Nini kifanyike kuutibu uchumi wetu dhidi ya madhara ya korona.

EZZ CHEZZ

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
1,230
1,352
Team.

Jana tumeambiwa na serikali kuwa utalii utaathirika kwa asilimia 75 hivi. Na hii ni kwa assumption kuwa janga hili la corona halitakuwepo baada ya Oktoba! Likiendelea shughuli itakuwa pevu zaidi. Pia iwekwe akilini kuwa madhara yataendelea kuwepo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Nini tafsiri ya hii kitu kwenye uchumi wetu.

Ikumbukwe kuwa mauzo ya nje (exports) ndiyo injini ya kukua kwa pato la taifa lolote lile (economic growth). Hii ni kwa kuwa mauzo ya nje yana tafsiri ya kuuongezea uchumi ukwasi/mtaji wake. Pia ikumbukwe kuwa utalii ndiyo bidhaa inayotuingizia zaidi fedha za kigeni tanzania: usd zaidi ya bilioni 2 kwa mwaka jana sawa na zaidi ya shilingi trilioni 5 za kitanzania. Yaani hata mazao yetu ya biashara yote yakiungana hayafui dafu.

Hivyo basi anguko la asilimia 75 kwa sekta ya utalii litapelekea tafsiri nyingi hasi kwa sekta nyingine pia.

Sasa nini kifanyike.

Naishauri tuelekeze rasilimali zetu (ikibidi serikali ikope nje) kwenye sekta ambazo hutuletea pesa za kigeni lakini ambazo matokeo yake ni ya mara moja. Sekta hizi ni: Kilimo cha mbogamboga, ufugaji, na uvuvi.

Hizi ndizo sekta za uzalishaji Tanzania ambazo fursa yake iko wazi na ni dhahili uhutaji wake (demand) unakua kwa kasi ulimwenguni kote ukichochewa pia na janga hili.

Mkakati.

Serikali mara moja iangalie namna ya kuwawezesha wazalishaji ambao tayari wako field (wazoefu). Yaani kama mkulima/wakulima wana greenhouse 1 kwa mfano, serikali iwasaidie kufanya expansion kubwa na ya haraka.

Vivyohivyo ikiwa mfugaji ana bwawa moja la samaki, awezeshwe akue haraka. Hii ifanyike kwa uangalifu na udhibiti mkubwa ili pesa ya umma isichezewe.

Sipendekezi pesa ya mkopo nyakati kama hizi za majanga kupewa wazalishaji wapya ili kupunguza uwezekano wa kushindwa (risk). Bali watarajiwa hawa wanaweza "kumezwa" kwa muda na wazoefu ili baadaye na wao wawe na ujuzi toshelezi.

Hitimisho.

Hii itapelekea kuziba au kupunguza ombwe la mapato ya nje litokanalo na kudorora kwa utalii. Kuna viashiria kuwa baadhi ya nchi zimechukua hatua hii tayari. Juzi tumemwona waziri mkuu wa Ethiopia akizindua bustani kubwa za mbogamboga. Pia rais wa Korea ya Kaskazini sasa hazindui tena makombora bali anazindua kiwanda cha mbolea. Akili ku-mkichwa!

Ombi maalum.

Uzi huu ni kwa ajili ya great thinkers kujadili hoja hii. Tafadhali usiweke siasa za rejareja hapa.

Nawasilisha.







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom