Nini kifanyike kuwa na tume huru ya uchaguzi kuanzia sasa na kabla ya 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kifanyike kuwa na tume huru ya uchaguzi kuanzia sasa na kabla ya 2015?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by LOGARITHM, Nov 4, 2010.

 1. LOGARITHM

  LOGARITHM JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Waheshimiwa wana JF na Watanzania Makini:

  Nimeumizwa vibaya sana moyoni mwangu kutokana na mkao na mwenendo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa jinsi ilivyofanyika NGUZO ya kati ya CCM katika UBAKAJI wa demokrasia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu,achilia mbali miaka iliyopita.

  Kwa mtazamo ulio chanya,uchaguzi ulio huru na wa haki ndio njia ya kistaarabu mahali popote Duniani ambapo umma wa nchi husika hufanya maamuzi ya kuiweka serikali madarakani itakayowaongoza kwa matakwa yao kuelekea hatima wanayoitaka.NA HESHIMA YA SERIKALI YOYOTE ILE MBELE YA MACHO YA WATU WAKE INATOKANA NA UHALALI WAKE ILIOPEWA NA UMMA WENYEWE KWA RIDHAA NA UWAZI USIOTIA SHAKA.

  Lakini inapotokea kuwa maamuzi ya UMMA yanatekwa nyara na genge la watu kupitia kitu kiitwacho NEC na kujitwalia mamlaka ya Uongozi kwa hila, DHANA nzima ya DEMOKRASIA na ustaarabu vinakoma na kukosa maana. Nabadala yake kunainuka ghasia, manung'uniko, na uvunjifu wa amani usiokuwa wa lazima kutokea.

  Kwa jinsi tulivyoshuhudia hadi sasa, dhana nzima ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi IMENAJISIKA. Haifai tena kuitwa kwa jina hilo kwa sababu haipo kwa ajili ya TAIFA, bali kama mhuri wa genge la watawala. Ni vema ikabadilisha jina, na ikajiita jina lolote lile linalosadifu wasifu wake halisi ulionyuma ya mapazia.

  Waheshimiwa watanzania, ikiwa hii Tume YAO itaendelea kufanya kazi hadi 2015 kama inavyofanya sasa, JE, KUNA JIPYA LOLOTE LA KUTARAJIA? Nionavyo mimi, hakuna, hata Upinzani ukimsimamisha MALAIKA kugombea,NEC YAO itafanya kama ilivyofanya.

  Great Thinkers, kuna OPTIONS gani zinazoweza kuziba ombwe hili, maana binafsi najua ADUI namba MBILI wa Watanzania kisiasa ni NEC. Namba moja mnamjua. Ninini kinaweza kufanyika katika huu mpito kuelekea 2015?

  Niko tayari kusahihishwa.
   
 2. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi naona the big solution is kuikataa na kusimama kwamba Watanzania wooootee hatuitambui tume hii iliyopo,, na kutaka ifanyike tume itakayo undwa na kamati ya bunge yenye wabunge sawasawa kati ya pinzani na Tawala,, hapo tutatengeneza kitu...
   
Loading...