SoC01 Nini kifanyike Serikali iweze kupata pesa baada kuachana na hii tozo kandamizi na wapi pa kuwekeza

Stories of Change - 2021 Competition

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
778
Katika hali isiyo ya kawaida maisha ya mwanadamu hasa mtanzania yanazidi kuwa magumu sana. Huku anadaiwa kodi ya nyumba na kuiendeleza familia na ndugu zake, huku anatakiwa kushiriki michango mbalimbali ya serikali ya kijiji, huku michango ya msikitini na makanisani inamsubiri yeye, huku mambo ya kijamii kama michango ya harusi na misiba inamuangalia yeye na asiposhiriki anatengwa na jamii.

Katika hali ya kuguswa na maisha magumu ya mtanzania, serikali HAIKUSTAHILI kuja na Tozo mpya kwenye miamala ya simu kwa sababu huu ni unyonyaji usiokubalika hata kuzima. Fikiria kila muamala ambao mtu huufanya mtandaoni, 18% hukatwa kama kodi iendayo serikalini na hata siku moja watanzania hawajawahi goma kuilipa, sasa kama mtu anamkata 18% then unaongeza Tozo kwenye huo muamala MIMI NADHANI HUO NI UNYONYAJI UNAOSTAHILI KUPINGWA KWA NGUVU ZOTE. Wanaotusisitizia tukubali hiyo tozo kandamizi wao hata kodi tu kwenye mishahara yao wameiondoa.

Nini kifanyike serikali iweze kupata pesa baada kuachana na hii tozo kandamizi.

1. Serikali kuondokana au kupunguza matumizi yasiyo ya lazima

Hii imekuwa upofu kwa serikali ya Tanzania kila awamu inayoingia madarakani kuendeleza na kulipia gharama kubwa mambo yasiyo na maana yoyote katika taifa hasa kiuchumi maana zaidi ya yote inaongezea tu serikali mzigo.
>Hivi kuna haja gani ya serikali ya kimasikini kama hii yetu ya Tanzania kuwa na wabunge zaidi ya 300 hadi 400 ambao kila mmoja mmoja hulipwa zaidi ya 10 Million kila mwezi?​
Mimi napendekeza idadi ya wabunge ipunguzwe hadi ibaki 1/3 ya wabunge wote waliopo bungeni. Kwa kuokoa 2/3 pesa inayoenda kwa wabunge ambao wengi wao ndo wamepelekea umaskini mkubwa unaolikumba taifa letu, serikali inaweza kuchukua pesa hizo na kuzielekeza kwenye miradi inayogusa raia wengi.​
> Hivi kuna haja gani ya kuwa na wakuu wa wilaya katika serikali yetu? Hivi fikiria katika halmashauri unakua na mbunge, mkuu wa wilaya, na mkurugenzi conflict of interest inaanzia hapa. Mimi napendekeza nafasi ya mkuu wa wilaya Tanzania nzima ziondolewe na majukumu yao wapewe wakurugenzi wa halmashauri chini ya usimamizi wa Wakuu wa mikoa. Hii itapunguzia serikali mzigo mkubwa wa kulipa mshahara watu hao ambao kiuchumi hawazalishi. Pesa itakayookolewa hapa ipelekwe kwenye miradi ya maendeleo inayogusa raia wengi.​
>Hivi katika taifa maskini Kama hili la Tanzania, kuna haja gani viongozi kujinunulia magari ya bei juu (v8) kwa pesa za serikali, kufanya mikutano kila mwezi kwenye mahoteli ya bei juu, kufanya ziara kwa rundo la msafara wa magari. Watanzania hatuna haja na mbio za mwenge hilo nalo jipu linalokula pesa nyingi za serikali kwa maana kama ni ishu ya mbio za mwenge kukagua miradi ya maendeleo Tanzania nzima kwani kazi ya Wakuu wa mikoa, mawaziri na Rais nini? Ondoa gharama kubwa za mbio ya mwenge. Pia Tanzania hatuna haja na baraza kubwa la mawaziri, kuna wizara zinaweza kuunganishwa na kuwa wizara moja hiyo piai itasaidia kupunguza matumizi makubwa ya serikali.​
2. Tanzania kutumia ushawishi wake kimataifa kuomba Mikopo

Watanzania mikopo sio mibaya kama unakopa kwa ajili ya kufadhili jambo ambalo lina manufaa kwa raia wengi. Kuna mikopo ya pesa na mikopo ya vitu. Kwenye mikopo ya pesa Taifa la Tanzania tumefeli vibaya na ndio maana unaweza kuona Deni letu la taifa limeongezeka angali uchumi wetu unashuka. Sasa badala ya kukopa Pesa, serikali inaweza kwenda kwenye mataifa yaliyoendelea na kukopa vifaa na mashine. Mfano matrekta kwa ajili ya kilimo cha kisasa.

3. Kubinafsisha au kuuza rasimali tulizo jaliwa na Mungu

Tanzania tumejaliwa na kubalikiwa kwa kuwa na rasilimali nyingi sana. Swali common sana kwa shule za msingi na O level, hivi ni kwa nini tuna rasilimali nyingi sana lakini taifa letu bado ni masikini?

Jibu ni kwamba bado hatujajua namna ya kutumia hivyo tulivyo navyo na mwisho tunasukumwa na ubinafsi wa watu wachache ndo waone wana haki ya ku enjoy rasimali za taifa.

Chukulia mfano ziwa Victoria, bahali yetu ya hindi kuna visiwa vingapi ambavyo tunaweza kubinafsisha kwa watu wa ndani au wa nje waviendeleze na serikali ikusanye hapo mapato. Vipi kuhusu wanyama poli kama Nyumbu, pundamilia, viboko, swala tulionao wengi hifadhini kwetu, kuwe na utaratibu wa kuwauza kwa wananchi ili watumike kama vitoweo hii pia itasaidia serikali kukusanya mapato bila kuwaumiza wanachi.

Baada ya serikali kuwa imeweza kutunza na kuongeza mapato hayo nini iyafanyie. Kikubwa serikali baada ya kufanya hayo idhamilie kuwekeza katika sekta zinazosaidia kukuza uchumi kwa haraka kama sekta ya Kilimo, Nishati na teknolojia

Pia serikali izingatie kuboresha ustawi wa wanachi wake kwa kuboresha sekta ya Elimu, Afya na Maji ili kusaidia akina mama huko vijijini kupata maji kwa ukaribu katika vijiji vyao.

Bonyeza sehemu ya Vote kupigia uzi huu kura.
Asante
 
Back
Top Bottom