Consultant
JF-Expert Member
- Jun 15, 2008
- 11,401
- 20,661
Uchaguzi huu umekwisha na Upinzani unapaswa kucheza karata zake vizuri ili kuepusha majanga mengine mwaka 2025. Kelele za kutaka uchaguzi urudiwe hazitozaa matunda sasa ambapo hata maandamano tu ya kupinga Mbowe kupewa kesi nzito yamefail.
Nini kifanyike
1. Wale Wapinzani wawili walioachiwa majimbo waachwe waingie Bungeni wakapiganie haki. Hii haitakuwa kubariki wizi uliofanyika.
2. Viti maalumu kutoka CHADEMA nao waende bungeni. Haki itendeke kwenye kuteua nani aende ili kuepuka kukipasua Chama zaidi.
3. Agenda kuu Bungeni kila mpinzani anaposimama iwe ni kudai KATIBA MPYA/marekebisho makubwa ya Katiba pamoja na kuifumua NEC.
4. Wapinzani waliopo nje ya Bunge watumie platforms zote kuimba wimbo mmoja: KATIBA mpya na NEC iliyo huru.
5. Ikitokea akafa Mbunge, Upinzani uwe umeshadeclare mapema kutokushiriki marudio yoyote ya Uchaguzi kwa NEC hii ya sasa.
6. Warsha mbalimbali ziandaliwe na kuibua mijadara ya umuhimu wa Katiba mpya/muundo wa NEC iliyo huru. Wanaweza kualikwa wadau mbalimbali hasa wale development parners (a.k.a mabeberu) ambao wana mchango mkubwa kwenye bajeti ya Serikali na hivyo wakikohoa kidogo tu Jiwe anaweza kuwasikia na kutii.
7. Wapinzani wajipange na kufungua matawi mpaka kwenye ngazi za kata. Mafunzo yaanze kutolewa mapema ili by 2025 kuwe kuna misingi imara na hata iwe rahisi kupata mawakala bora kuliko ilivyokuwa mwaka huu.
Kususa haitakuwa strategy nzuri. Sanasana itawapa nafasi CCM kujiandaa vizuri mwaka 2025 na wao wakaja na system ya “kura za mapema” kama ilivyokuwa Zanzibar mwaka huu ili waibe kiulaini na kufunga hesabu mapema.