Nini kifanyike kuwabaini wafanyakazi ambao waliiba mitihani?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,636
Haya ni maoni yangu tu, Baada ya kutumbuliwa wale wenye vyeti feki sasa tuhamie
kwa wale ambao waliiba mitihani au walifanyiwa mitihani, kumbukumbu zangu zina
onesha kuna miaka mitihani hususani ya kidato cha nne ilikuwa inavuja sana.

Pendekezo langu ni kuwa watu wafanye tena mitihani ili kuwabaini ambao waliiba
mitihani hiyo, Sijui wewe mtazamo wako unafikiri ni mbinu gani itumike kuwabaini
walioiba mitihani?
 
Mkuu, hii post asiione mzee utatuua wenzio na akiiona tu............................
 
Duh! hii balaa mpka 'waifu' kanikasirikia kwa post hii.
 
  • Thanks
Reactions: Ftc
Hakuna ushahidi na ndio maana napendekeza itafutwe
mbinu ya kuhakiki kama walifaulu kihalali
Mbinu gani kwa mfano itatumika kujua labda mfano bwana Jose alifaulu kihalali au alifanya ujanjaujanja kufaulu??
 
Haya ni maoni yangu tu, Baada ya kutumbuliwa wale wenye vyeti feki sasa tuhamie
kwa wale ambao waliiba mitihani au walifanyiwa mitihani, kumbukumbu zangu zina
onesha kuna miaka mitihani hususani ya kidato cha nne ilikuwa inavuja sana.

Pendekezo langu ni kuwa watu wafanye tena mitihani ili kuwabaini ambao waliiba
mitihani hiyo, Sijui wewe mtazamo wako unafikiri ni mbinu gani itumike kuwabaini
walioiba mitihani?

Mkuu mbona kama vile baada ya Wewe Kutumbuliwa kwa Vyeti Feki sasa unataka kuwaharibia na wengine nao yawakute?
 
Ni wazi kuwa baraza la mitihani wapo makini sana na kila mwaka wanawafutia mitihani wale wote wanaojaribu kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Hivyo mtu mwenye cheti halali cha NECTA haikubaliki na haiwezekani kuwa alifanya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani.

Kwa ufahamu wangu ni kwamba wale waliokuwa wamefukuzwa kwa kufoji vyeti na kuiba vyeti vya watu ndio hasa waliokuwa wameiba mitihani lakini kutokana na umakini wa baraza la mitihani wakabainika na kufutiwa matokeo na kujikuta wanapata ziro na kukosa vyeti.
Wakaamua kutafuta Plani B ya kufoji vyeti.


Kwa kifupi ni kwamba Hakuna mbinu ya kuwabaini.
Na hakuna Leagal justification kwa hilo suala kwa kuwa hakuna ushahidi unaoweza kumtia mtu hatiani.

Lakini kwa wale wezi wa vyeti wanapaswa kufikishwa mahakamani kwa kufoji document za serikali na kufanya udanganyifu kwa kujitambulisha kwa majina yasiyo yao na kutoa taarifa za uongo kwa umma.

Kuiba mitihani ni suala la wakati huo wa kufanya mtihani na wakati wa kusahihisha mitihani mara nyingi vilaza wanabainika kwa kuwa wanaCopy na kupest. Hao mara nyingi wanafutiwa mitihana.
Kama Baraza la mitihani walishindwa kubaini kuanzia kwenye chumba cha mitihani mpaka wakati wa kusahihisha mitihani basi kuna kila sababu ya kusema kuwa hapakuwa na wizi wala udanganyifu.

Tofauti iliyopo ni kuwa waliofoji hawakupita katika chujio la baraza la mitihani ambalo linaanzia chumba cha mtihani na kumbukumbu zao hazipo. Hao wana kila sababu ya kushitakiwa na baraza la mitihani kwa kufoji document zao na kuzitumia.

Ni sawa na mfano wa mwizi Aitwaye Mshararabwe aliyekamatwa akiwa amebeba TV alipoulizwa akasema nimeinunua dukani kwa Mangi. Na alipoulizwa aonyeshe risiti akakutwa ana risiti .
Waliporudi dukani kwa Mangi ikaonekana kuwa ile TV imeibiwa nyumbani kwa Dusugulukochu na risiti aliyonayo ameifoji na haikutolewa dukani kwa Mangi.
Hapo kuna kosa la wizi na kosa la kufoji documenti.
Tofauti na Mgogondwa aliyekutwa akiwa amebeba TV na risiti yake alipoulizwa akasema ameinunua dukani kwa Mangi . Waliporudi kuhakiki dukani kwa Mangi, Mangi akathibitisha kuwa huyo ni kweli ni mteja wake na walipoomba kitabu cha risiti wakakuta kuwa kuna nakala ya hiyo risiti na imetolewa na kulipiwa kihalali kwa tarehe hiyo.
Na walipofika getini wakakuta kuwa daftari la wale wanaoingia na kutoka dukani limesainiwa kwa jina lililopo kwenye risiti na Kuonekana kuwa aliipita na kupekuliwa getini na kuruhusiwa kupitisha mzigo wake.
Hata kama baadae itabainika kuwa ndani ya droo ya pesa dukani kwa Mangi kuna Noti feki ya Sh. 10000 huwezi kumshitaki Mgogondwa kuwa ndiye aliyeiweka kwa kuwa taratibu zote zilifuatwa ikiwa ni pamoja na kuingiza pesa kwenye mashine ya kubaini pesa halali na feki.
Hapo hasara itabaki kwa Mangi kwa kuwa atakua anatapatapa tu kumpeleka Mgogondwa mahakamani.

Kwa mfano huo hawa watu wawili ni vigumu kuwapeleka wote mahakamani kwani mmoja ana document halali iliyopitia kwenye taratibu zote zilizopo dukani kwa Mangi na mwingine amefoji na hakuwahi hata kufika dukani kwa Mangi siku hiyo.

Kwa hiyo Ndugu Mleta Mada haiwezekani na haitawezekana kuthibitisha kuwa mtu mwenye cheti chake kuwa aliiba mitihani.

Na ukumbuke kuwa serikali imapofanya jambo wamefanya utafiti wa kutosha kuwa wana ushahidi wa kutosha ili wasije wakashitakiwa mahakamani na kudaiwa fidia.
 
Mbinu gani kwa mfano itatumika kujua labda mfano bwana Jose alifaulu kihalali au alifanya ujanjaujanja kufaulu??
Kwa mfano cheti chake kiaonesha ana A saba angalau kumtafutia
maswali ambayo si magumu sana ambay mtu mwenye A kwenye
somo husika hawezi kubabaika sana (walimu wanajua zaidi mbinu hii)
 
Mkuu mbona kama vile baada ya Wewe Kutumbuliwa kwa Vyeti Feki sasa unataka kuwaharibia na wengine nao yawakute?
Inawezekana kabisa si tunataka ufanisi wa kweli, sisi tumekubali
matokeo bado hao wengine, yaani kugushi cheti liwe kosa kubwa
kuliko kuiba mtihani?
 
Kufaulu ni kufaulu tu hajalishi umetumia akili zako peke yako,umeigia au umesaidiwa au umetumia nondo(kibomu) kwenye mtihani unatumia njia zote ili ufaulu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom