nini kifanyike mwaka 2011 kulikomboa taifa la tanzania dhidi ya ufisadi?

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
wajumbe tunahitaji michango yenu nini kifanyike mwaka ujao ambacho kitasaidia kuondoa ufisadi?
 
Tuwasupport viongozi wetu wenye msimamo wa kupinga ufisadi kwa dhati! Tutekeleze kwa vitendo watayo tuambia.
 
Watanzania wenye uchungu na nchi hii, wenye uelewa na wenye moyo wa ukakamavu, tuamue kupambana na hawa mafisadi kwa kuwahoji uhalali wa mali zao, uhalali wa unyang'anyi wanaoufanya, uhalali wa dhuluma zao kwetu wote. Kundi la kwanza linalonikatisha tamaa ni wasomi wa nchi hii ambao wanwaogopa viongozi wa nchi kuliko mungu wao.
TUMEKWISHA maana viongozi wetu wote ni KUNDI LA SHETANI NA WAHUNI TU. Hakuna na mtoto wa Mkulima wala wa Ngoyai wote sawa tu.:embarrassed:
 
wajumbe tunahitaji michango yenu nini kifanyike mwaka ujao ambacho kitasaidia kuondoa ufisadi?

huwezi kuondoa ufisadi..... kwani hii ni ecological niche ...... simba wanakula swala..... binadamu wanakula sato...... mimea inavuta carondioxide .... fisadi anakula na kuhujumu wananchi...... labda kupunguza ufisadi
 
Nafikiri kuna haja ya kuchunguza kwanza ni nini chanzo cha ufisadi. Hawa tunaowaita mafisadi ni Ndugu zetu, Majirani zetu, Kaka zetu, Baba Zetu, Mama Zetu, Wadogo Zetu au hata marafiki zetu na ni watu tunaoishi nao katika jamii. Swali ni je kwanini ni mafisadi?

Mimi nafikiri kinachochangia ufisadi ni kukosekana na mwamko wa utaifa na kukithiri kwa ubinafsi kunakotokana na kuendelea kwa kuzorota kwa hali mbaya ya huduma za jamii.

Pia Uvivu na kukosa dira lakini pia kuendelea kwa umasikini unaotokana na kipato kidogo ambacho huwa ni msukumo wa kupokea rushwa au kulazimika kufanya ufisadi ili kuweza kupata fedha za kumudu gharama kubwa za maisha ya sasa.

Ukiangalia kwa umakini utakuta Ufisadi umezunguka katika sababu hizo.

Suluhisho la kuondokana na Ufisadi:

1. Kuna haja ya Viongozi wetu kuamsha dhana ya utaifa na kusisitiza ufanyaji kazi kwa bidii na kujituma kwa uadilifu.

2. Pia kuna haya ya kusisitza katika uwiano wa vipato pamoja na kupunguza gharama za Serikali katika mambo ambayo yanaonekana kufaidisha wachache (Kwa mfano Ununuzi wa Magari ya Kifahari).

3. Kuelekeza nguvu katika taaluma na maendeleo ya sekta ambazo zinaonekana hazina thamani katika jamii kama (ualimu, polisi, madaktari na wahandisi).

4. Kuchukua hatua za kisheria bila ya Uonevu na bila ya kuonea huruma wale ambao wanabainika kufanya ufisadi au kuliingiza taifa katika gharama kubwa na mzigo wa madeni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom