Elections 2010 Nini kilichotokea Zanzibari? ni muafaka tu au kuna kingine Tusichokijua

Tuzo

Member
May 26, 2009
24
2
Nilivyomuona Shariff Hamad akiyapokea matokeo na kutoa pongezi kwa Shein, ilikua kama alishayajua matokeo muda mrefu tu..... Na ukiiangalia picha hii (toka michuzi blog) Mshindi na mshindwa wakishangilia pamoja imenishangaza sana.sijawahi kuona mshindwa akimsaidia aliyeshinda kushangilia. atleast angekaa kimya akiobserve mwenzake akishangilia.Ni muafaka tu or?
 
Alikubali yaishe kuliko kumwaga damu zawatu anaowapenda mno wa nchiyake ya zanzibar,ni mfano wakuigwa ktk viongozi wakiafrika waliojaa uroho wamadaraka,kwa hakika anastahili kupewa nishani ya amani ya nobel yeye maalim seif na rais mstaafu mh.aman abeid aman karume,hakika historia ya nchi hii haitowasahau milele kwa muafaka wakweli walioufanya,mungu ayalinde makubalianohaya ya wazanzibari amiin.
 
Jamani kwanini siku zote tunakua na mashaka? Kama ingekua Maalim Seif hajapewa madaraka mgesema CCM imeiba kura, amepewa madaraka kwaajili ya kudumisha Zanzibar na wanaanchi wake na kutengeneza serikali ya mseto sasa imekua habari ya kuafaka. What is this people, why can't we get along na tuwe tayari kuibeba nchi yetu? Maalim Seif na Dr.Shein ni watu watulivu sana, waachieni waanze kulijenga Taifa.
 
Nilivyomuona Shariff Hamad akiyapokea matokeo na kutoa pongezi kwa Shein, ilikua kama alishayajua matokeo muda mrefu tu..... Na ukiiangalia picha hii (toka michuzi blog) Mshindi na mshindwa wakishangilia pamoja imenishangaza sana.sijawahi kuona mshindwa akimsaidia aliyeshinda kushangilia. atleast angekaa kimya akiobserve mwenzake akishangilia.Ni muafaka tu or?

If you want to defeat them be part of them!!

subiri serikali itangazwe nd utajua cha zaidi ndani ya hayo uloyaona.:tape::tape::tape:
 
kwa ukweli nawaonea wivu waZbar, ubinafsi wa viongozi uko pembeni, wanafikiria maslahi ya nchi yao na watu wao,
najua kinachofuata ni kufikira jinsi ya kuiteka bara, we utaona tu.
 
Hii style hata huko Kilwa imetokea CUF na CCM wakishangalia pamoja sijui wamechakachua hizo sare?
 
shein%26kikwete.JPG
 
Hii style hata huko Kilwa imetokea CUF na CCM wakishangalia pamoja sijui wamechakachua hizo sare?
:smile-big: Ukiuza utumbo usiogope nzi mkuu... pana maana pana sana hapo:smile-big: UNAJUA KILICHOTUPONZA BARA HUKU... TUMEMKIMBIZA MWIZI WETU KWA MAKELELE AKAPATA PA KUJIFICHA.. KULE PEMBA MWIZI ALIKIMBIZWA KIMYAKIMYA NDO MAANA SISIEMU WAKITEGEMEA KUPATA KITI WAKAKOSA, NA UNGUJA IKAWABIDI WANYANG'ANYE, AMA HAMKUJUA KWAMA MAALIM ALISHINDA KWA 54% ???
 
Mbona hawa hawakamatwi kwa kumvalisha ngombe kofia ya ccm

nashangaa kwa sababu hata wale waliomvalisha mbwa tshirt ya ccm walikua wanatafutwa, sasa na hawa waliomvalisha n'gombe kofia? au ng'ombe ana thamani sana kwa sababu ya nyama? huku mbwa naye akiwa na thamani ya ulinzi. utataaaaaaaa
 
..nadhani situation ya Zenj ni unique.

..with the benefit of a hindsight, huu mseto ulitakiwa uwepo tangu wakati Zenj wanapata uhuru toka kwa Muingereza.

