Nini kifanyike Taifa Stars iende Cameroo?

Simchezo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
443
344
Wadau, hivi tufanyaje ili twende Cameroon? Je tukiifunga Uganda na Lesotho wakaifunga Cape Verde idadi sawa ya magoli nani ana advantage? Tuanze kujadili namna ya ku move forward badala ya kulalamika. Ahsanteni.
 
Hivi Amunike alishawahi kuwa kocha? Bora Maximo stars ilikuwa inaonyesha hata shoo gemu kuliko hii ya amulike
 
Wapige ganzi wachezaji wa Uganda na Ndege ya Lesoto ihujumiwe wasiende Cape Verde. Tutumie mfano wa kukosa hoja ukatumia ubabe.
 
Wadau, hivi tufanyaje ili twende Cameroon? Je tukiifunga Uganda na Lesotho wakaifunga Cape Verde idadi sawa ya magoli nani ana advantage? Tuanze kujadili namna ya ku move forward badala ya kulalamika. Ahsanteni.
simple. sasa ni payback time kwa Uganda.
tuliwabeba kwa kumng'oa nduli Amini nao sasa watubebe.

lolzzzzz!!!!
 
Njia rahisi ni kununua gemu ya Uganda
kwenye michuano hiyo sio kitu rahisi kama unavofikilia,ikibainika tu uganda anapigwa faini na kufungiwa miaka mitatu!!!je yupo tayari kufanya hivyo? na wewe pia unafungiwa!!kilichopo ni kupiga mpira tu japo kwa mpira wetu huu ni ngumu kumfunga uganda
 
Wadau, hivi tufanyaje ili twende Cameroon? Je tukiifunga Uganda na Lesotho wakaifunga Cape Verde idadi sawa ya magoli nani ana advantage? Tuanze kujadili namna ya ku move forward badala ya kulalamika. Ahsanteni.
cape vedre akishinda tu hiyo mechi yake hata kwa bao moja tu sisi hata tushinde mabao 100!!hatuendi kwani wanachoangalia ni HEAD TO HEAD
 
Tupige la Nape
 
Tuwaachie wenye uwezo waende huko.. Sie hata ikitokea miujiza tukaenda huko tutadhalilishwa vibaya sana.. Bado hatujapata huo uwezo, na tuache pia kupeleka lawama kwa makocha.. Nashangaa hatujiulizi hivyo vilabu vyetu tu, (ambapo wachezaji wengi wa timu ya taifa wanatokea) vinachemsha kwenye mashindano ya Africa..
 
Ni kuliiiba tu.

Au tumuite mkurugenzi wa tume ya uchaguzi wa Tanzania afanye yake.

Kama anaweza kuifanya ccm ishinde,afanye yake taifa stars ishinde.
 
Cape Verde bado wananafasi..Wale Lesotho hawawezi kuwafunga Cape Verde kwao labda draw kwa taaabu...Uganda anakufa kwa mchina(yule mganga wa Yanga apewe pesa..Kagere mechi na Yanga anasema alikuwa anamuona Kakolanya mkubwaa kama king Kong)I'm joking
 
cape vedre akishinda tu hiyo mechi yake hata kwa bao moja tu sisi hata tushinde mabao 100!!hatuendi kwani wanachoangalia ni HEAD TO HEAD
Kwani Cape Verde si ana point 4 sisi tuna point 5...mechi ya mwisho Cape verde akishinda anakuwa na 7 na sisi tukishinda tutakuwa na 8.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom