Nini kifanyike unapokuta Mgombea wa Chama cha upinzani anapoungwa Mkono na Viongozi wa Chama Tawala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kifanyike unapokuta Mgombea wa Chama cha upinzani anapoungwa Mkono na Viongozi wa Chama Tawala?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Mar 27, 2012.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mimi napata mashaka kidogo na utata wa swala kugombea nafasi ndani ya Chama cha upinzani ila hali ukiungwa mkono kwa hali na mali kutoka chama tawala......

  Hii inaleta tafsiri tata sana mfano unapokuta kijana anatangaza nia ya kuukwaa umwenyekiti wa Chama pinzani wanajitokeza watuhumiwa wa ufisadi na wanaokikandamiza nchi hii na watu wake kwa miaka 50 na kumwaga sifa na kumjazia pesa kwenye acount zake ni swala la kulifanyia kazi na si kucheka cheka kama ambbavyo marafiki zangu wanafikiri.

  Tufike mahali to employ great thinkers pengine watusaidie what is behind this move.... Mimi nafikiri kila mtanzania ana majibu.

  Leo hii akija mgombea yeyote katika nafasi yeyote iwe ubalozi au Rais, anaungwa mkono na any one of member katika ile list of shame au mtu yeyote mwenye uhusiano directly or in directly lazima tumjadili kwa kina sana na tujiridhishe kulikoni. Haijalishi hata kama anaushawishi kiasi gani lazima tumchunguze sana....

  Inapotekea mtanzania yeyote anatamka na kuseama ANATAKA SANA URAISI lazima tumchunguze na kujua ana nia gani?


  Mimi naanza uchunguzi wangu kuanzia leo hadi 2015
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  stein na ww umevutwa na title za magazeti

  1. hajasema anagombea mwaka 2015
  2. amesema chama chake kikiamua...na wananchi wakiridhia
  3. kasema ndoto zake

  plz acheni kufuata mkumbo jamani aibu ya karne hii....usiwe kama mtei bana

  zito 2015 hana umri wa kugombea urais pleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeese
   
 3. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Waberoya,

  Anyway Sikumtaja lakini kama akiwa kwenye hiyo group ni sawa tujadili... Ila kikubwa ni tufanye nini kama mgombea nafasi ya umwenyekiti au Urais kutoka upinzani anaungwa mkono na chama tawala na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi hasa katika nchi kama hii yetu?

  Na ikafika hatua hadi wakaanza kumwezesha kifedha na mambo mengine?
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama kweli mgombea wa Chama cha upinzani anaungwa mkono na Chama Tawala basi mimi ninashauri huyo mgombea asimamishwe kugombea URAIS.

  Kwani kama atasimamishwa huyo mgombea, chama tawala kitaondoa katika kinyang'anyilo cha urais mgombea wao. Hivyo huyo mgombea wa upinzani anayeungwa mkono na chama tawala ATAPITA BILA KUPINGWA.

  Lakini kama anaungwa mkono na chama tawala, halafu bado chama tawala kikasimamisha mgombea wake, basi hilo ni changa la macho. Kwani cham tawala CCM kina kawaida ya kuunga MKONO wagombea weak, ili kipate ushindi wa mchekea! Na kuawapiga vita wagombea wanaotoa upinzani kwake. Mfano Augustine Mrema NCCR 1995, Prof Ibrahim Lipumba CUF 2000, Dr. Slaa CDM 2010. TAFAKARI
   
 5. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda sana hii, ila kama anaungwa mkono na wapiga kura nadhani siyo issue kwani wapo waTZ wa kawaida ambao hawanufaiki na ufisadi unaoendelea nchini lakini ni wanaCCM na wanasema wao huchagua mtu na si chama..
   
 6. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anayeungwa mkono na chama tawala anafaa sana maana atapata majority ya kura, za wapinzani wenzake na chache za watawala.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  akiungwa mkono na ikathibitika akiungwa mkono wananchi wataamua!!! unless unasema tukijadili na kufikia conclusion basi tuta endorse tulichoamua..hatuna nguvu hiyo!!

  theoretically we can say anything and

  Practically iko tofauti kabisa.....hawa watu wetu wa kofia na kanga na kilo moja ya mchele wako kivinginge

  Personally sita-msupport mtu ambaye anaungwa mkono na mafisadi waliothibitika ni mafisadi..Kama fisadi yuko mtaani , huyo siyo fisadi
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu kote tumeenda sawa,ila hapa mwisho umeniacha kidogo,unasema kama fisadi yupo mtaani huyo si fisadi,kwa maana ya kua yule ambae hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria lakini anahisiwa na kutajwa au???
   
 9. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Issue si kushinda kwa kura nyingi issue ni utakuwa kiongozi kwa maslahi ya nani?, si mara ya kwanza tunaona haya ni sehemu nyingi sana hapa kwetu.. Leo hii mtu akiungwa mkono na mafisadi do you think atakuwa pale kwa aslahhi ya wengi au wale wenzake wachache..

  Nadhani ifike mahali kiongozi anatambuliwa na mtu na si mtu kuutaka uongozi ..
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Waberoya, naomba tuwe realistic.
  Ninaona unataka watu wachukulie kauli ya Zitto kirais rais sana kwa misingi ya kwamba ni haki yake kuwa na nia, na sasa naona unasema kauli yake sio issue sababu by 2015 atakuwa hana umri unaoruhusiwa kikatiba kugombea urais.

  Sijakuona ukitoa maoni juu ya taswira zifuatazo.
  1. Kwanza, kwamba ZITTO sio kama Nape au John Shibuda, kwamba wakisema wanataka kugombea urais kauli zao tutegemee ziwe na weight kama kauli ya Zitto, ni sawa sawa na mtu mmoja kauliza kwamba mbona hamad aliposema anataka kugombea uenyekiti au ukatibu mkuu cuf haikuwa issue ila zitto kutaka urais inakuwa issue?

  naomba tuwe realistic katika hili, na ushahidi tunao kwamba hapa hapa JF ameleta mvurugano, ZITTO ana nguvu fulani za kisiasa nchini.na ninakubaliana na wewe asilimia mia kwamba ni haki yake kuwa na nia na hata kuelezea nia hiyo. lakini kwa nguvu alizonazo kama na yeye anazijua kutoa kauli kama hiyo katika kipindi ambacho chama chake kiko kwenye mchakato muhimu sana wa maendeleo yake ni ABUSE OF HIS INFLUENCE.

  NA HAPA AMEONYESHA JINSI ALIVYOPUNGUKIWA NA BUSARA ZA UONGOZI.
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  fisadi hawezi kuwa mtaani bana! fisadi hawa tunakula hotelini mwao, tunanunua bidhaa zao, tunapanga nyumba zao na kupanda daladala zao!! I am talking about criminalised society it seems we have accepted them!
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  busara is a relative term bro.
   
 13. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duh kweli Zitto ana damu ya kunguni
   
 14. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu ukufuatilia wengi wa wanaotaka Zito agombee Urais au Umwenyekiti wengi wao ni WanaCCM, au Watuhumiwa wa ufisadi na wanamwambia si kwa kuitakie mwa TZ bali kuipunguzia mnguvu CCM...

  Kibaya Zaidi hata Zito analifahamu hilo.. Mimi nawashukuru sana viongozi wa CDM kwa kumwacha kama alivyo maana Zito haeleweki...

  Tukifuatilia hata humu JF wanaotaka Zito awe Rais kama si Fisadi ni mwana CCM mfano JK, Makamba, au baadhi wa watu wa Kigoma kwa sababu zao binafsi..
   
Loading...