..Wazungu wana msemo wao wa "better late than never." finally serikali ya Mseto ipo Zenj, sasa hakuna sababu yoyote ile ya Zenj kutokupiga hatua za maendeleo kwa haraka.
 
kwa ukweli nawaonea wivu waZbar, ubinafsi wa viongozi uko pembeni, wanafikiria maslahi ya nchi yao na watu wao,
najua kinachofuata ni kufikira jinsi ya kuiteka bara, we utaona tu.

Sio CCM
Kama kweli wanafikiria maslahi ya nchi yao na watu wao
wangeacha nguvu ya wananchi itumike na sio kuwaibia kura
 
Seif hakukubali matokeo kirahisi hivyo, maana inaonyesha alishinda! Mwinyi huyu huyu ndiye aliyetuliza mzuka ambao ungezuka Zanzibar kuliko kipindi chchote katika historia hii! akina mama wa CUF walikuwa wanasubiri matokeo ili hali wakitoka machozi!!

No doubts next president atakuwa Seif huko zanzibar na hivi ndivyo walivyokubaliana. Offocurse influence ya CUF na hii 'kukubali matokeo' zanzibar ndiyo umesababisha bara akina Lipumba kushangilia hali wakijua zanzibar yao 2015!!!!!
 
Sijui ni macho yangua ama...........huyu jamaa suka wa mkokoteni naona kama napunga mfuko wa kiroba cha cognac! ama ni mimacho yangu?:smile-big::smile-big:
 
Kilichotokea Zanzibar ni uelewa kuwa maslahi ya Taifa ni lazima yaekwe mbele, ni kukaa na kupima between two side of coin. Kama Maalim Seif angeyakataa matokeo Dkt. Shein angelitangazwa tu na ndio ungelikuwa mwisho wa Serikali ya Kitaifa na kwa vyovyote vile roho za wananchi wasio na hatia zingepotea - Wazanzibari wangalirudi nyuma zaidi kuliko kabla ya makubaliano yao.
Lakini tuangalie walipo sasa sehemu hii ya Tanzania iko kwenye utulivu wa hali ya juu ingawa huwezi kuwaridhisha wote lakini wengi ya wakazi wake wamefurahishwa na hali hii na ndio ukawa unawaona wanashangilia ushindi kwa kila mtu anavyoelewa kwani ni ushindi wa Wazanzibari wote.
Kitachotokea ni kunyongonyea utawala wa CCM Zanzibar kwani ukitaka kuuangusha Mti mkubwa aanza kuupekecha kuliko kutaka kuupiga shoka moja tu - hii ndio nafasi aliyoiona Maalim Seif at last na ndio anayoitumia.
 
Zanzibar ya leo wa kupewa sifa na heshima ni Aman Abeid Karume, aliyekuwa jasiri kufuata nyayo za Abood Jumbe na Maalim Seif lakini katika akili ya hali ya juu kabisa ambayo mtu wa kawaida huwezi kubaini. Amani Karume aliweza kuiweka CCM kando na kuangalia Zanzibar kwanza. Akatoa utata wote kuwa Zenji sio nchi na Zenje ina Amiri Jeshi Mkuu.

Sifa kwako Karume Jr.
 
Seif hakukubali matokeo kirahisi hivyo, maana inaonyesha alishinda! Mwinyi huyu huyu ndiye aliyetuliza mzuka ambao ungezuka Zanzibar kuliko kipindi chchote katika historia hii! akina mama wa CUF walikuwa wanasubiri matokeo ili hali wakitoka machozi!!

No doubts next president atakuwa Seif huko zanzibar na hivi ndivyo walivyokubaliana. Offocurse influence ya CUF na hii 'kukubali matokeo' zanzibar ndiyo umesababisha bara akina Lipumba kushangilia hali wakijua zanzibar yao 2015!!!!!

Naamini Mwiny aliahidi kitu huko, mimi binafsi nina mashaka na muafaka; kama maalim alishinda kwa nini walazimishe wao ndo waanze? Si serikali ni ya umoja wa kitaifa!!! Kwa nini inabidi maalim ndo awe wa kupewa!!!?
:tape::A S angry::doh:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom