Nini kigezo cha kuchagua watu kuwa Viongozi mbalimbali wa kamati za Bunge?

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,503
252
Kwa ajili ya kuboresha utendaji wa bunge na kuifanya Serikali iwajibike ipasavyo kwa wananchi wake Bunge liliamua liwe na kamati mbali mbali ambazo zitakuwa zikifuatilia mambo mbalimbali ya msingi mathalani utendaji wa mashirika ya UMMA, mambo ya Ardhi, Elimu, Kilimo, Mambo ya nizamu, Ulinzi na Usalama, Mambo Ya fedha na nyinginezo nyingi.

Kamati hizi hupaswa kuwa na watu makini na wenye uzalendo na uchungu wa nchi yao.

Sasa swali linalo nitatiza mimi ni hili:::Je ni kigezo gani huwa kinatumika kuchagua viongozi wa kamati hizi?

Na kama kigezo ni hicho hapo juu kinazingaziwa je unazani kamati zote zina viongozi wanaostahiki au Kuna ambazo unamashaka nazo kama Mtanzania Mzalendo na mpenda maendeleo?

Tujuzane
 
ukikubalika sana na ccm hata ukiwa upinzani utapata uongozi wa hizo kamati,ukiwa muuza unga unakuwemo kwenye kamati(idd azzan-hesabu serikali za mitaa),mla rushwa(zambi) etc etc etc
 
Kwa ajili ya kuboresha utendaji wa bunge na kuifanya Serikali iwajibike ipasavyo kwa wananchi wake Bunge liliamua liwe na kamati mbali mbali ambazo zitakuwa zikifuatilia mambo mbalimbali ya msingi mathalani utendaji wa mashirika ya UMMA, mambo ya Ardhi, Elimu, Kilimo, Mambo ya nizamu, Ulinzi na Usalama, Mambo Ya fedha na nyinginezo nyingi.

Kamati hizi hupaswa kuwa na watu makini na wenye uzalendo na uchungu wa nchi yao.

Sasa swali linalo nitatiza mimi ni hili:::Je ni kigezo gani huwa kinatumika kuchagua viongozi wa kamati hizi?

Na kama kigezo ni hicho hapo juu kinazingaziwa je unazani kamati zote zina viongozi wanaostahiki au Kuna ambazo unamashaka nazo kama Mtanzania Mzalendo na mpenda maendeleo?

Tujuzane
Kutokana na shughuli za kamati ya bunge kama ulivyozielezea, moja ya sifa kubwa ya wajumbe wake ni kuwa na background ya kufanya kazi katika hizo sector sometime in their lifetime au kuwa na elimu ya kuweza kuelewa mambo yanavyotakiwa kufanywa hili kuleta ubora katika hizo sectors.

Kamati azitakiwi kuwa na mabishano ya kisiasa kama wanavyokuwa bungeni bali kujadili maendeleo ya wizara au sector husika kuhusu mwelekeo wake na faida zake ki ujumla kwa taifa. Ndio maana kwenye mataifa mengine utaona inawaita wafanya biashara kuelezea mwenendo wao kama wameona foul play ambayo serikali inafumbia macho au hata kutafuta opinion zao kuhusu kodi kadhaa na faida za hiyo sector au effect za kodi katika sector.

Wanaweza pia kumwita waziri kuelezea utendaji wake panapo utata na kutaka ufafanuzi mawaziri wa wenzetu wanajua everything that is happening in their ministries maana wao ndio wakutetea au kuwajibishwa if things go wrong, UK wao wanaweza mwita mpaka waziri mkuu kuelezea kwenye utata kama yeye ni muhusika wa policy au maamuzi.

Kigezo kikubwa hapa ni previous knowledge and experience ya mwanakamati, na kwenye nchi anzilishi ya mambo haya ya kamati 'USA' na wengineo waliokopi huu mfumo wameamua asilimia kubwa ya wanakamati wabaki walewale so long as wataendelea kuchaguliwa majimboni na ikiwa majukumu yao mengine hayawazuii kukaa kwenye kamati, the idea behind it is that they will gain more and more experience to be able to scrutinize the government organs, polices and it wider impact for them to produce effective checks.
 
Back
Top Bottom