Nini kifanyike kuwawekea mazingira mazuri ya biashara wachuuzi Tanzania

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,227
26,047
Amani iwe nanyi. Natumai wote mu wazima na mnaendelea vizuri na majukumu yenu.

Leo katika makala zangu za kushauri juu ya mambo gani tunatakiwa tufanye, nimeona ni vizuri nishauri juu ya suala kama linavosomeka kwenye mada yangu hapo juu.

Natumai kuna wenye macho wanasoma na siku moja inaweza tokea yakaja kufanyiwa kazi.

Tanzania kwa kifupi kumekuwa na ongezeko kubwa la wachuuzi nikimaanisha wafanyabiashara wadogo ambao wamekuwa wakifanya biashara zao kwenye maeneo ambayo hayajapangwa au kuwekwa vizuri.

Si jambo la ajabu kwa hapa Tanzania kukuta wachuuzi wamepanga biashara zao chini kwenye udongo au wakiwa wamejenga vibanda vyao vya mbao au mabati pembeni mwa barabara kiasi ambacho kinafanya sio tu maeneo yetu kuwa machafu bali kinafanya pia maeneo yetu kuonekana vibaya, kutopendeza na pia kuharibu mipango mingi.

Ukiwa unaingia mkoani Dar es Salaam kwa pande zote mfano Bunju, Mbezi ya Kimara, Pugu au Mbagala utakuta lundo kubwa la wachuuzi ambao wameweka vibanda vyao vya mbao au mabati na wengine wakiwa wamepanga bidhaa zao chini huku wakiuza bidhaa mbalimbali kama nguo, vyombo, vyakula nk.

Sio tu huko bali hata maeneo kama Mwenge, Tandika na kwingineko utakuta hali za namna hiyo. Hili lipo hata mikoani mfano Mwanza, Mbeya, Morogoro na sehemu nyingine nyingi.

Kusema ukweli mtindo huu unaharibu maeneo yetu, unaharibu miji yetu na pia unaonesha ni kwa jinsi gani kama taifa tunashindwa kupanga maeneo yetu, watu wetu na hata miji yetu.

Katika kuondoa hili jambo nilikuwa nina mapendekezo yafuatayo:

1. Halmashauri za miji/majiji zinunue maeneo pembeni ya vituo vikubwa vya magali ya usafiri na wayatumie maeneo hayo kujenga masoko ya kisasa yenye miundombinu yote mfano vyoo na hata bank kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.

Mfano Mbezi Mwisho, linunuliwe eneo kubwa ambalo halmashauri wajenge soko la kisasa lenye miondombinu yote mizuri.

Wafanyabiashara wawekwe kwenye haya masoko na waelekezwe na kusimamiwa vizuri juu ya kufanya biashara.

Isiruhusiwe kabisa wafanyabiashara kufanya biashara nje ya maeneo hayo na kama tatizo la wateja litakuwa limeshatatuliwa.

2. Katika vituo vidogo pia vya barabarani, Halmashauri zitenge/zinunue maeneo yenye ukubwa wa wastani. (Hili najua sio lazima lifanyike kwenye vituo vyote bali vinaweza kuchaguliwa vichache tu).

Mfano njia ya Mbagala kwa Dar es Salaam vinaweza kuchaguliwa vituo 5.

Kwenye vituo hivi yajengwe masoko ya saizi ya kati kisasa yenye mpangilio mzuri na miundombinu bora.

Kisha wafanyabiashara waelekezwe na kusimamiwa kufanya biashara kwenye maeneo hayo.

Mamlaka zihakikishe kwenye maeneo hayo kuna usimamizi thabiti wa jinsi ya kufanya biashara.

Labda swali linaweza kuwa je fedha zitapatikana wapi?

Hili suala sio gumu sana kwa sababu zinaweza kutumika fedha za mapato ya ndani halafu miondombinu ikishajengwa kunawekwa utaratibu maalumu wa wafanyabiashara hao kulipia kidogo kwa mwezi au wiki.

Fedha hizo zikusanywe vizuri na kutumika kurudishia mitaji iliyotumika. Baadae zitatumika kufanya maintanance ya maeneo husika.

Je tunaweza kuanzaje?
Katika kutekeleza mpango huu sio lazima serikali ikaanza na halmashauri zote nchini.

Tunaweza anza na chache za mfano kama 2. Then utekelezaji ukiwa vizuri utekelezaji unaendelea kwenye halmashauri nyingine kwa utaratibu maalum.

Asanteni. Naomba kuwasilisha.
 
Mods Naomba mrekebishe heading isomeke

Nini Kifanyike Kuwawekea Mazingira Mazuri ya Biashara Wachuuzi hapaTanzania?
 
Tanzania ni failed state.

Kila mtu ameachwa ajitafutie vyovyote awezavyo ilimradi asiwasumbue watawala.

Hakuna Utaratibu.
 
Mods wafanya maamuzi nchi Hii ni wana siasa- Target ya mada Hii ni wana siasa. Ipelekeni jukwaa la siasa
 
Back
Top Bottom