hofu kubwa.

Ripoti ile haikupewa nafasi kuwasilishwa kwa Rais wala bungeni haikujadiliwa. Rais hakuwahi kuizungumzia hata kidogo

Baada ya kelele kuwa nyingi za wapinzani na wananchi kuhusu 1.5T ziko wapi ndio akaibuka Polepole makao makuu madogo 'akipiga' hesabu kutuonesha ilipo 1.5 T

Misukosuko ilimfuata Prof Assad mpaka kutolewa kwake. Kuna kipindi hadi kulizuka tetesi za kutekwa kwake.

Wenye akili tukajua hakukuwa na dhamira ya kweli kupambana na wizi na ufisadi ila ilikuwa hadaa na danganya toto huku viongozi wakijinadi kwa Uzalendo.

Sasa leo wale wapenzi na wakereketwa wa mtu mmoja badala ya Taifa mshangazwa nini na ripoti huru ya CAG wa sasa? Ambayo hazifiki 1.5 T.

Kipi kinachowashangaza mpaka mnaleta chuki kwa CAG, spika na hata Rais Samia. Lazima tuelezane ukweli ili tusonge mbele, hizo ndege mlitaka hasara ifike ngapi? Yaani hakuna mipango, madeni yanaongezeka tu, ndege haziruki na hasa kila siku bado mnataka tuendelee kisa tu ndio mradi wake pekee huku watumishi hawapandishiwa madaraja na kuongezewa mishahara miaka mitano sasa na wastaafu mlikuwa mkiwazungusha na uhakiki mpaka leo

Si alikuwa akisema msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Sasa kwa nini mnataka CAG asiseme ukweli? Wapinzani wamekuwa wakisema mara kadhaa kuhusu baadhi ya mambo, mkawaita wahaini, wasiopenda nchi yao, wanatumiwa na mabeberu. Tulieni
Tulikuwa tunapigwa sana awamu iliyopita na mademu zetu kugongwa at will. Mungu angalau katuletea maza kutufariji.
 
Hii ripoti ya CAG imetuonyesha,kutufundisha na kutuonya kuwa tunahitaji taasisi imara na siyo mtu mmoja mwizi na fisadi anaejidai na kujinadi imara.

Kwa ushahidi wa ripoti hii ya CAG Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi,fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda ili kuaminika.
Na kuwadanganya wasiojielewa kuwa ni Mzalendo
 
Back
Top Bottom